Wazee wetu wa zamani walidumu sana katika ndoa zao labda kwasababu wanawake walifundishwa kuwatii waume zao huku mfumo dume ukiwa umeshika hatamu katika jamii zetu.
Lakini sasa imekuwa tofauti kwani kumeonekana kukiwa na wimbi kubwa la talaka na pia wanawake wengi kukosa bahati ya kuolewa labda kwa upande mwingine hizi zinaweza zikawa sababu
Moja, ndoa za kulazimisha zimepungua, ikumbukwe zamani mwanamke alikuwa anatafutiwa mchumba wa kuolewa naye na wazazi wake na kulazimishwa kuolewa naye hata kama hampendi, hii ilisababisha wasichana wengi kupata wenza kipindi hiki, tofauti na sasa ambapo tunajichagulia wenyewe na tunatafuta wenyewe watu wa kuwaoa au kuolewa nao.
Lakini pia,kuanzishwa sera mbalimbali za kumuunga mkono mwanamke, mfano msemo wa hamsini kwa hamsini. Kupitia sera hizo wanawake wameweza kusoma kupata ajira na kuwa watu wakubwa na maarufu kupita waume zao, ni suala la kujiuliza mkeo akiwa na cheo kikubwa kuliko wewe heshima itakuwepo?
Lakini pia, kujipatia kipato kumewafanya wanawake wengi wasipitie manyanyaso kutoka kwa waume zao, hivyo akipata msukosuko kidogo anaona njia rahisi ya kuepuka Hilo Ni kutalikiana.
Lakini wanaume pia wamejikuta wakishindwa kuanzisha mahusiano na wanawake wenye pesa wakiogopa kunyanyasika. Cha kuelewa ni kwamba, sasa mambo yamebadilika na tukubali au tukatae lazima tuishi kwa kutegemeana na kuheshimiana ukimjali mwenza wako na kumchukulia kuwa yeye ni bora na ni muhimu katika maisha yako itasaidia kupunguza talaka zisizo na msingi lakini pia ndoa zitakuwepo.