Kwanini watu wanasherekea siku zao za kuzaliwa?

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
4,410
5,807
Habari zenu wakuu wa hapa jukwaanii.

Kila siku huwa najiuliza kwa nini watu wengi wanaingia katika utamaduni ambao binafsi nauona kama utamaduni wa kigeni (UZUNGU) kwa kufanya sherehe au tafrija kwa furaha ya siku ya kuzaliwa sijui kama watu hawa huwa wanajua kuwa kila siku mpya mwanaadamu hupunguza siku za kuishi na kulisogelea kaburi sasa ajabu watu hawa huwa wanafurahia kufa?, Au hufanya hiyo bila kujua maana umri haupungui Bali unazidi kila siku.
Asante

kalidegree
 
KWA NCHI HII UKIMALIZA MWAKA HUJAFA, HUJAPEWA KESI YA UCHOCHEZI, HAUPO JELA LAZIMA USHEREKEE BIRTHDAY *****
4bb5d1229ada7f836f0f7a7340c461e5.jpg
 
Labda pia nikurudishie swali wewe, kwanini huwa unasherekea kila inapofika tarehe moja ya mwaka mpya?
 
Duniani kuna vitu vitatu vinavyokamilisha neno maisha kuzaliwa ,kuoa au kuolewa na kufa
na maisha ni kipindi cha kati ya kuzaliwa na kifo kwa kiumbe hai chochote ,hasa binadamu

so vipindi hv kila kinapokuja ni lazima kusherekea
 
Sio wote, ila wanafanya Just for fun, kama una hela, una marafiki, una furaha..unafanya tu hizo mambo ku enjoy zaidi
Halafu mambo ya kusema sio utamaduni wa mwafrika kwani mwafrika ameiga tamaduni ngapi za kigeni hadi mpaka sasa?
Watu wanaoweza kujivunia utamaduni wao labda waarabu, sio waafrika, waafrika hawana utamaduni!!
 
Habari zenu wakuu wa hapa jukwaanii.

Kila siku huwa najiuliza kwa nini watu wengi wanaingia katika utamaduni ambao binafsi nauona kama utamaduni wa kigeni (UZUNGU) kwa kufanya sherehe au tafrija kwa furaha ya siku ya kuzaliwa sijui kama watu hawa huwa wanajua kuwa kila siku mpya mwanaadamu hupunguza siku za kuishi na kulisogelea kaburi sasa ajabu watu hawa huwa wanafurahia kufa?, Au hufanya hiyo bila kujua maana umri haupungui Bali unazidi kila siku.
Asante

kalidegree
cha kushangaza mtu anasherehekea siku yake ya kuzaliwa lakini ukimwuliza kwa sasa umetimiza miaka mingapi anaanza kujishaua haweki wazi umri,nafikiri haina maana
 
sasa wewe hapo huoni kama unaposema kuwa siku yako ya kufa inakaribia kila siku mpya inapoanza! ndio unapopata sababu ya kusherekea siku yako ya kuzaliwa inapofika ikikukuta bado upo hai?
 
Sio wote, ila wanafanya Just for fun, kama una hela, una marafiki, una furaha..unafanya tu hizo mambo ku enjoy zaidi
Halafu mambo ya kusema sio utamaduni wa mwafrika kwani mwafrika ameiga tamaduni ngapi za kigeni hadi mpaka sasa?
Watu wanaoweza kujivunia utamaduni wao labda waarabu, sio waafrika, waafrika hawana utamaduni!!
Sijasema wote ni baadhi tu
Kama wewe ndio mnaamua
Kufanya upuuzi huo kuwa muhimu
Mnatuaribia watoto.

Maana kila MTU siku hizi ni Mzungu asie jitambua.
 
cha kushangaza mtu anasherehekea siku yake ya kuzaliwa lakini ukimwuliza kwa sasa umetimiza miaka mingapi anaanza kujishaua haweki wazi umri,nafikiri haina maana
Haina maana.
Wanapotea lakini hawa elewi
Kabisa.
 
sasa wewe hapo huoni kama unaposema kuwa siku yako ya kufa inakaribia kila siku mpya inapoanza! ndio unapopata sababu ya kusherekea siku yako ya kuzaliwa inapofika ikikukuta bado upo hai?
Kwa mungu sio kwa Mzungu
Habari ya kifo ni nzito sana
Ilikuwa ni fursa ya kutafakari
Huko tuendako na si kufurahia.
 
Kwa mungu sio kwa Mzungu
Habari ya kifo ni nzito sana
Ilikuwa ni fursa ya kutafakari
Huko tuendako na si kufurahia.
Ambao wanatenda yaliyo mema, wanauogopa sana ulimwengu wanatamani siku yao ifike wakakae mahali salama.
Ila wanaoupenda ulimwengu, hawataki kusikia habari ya kifo kabisa.
 
Duniani kuna vitu vitatu vinavyokamilisha neno maisha kuzaliwa ,kuoa au kuolewa na kufa
na maisha ni kipindi cha kati ya kuzaliwa na kifo kwa kiumbe hai chochote ,hasa binadamu

so vipindi hv kila kinapokuja ni lazima kusherekea
Tambua kama umri unakutupa mkono unazidi kulisogelea kaburi
 
Back
Top Bottom