Deinstein 01
JF-Expert Member
- May 12, 2024
- 2,087
- 3,916
Habari Wakuu!
Kwenye haya maisha wapo watumwa na wapo watu walio huru. Utumwa ninao uzungumzia hapa si ule ambao tulifundishwa mashuleni bali ni ule wa mtu kuchukua maamuzi kutokana na hisia zake au tamaa zake au fikra za mtu mwingine bila ya kutumia akili zake na utashi wake mwenyewe.
Na watu wengi bado wapo kwenye kundi la utumwa kwakuwa hao watu hawaishi
kwa miongozo yao wenyewe. Najua hata mashuleni tulifundishwa ya kuwa nchi iliyo huru huwa na katiba yake mwenyewe ambayo ndo ina miongozo ya jinsi nchi itakavyojiendesha.
Vivyo hivyo, hata mtu aliye huru huwa na miongozo aliyojiwekea ambayo inamsaidia kuishi maisha yake kwa amani na furaha. Naam siku zote mtu mwenye furaha ni yule aliye anayeishi maisha yake kwa misimamo yake mwenyewe na si anayeishi kwa kumtazamia au kumridhisha fulani.
Na si lazima miongozo uliyojiwekea ikubaliwe na watu wanaokuzunguka. Mfano mimi nina kanuni yangu inayosema "Men should never fall in love, falling in love is for women" mara nyingi nikisemaga hivi watu huwa wananiponda ila mimi sijali kwa kuwa naona hii kanuni ina manufaa kwangu.
Kumbuka ya kuwa hata katiba ya nchi huwa inapitia maboresho vivyo hivyo hata miongozo uliyojiwekea unaweza ukairekebisha kulingana na experience na challenges ambazo unapitia kwakuwa si kila mtazamo ulionao ni sahihi.
Hivyo basi, ningependa kuwaasa watu wawe na muda wa kutafakari juu ya maisha yao ili waweze kuunda misimamo na miongozo itakayowanufaisha maisha yao ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Yangu ni hayo tu!