Kwanini watu wanaiponda sana wilaya ya Rombo kwa ulevi lakini bado kuna maendeleo?

mcTobby

JF-Expert Member
Feb 16, 2018
373
1,000
Unajua Hii wilaya kwanza kijiografia ipo mwinuko kati ya mita 1300 hadi 2200. Kuna hali nzuri sana ya hewa hilo halina ubishi .

Watu wanaposikia hii wilaya kitu cha kwanza wanajua watu wa huko ni walevi choka mbaya kiasi kwamba hakuna maendeleo yeyote. Ila laiti wangejua Hii wilaya kila mtumishi wa umma aliyeajiriwa iwe kwenye shule , benki au polisi hawatamani kuhama wasingeibeza.

Ni kweli pombe inanyweka tena sana kuanzia pande za kikelelwa mpaka mamsera mashati ,usseri ndani ndani pombe inanyweka ila watu wanapadis ohooo Rombo hakuna maendeleo kisa ulevi.

Na huku kunywa pombe kunachangiwa na upatikanaji rahisi wa malighafi ya kutengeneza pombe ya mbege ambazo ni ndizi pamoja na hali ya hewa (baridi) ila maendeleo yapo na watu wapo wanakimbizana kuitafuta shekeli kwa udi na uvumba. Iwe ni kwenye biashara kilimo n.k mfano Kilimo cha viazi Rongai ,mahindi japo sio sana n.k.

Viwanda vya mbao vipo kuanzia kikelelwa tarakea hapo kwa maulid peleka hadi Mashima usseri n.k. kwa takwimu za haraka haraka za pale ofisi ya Rongai kuna karibia viwanda 200 ambavyo vipo registered katika kuchakata mbao.

Kama msitu upo Norh Kilimanjaro forest plantation wenye almost hectare 8000 na point.
Utalii wa mlima Kilimanjaro n.k.

Kwa vile tupo mpakani hapa siku za weekend wakenya wanakuja ku spend na familia zao kupata kitimoto ,bia au ugali samaki snow cape AU resort inn . Kwa kifupi wakenya kutoka kwenye miji ya kimana ,oloitoktok ,illasit n.k

Sehemu yao ya kujivinjari ni tarakea ,Mashima au mashati huko ..maana huku bia ni rahisi sana ukilinganisha na kwao. Kwa kifupi kiuchumi wilaya ya Rombo inajiweza. Msipadis sana kama hamjawahi fika naomba mfike .

Haters karibuni kwa mapovu
 

luambo makiadi

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
7,956
2,000
Huwezi ukaupata ukweli wa nyumba kutoka kwa mwenye nyumba..
Rombo ni wilaya ya kwanza tz vijiji vyake vyote kuwa na umeme 100%.

Rombo Hakuna nyumba ya nyasi hata moja ,route za mabasi ya mikoan kuja ROMBO ni nyingi mno hii inaashiria mzunguko mkubwa wa pesa.
  • Rombo_dodoma(shabiby)
  • Rombo mwanza(mghamba)
  • Rombo moro (Bm)
  • Rombo singida(mtei exp)
  • Pia bus za ROMBO Dar Ni zaidi ya 10
 

luambo makiadi

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
7,956
2,000
Rombo ni wilaya yenye maendeleo sana kwanzia makazi bora, miundombinu hadi pesa.

Rombo ina mzunguko mkubwa sana wa pesa.

Karibia kaya zote rombo nyumba Zina umeme haya Ni maendeleo makubwa.

Viwanda Ni vingi kwanzia viwanda vya maji SEQUA ,viwanda vya mafuta mashati nk.

the beautiful ROMBO​


FB_IMG_16127922676068706.jpeg
 

ligend

JF-Expert Member
Oct 14, 2019
449
1,000
bila shaka hapa ni mashati
Rombo ni wilaya yenye maendeleo sana kwanzia makazi bora, miundombinu hadi pesa
Rombo ina mzunguko mkubwa sana wa pesa
Karibia kaya zote rombo nyumba Zina umeme haya Ni maendeleo makubwa
Viwanda Ni vingi kwanzia viwanda vya maji SEQUA ,viwanda vya mafuta mashati nk
the beautiful ROMB
 

ligend

JF-Expert Member
Oct 14, 2019
449
1,000
Rombo ni wachapakazi sana na sehemu iliyokamilika ktk kila sector na kikubwa ni ule mpaka na Kenya unafanya mzunguko wa pesa uwe mkubwa sana hasa pale Tarakea na pia ni wilaya iliyo na wageni wengi sana hasa wasambaa na wapare hivyo huchochea maendeleo.
 

mwenye shamba

JF-Expert Member
May 31, 2015
883
1,000
Hiyo Rombo yako nimekaa kama mtumishi zaidi ya miaka minne,naijua nje ndani,mnajimwambafy sana as if kuna la maana sana,huku geita rombo yako yote nakushushia kata ya lwamgsa tu mnakaa chini.
 

luambo makiadi

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
7,956
2,000
Hiyo Rombo yako nimekaa kama mtumishi zaidi ya miaka minne,naijua nje ndani,mnajimwambafy sana as if kuna la maana sana,huku geita rombo yako yote nakushushia kata ya lwamgsa tu mnakaa chini.
Weee geita ipi? Geita imejaa umaskini mkali ukitaka kujua umaskini wa eneo angalia makazi tu, ulishawah ona nyumba ya nyasi hata moja ROMBO? Ila geita yako 40% Ni nyumba za nyasi

Geita Ni mkoa wa 3 kwa umaskini Tanzania unasema nn?

Ukibisha nitaendelea kukuumbua

808706694.jpeg
 

Maili tatu

JF-Expert Member
Aug 8, 2020
472
1,000
Mtoa mada amesema kweli kabisa, kwa ujumla rombo na maeneo mengine ya moshi ni mazuri mnooo, yani migombani huko unakuta mijumba ya maana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom