Kwanini watu waliofika Chuo Kikuu hawawezi kujieleza kwa lugha moja?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,735
Wengi hawawezi kuongea kiswahili mfululizo bila kuchanganya na Kiingereza.
Na wengi zaid hawawezi kuongea Kiingereza kwa mfululizo bila kukwama njiani na wakati mwingine wanachanganya na Kiswahili au wanarudi kwenye Kiswahili tena.

Mfano: Malumbano ya hoja ITV wengi wakiwa ni wanafunzi wa vyuo lakini Muda mwingi uliishia kwa Mtangazaji kuwasisitiza waongee Kiswahili bila kuchanganya Lugha.Sasa hii kasumba inaingia mtaani, karibu wote tunaelekea huko. Hata humu JF tumo wengi wa namna hiyo.

Swali...
Je? Kuna haja ya KISWA-ENGLISH kuongezwa kuwa Lugha ya tatu ya taifa Tanzania? Au tuzitendee haki Lugha zetu hizi mbili zisizoingiliana kiasili.
 
you know lugha ya english is simple and imejifupisha ila ina maana ndeeefu neno fupi
ina leta raha sisi peoles wa Tanzania

teh teh teh sasa hapo sijui utaelewaje mwenzangu na mimi wa ST kayumba

ni sheeder kiswa english hiki.
 
you know lugha ya english is simple and imejifupisha ila ina maana ndeeefu neno fupi
ina leta raha sisi peoles wa Tanzania

teh teh teh sasa hapo sijui utaelewaje mwenzangu na mimi wa ST kayumba

ni sheeder kiswa english hiki.
hahahahaa
 
Watu kujua lugha nusunusu mtu unaweza kukosa neno mbadala unaamua kuweka neno la lugha nyingine ili upate kueleweka vizur...
Pia kuna maneno mengine ya kiswahili kutamka huwa ni marefu hivyo ilikufupisha mtu anatumia kingereza kama ataona neno hilo kwa kingereza ni fupi...
Pia kingine ni mazoea tu ukijizoosha hivyo mwisho wa siku una kuwa addicated..:D:D:D:D
 
Watu kujua lugha nusunusu mtu unaweza kukosa neno mbadala unaamua kuweka neno la lugha nyingine ili upate kueleweka vizur...
Pia kuna maneno mengine ya kiswahili kutamka huwa ni marefu hivyo ilikufupisha mtu anatumia kingereza kama ataona neno hilo kwa kingereza ni fupi...
Pia kingine ni mazoea tu ukijizoosha hivyo mwisho wa siku una kuwa addicated..:D:D:D:D
Unapo wakilisha mada ni vizuri kutumia lugha moja hasa ile inayoeleweka na wengi. Kuchanganya lugha kunaleta utata.
 
Hahahahah hawana tofauti na Hamo Rapa anaesema yeye ni Strong Woman....
Hamorapa alikuwa anajua ila utamkaje ukazingua watu strong human,strong woman. Kila nchi kabila wanautamkaji wao,usitegemee mhaya akitamka neno ni sawa na msukuma la sivyo angalia kingereza cha mhindi,mwarabu,mtz,mkenya,mwingereza na mmarekani
 
Wewe unatarajia nini kama walimu wo-o-te wa CHUO KIKUU cha Nelson Mandela Arusha kimekutwa na waalimu 49 FEKI? Hapo ni kwenye chuo kikuu ! Walimu feki wanafundisha wanafunzi na kuwapa vyeti halisi (original). Hivyo vyeti vitakuwa halisi kweli? Elimu yetu sisi Watanzania imekuwa feki. Watu wanaomaliza vyuo vikuu hawajui vizuri sio Kiingereza tu, hata Kiswahili. Unamsikia mtangazaji (aliyemaliza chuo kikuu) akisema 'katika ajali ile watu 35 'waliweza' kufa ! Kwenye lugha ya Kiswahili unatakiwa useme mtu 'ameweza' kama tu amefanya jambo ambalo alikuwa anajaribu kulifanya. Unaposema mtu ameweza kufa kwenye ajali una maana alikuwa anajaribu kupata ajali afe? Unaweza pa kusoma kwenye gazeti (linalosimamwa na mhariri mwenye Shahada ya Uzamili) habari ambayo imeandikwa 'lile 'roli' (sio lori) limemngonga mtu na kufa. Kwa maana hiyo, kilichokufa ni lori sio mtu. Tena lori limeandikwa 'roli' Tanzania tuna tatizo kubwa sana na 'kumiliki' lugha (mastery of language)

Tafuta kanda ambazo zina hotuba za Mwalimu Nyerere. Kamwe hutasikia amechanganya lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Lakini hata waheshimiwa wabunge wetu sasa wanachanganya hizo lugha mbili. Hayo ni matokeo ya elimu ambayo haiko sawa. Kama mtu anaenzi Kiswahili, atajaribu kila awezalo asikichanganye na Kiingereza. Kwa hiyo japo kuna watu wengi sana wanasema eti masomo yawe yanafundishwa kwa Kiswahili, hiyo lugha yenyewe haijulikani vizuri na Watanzania wengi.
 
Unaona ! Hata kwenye 'post' hiyo hapo juu mimi mwenyewe nilyezungumzia Kiswahili feki nimeandika sentensi feki. Ngoja nichanganye na Ung'eng'e. I am sorry !
 
Back
Top Bottom