Sababu 3 Kwanini Magufuli Anatumia Kiswahili kwa Wageni na Ngambo... na maana yake kwetu...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,362
39,083
1112688

(picha na New Zimbabwe.com)​

Na. M. M. Mwanakijiji
Inawezekana zipo sababu kubwa tatu ambazo zimemfanya Rais Magufuli kuanza kutumia lugha ya Kiswahili anapokutana na wageni wa kigeni pale Ikulu au anaposafiri kwenda ng’ambo. Sababu hizo zikieleweka zinaweza kutudokeza kidogo kwanini yumkini Rais amefikia uamuzi huo. Naomba kupendekeza tu kuwa tunaweza tusizikubali sababu hizi na inawezekana zikaonekana si za msingi lakini zinaweza kuwa na maana kubwa kitaifa.
Sababu hizi tatu zaweza kuwa ni:
 • Ameamua kuitangaza na kuikuza lugha Kiswahili kimataifa.
 • Hajiamini kujieleza kw aufasaha katika lugha ya Kiingereza
 • Sababu zote mbili za a na b.
Kwa vile hakuna chombo chochote cha serikali kilichotoa taarifa za uamuzi na sababu ya Rais kutumia lugha ya Kiswahili kwa namna hii basi ni haki ya Watanzania kukisia sababu hizi hadi itakavyoelezwa vinginevyo. Ni bahati mbaya na makosa kuwa vyombo ambavyo vingeweza kutoa taarifa hizo hajifanya hivyo. Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Wizara ya Habari na Utamaduni, au hata Ofisi ya Rais wenyewe wangeweza kuwaeleza tu Watanzania sababu ya uamuzi huu. Kwa vile hawajafanya hivyo, na sidhani kama wanampango wa kufanya hivyo basi sisi wengine tumejipa uhuru na haki ya kudhania. Naomba niziangalie sababu hizi tatu na maana yake kwa taifa.
 • Ameamua kuitangaza na kuikuza lugha ya Kiswahili kimataifa.
Lugha ya Kiswahili ni lugha kubwa, inayoeweka na watu wengi zaidi Afrika kuliko lugha nyingine yeyote ya Kiafrika. Karibu nchi 14 za Kiafrika zina wazungumzaji wa aina ya lugha ya Kiswahili. Ukichukulia tu kwa haraka haraka kuwa watu wa Tanzania na Kenya peke yake ambao wanaelewa Kiswahili kwa kiasi unaona kuwa tayari karibu watu milioni 100 wanaelewa kwa namna Fulani lugha ya Kiswahili. Miaka ya karibuni tayari mataifa mengine ya Kiafrika yameanza kukipokea Kiswahili kama lugha rasmi mojawapo.
Hivyo, Rais anapotumia lugha ya Kiswahili anakipa jukwaa kubwa zaidi kuliko huko nyuma. Tulizoea kwa muda mrefu kuwa marais wetu wanapoenda nje hata kwa majirani zetu wanalazimika kuzungumza lugha ya Kiingereza. Kwamba, sisi Waafrika hatuna lugha inayotuunganisha watu (lingua franca) wote isipokuwa zile lugha za kigeni. Kiswahili kama lugha ya Kiafrika ni rahisi kutamkika kwani misingi yake ya maneno iko karibu katika lugha zote za kibantu na kwa kiasi kikubwa lugha nyingine za Kiafrika.
Kwa kutumia lugha ya Kiswahili Rais anaipa heshima lugha yetu; heshima ambayo inastahili. Hivi majuzi wakati Rais Donald Trump wa Marekani alipoenda Japan tuliona jinsi Waziri Mkuu wa Japan Abe Shinzo akizungumza Kijapani. Hili limetokea hata kiongozi huyo wa Marekani alipokutana na Rais wa China au wa Urusi. Kibarua ilikuwa ni kwa wakalimani kutafrisi kutoka lugha moja kwenda nyingine. Hili halikuwa jambo la ajabu.
