Kwanini watu wenye roho nzuri huwa hawatajiriki?

Kwa sababu huwa tunagawa vitu vingi vya thamani kubwa bure wakati wengine huviuza.. Nilishawahi kwenda kwa mwanasheria mmoja kumuomba anigongee muhuri kwa sh elf tatu akakataa kata kata hadi niwe na elfu tano.. Unaona sasa, mtu anakunyima tu wino kisa umepungukiwa buku mbili je ni kitu gani kingine anaweza kukupa bure?
Mmezoea kuwalalia walimu wanaowafundisha watoto wenu tuition kwa mkopo.
 
Ubarikiwa familia zao

Baba angu alikuwa na roho nzuri sana hata alipokufa mpaka leo sijawahi kuwa na shida,watoto wote hatujawahi kupata shida katika maisha yakusema hii ni shida kubwa.Wote tuna maisha mazuri sana ..

Mimi binafsi nimejifunza kupunguza kugawa ukubwani lakini toka nimeanza kutoa pesa na vitu sijawahi kufilisika hata siku moja na ndo Kwanza naongeza mali Kila siku...

Mtu akitoa kitu ni kwasababu ni tajiri yaani anazo hizo mali za kutoa... ukiona hutoi kbs ni kwasababu huna Cha kutoa. Sasa mtu anataka awe na billions za pesa bank halafu watu wako wa karibu Wana shida, Pesa zote za nini!

Halafu mtoaji Ana lala usingizi mnono usiku...
Hongera Sana mkuu...Mimi pia dingi ni mtoaji Sana mzuri wa misaada toka nazaliwa namuona..kastaafu bado anatoa balaa had unamsema..ila Nawaona anabarikiwaga Sana yeye na mkewe... Maisha yao kwakweli huwez amini km ni wastaafu .wanaishi kifahari! Dah ..God bless them!
Ila Kuna watu wakisaidia mioyo yao inajawa amani na Neema zaidi ..they say "When Grace locates you it breaks protocols". Ndo ww na ndugu zako mnapitia hapa sasa!♥️
 
Ila binadamu bwana..sijui kwanini hatunaga shukrani.
 
na nadra sana kuzeeka,wengi hufa mapema.

hawa hunifanya niamini Mungu ana matumizi huko na watu wema.

angalia wapuuzi wanavyopuyanga.mpaka wanatoboa 90 huko.

Ha ha ha kama yule mzee wa rwanda kabuga alieagiza kontena la mapanga ya kuchinja watu.. yupo hai mpaka leo.. kakamatwa na miaka zaidi ya 90 kajificha ufaransa
 
Back
Top Bottom