Kwanini watu wengi sasa suala la ndoa wamekuwa wakilisikilizia kwenye bomba?

Ornate

Member
Jul 13, 2021
26
33
Wazee wetu wa zamani walidumu sana katika ndoa zao labda kwasababu wanawake walifundishwa kuwatii waume zao huku mfumo dume ukiwa umeshika hatamu katika jamii zetu.

Lakini sasa imekuwa tofauti kwani kumeonekana kukiwa na wimbi kubwa la talaka na pia wanawake wengi kukosa bahati ya kuolewa labda kwa upande mwingine hizi zinaweza zikawa sababu

Moja, ndoa za kulazimisha zimepungua, ikumbukwe zamani mwanamke alikuwa anatafutiwa mchumba wa kuolewa naye na wazazi wake na kulazimishwa kuolewa naye hata kama hampendi, hii ilisababisha wasichana wengi kupata wenza kipindi hiki, tofauti na sasa ambapo tunajichagulia wenyewe na tunatafuta wenyewe watu wa kuwaoa au kuolewa nao.

Lakini pia,kuanzishwa sera mbalimbali za kumuunga mkono mwanamke, mfano msemo wa hamsini kwa hamsini. Kupitia sera hizo wanawake wameweza kusoma kupata ajira na kuwa watu wakubwa na maarufu kupita waume zao, ni suala la kujiuliza mkeo akiwa na cheo kikubwa kuliko wewe heshima itakuwepo?

Lakini pia, kujipatia kipato kumewafanya wanawake wengi wasipitie manyanyaso kutoka kwa waume zao, hivyo akipata msukosuko kidogo anaona njia rahisi ya kuepuka Hilo Ni kutalikiana.

Lakini wanaume pia wamejikuta wakishindwa kuanzisha mahusiano na wanawake wenye pesa wakiogopa kunyanyasika. Cha kuelewa ni kwamba, sasa mambo yamebadilika na tukubali au tukatae lazima tuishi kwa kutegemeana na kuheshimiana ukimjali mwenza wako na kumchukulia kuwa yeye ni bora na ni muhimu katika maisha yako itasaidia kupunguza talaka zisizo na msingi lakini pia ndoa zitakuwepo.
 
Wanaume wengi mme kuwa mkitizama wanawake kwa matarajio makubwa na kuacha kabisa kujitazama wenyewe kwanza.
"Matarajio makubwa na kuacha kabisa kujitazama wenyewe kwanza"

Kwa kauli hij itoshe tu kusema hiki kizazi kinakimbia kwa kasi sana ya kulea vitoga
 
Mwanamke halisi humpenda mwanamke halisi. Sisi wanaume tujitambue Kwanza SSI no jina Nani na ipi role yetu ktk ndoa. Hats hyo zamani ndoa zilidumu coz enzi hzo men were real men.
 
Tatizo linaanzia kwenye kusumbukia 'vilivyoumbwa' na kumpuuza 'aliyeviumba'.Huu ndio mzizi mkuu, hizo sarakasi ni matokeo tu.
 
Ndoaa sio kipaumbele siku hizi.

Kikubwa kua na watoto basi. Wanawake wengi siku hizi wanapenda zaidi maisha ya kua huru na kufurahia maisha.

Wadada wengi nakutana nao hawana mpango wa kuolewa, wengi wanatafta wanaume wa kuwazalisha na walee watoto pamoja kama co-parents na sio wife and husband.

Mimi mwenyewe mpango wa kuoa sina, hapa nimepanga mwakani nizae watoto 2 na wanawake 2 tofauti halafu nitulir kula maisha.

Usiwe stressed na mambo ya ndoa.
 
hizo takwimu sijui mnapata wapi

kila weekend naona harusi tu
watu wanaoana kuanzia ijumaa mpaka jumapili
Watu tuna kadi za michango mpaka tumeacha kupokea simu wala kusoma msg za watu whatsaap...kila akitizama anakutana na tiki ya kijivu!!!
 
Back
Top Bottom