Hivyo, pamoja na kuitangaza na kuikuza lugha hii Magufuli anaipa heshima ambayo inastahili. Kwamba, wazungumzaji wa Kiswahili hata wakiwa na vyeo vya juu kabisa wasijione duni mbele ya wageni. Mmoja wa washairi wakubwa kabisa – kama siyo mkuu kabisa – katika historia ya nchi yetu marehemu mzee Shaaban Robert aliwahi kuandika utenzi wake mashuhuri wa “Titi la Mama li Tamu”. Ubeti wake wa kufungulia Shaaban Robert aliandika:
Titi la mama litamu,hata likiwa la mbwa,
Kiswahili naazimu,sifayo iliyofumbwa,
Kwa wasiokufahamu,niimbe ilivyo kubwa,
Toka kama mlizamu, funika palipozibwa
 • Hajiamini katika kujieleza katika lugha ya Kiingereza
Kwa wale ambao tumepata nafasi ya kumsikia Rais Magufuli akizungumza Kiingereza ni wazi kuwa tunaweza kuona akifanya makosa ama katika matamshi, muundo au fasihi ya lugha ya Kiingereza. Makosa ambayo Magufuli anayafanya wengi ambao wanajifunza lugha ya Kiingereza au wamejifunza lugha hiyo ukubwani wanaweza kujikuta wakiyafanya. Hili ni kweli pia kwa wazungumzaji wa asili wa lugha ya Kiingereza. Makosa haya yanaitwa “common mistakes” au “Common errors” katika lugha ya Kiingereza.
Makosa haya ya lugha si ya kipekee kwa lugha ya Kiingereza. Kwa mtu anayejifunza lugha ya Kiswahili au lugha nyingine yeyote anaweza kujikuta akiyafanya mara kwa mara. Ama katika kutamka maneno au katika muundo na sarufi ya lugha hiyo. Kwa mfano kwa watu wengi wanaojifunza Kiswahili wanaweza kushangaa kuwa lugha yetu haina sana msisitizo katika herufi Fulani kama ilivyo katika lugha nyingine nyingi.
Sasa Magufuli inawezekana ameona watu wanamsema au anaonekana kama kituko kwa wageni pale anapovunja lugha ya Kiingereza hasa kwa vile ni msomi wa PhD. Hili linatuleta kwenye hoja nyingine ndani ya hoja hii kuwa kuwa msomi wa eneo Fulani haina maana mtu anaimudu lugha ya Kiingereza. Kiingereza cha kisomi (academic writing) mara nyingi si kigumu kama kile cha kujieleza. Hii ni kwa sababu lugha ya kisomi ina maneno yake na ni rahisi kufuata. Si kila msomi anaweza kuandika riwaya ya Kiingereza au insha ya kijamii kwa Kiingereza bila kupata shida ya maneno. Hili linatokea hata kwa wasomi kutoka nchi nyingine ambazo hawazungumzi Kiingereza kwa asili (native English speakers).
Sasa kama Magufuli anaona hajiamini kwa sababu ya makosa ya mara kwa mara – ambayo si ya ajabu sana – inawezekana kuamua kuzungumza Kiswahili ni salama na bora kwake kuliko kujionesha udhaifu wake wa lugha.
Ikumbukwe hili si tatizo la Magufuli tu. Wapo watu wetu wengi tu ambao wanaweza kuchanganya maneno ya Kiingereza kwenye Kiswahili (Kiswakinge) lakini hawawezi kuunda kauli zinazoeleweka za lugha ya Kiingereza. Na wengine hata Kiswahili kilichonyoka (kisichonganyana) na Kiingereza hawawezi kukitumia. Tumeona mambo haya Bungeni ambapo sharti mojawapo ni kuwa mgombea awe anaweza kujua lugha ya Kiingereza au Kiswahili. Tumeona watu wanaoomba kugombea Bunge la Afrika ya Mashariki wengine wakivunja maneno hadi unasikia kujing’ata ulimi! Lakini watu wale wale wanaweza kujieleza kwa Kiswakinge!
 • Mchanganyiko wa Sababu 2 za Kwanza
Inawezekana kabisa kuwa Rais ameamua kufanya hivi kutokana na sababu zote mbili kwamba anataka kuienzi, kuiheshimu na kuipa jukwaa kubwa lugha ya Kiswahili lakini vile vile yeye mwenyewe hayuko mzuri sana (kama Watanzania wengine wengi) kutumia lugha ya Kiingereza kwenye hadhara. Kama hili ni kweli basi hakuna aibu katika yote mawili; yote mawili yanaweza kuwa sababu za kutosha tu.
Hii ina Maana gani kwa taifa?
Swali kubwa la msingi ni je jambo hili lina maana gani kwetu kama taifa? Je, ina maana sasa Watanzania wasijifunze Kiingereza kabisa na wote wajifunze kila kitu kwa Kiswahili? Je, ina maana lugha ya Kiingereza si muhimu tena? Naomba kupendekeza mambo yafuatayo:
 • Ikumbukwe kuwa kama taifa na kama mtu mmoja mmoja hatuwezi kukwepa matumizi ya lugha ya Kiingereza. Kwanza kwa sababu mfumo wetu wa kiserikali unafuata kwa kiasi kikubwa mfumo wa Kiingereza lakini pili ni kuwa kwa vile lugha ya Kiingereza ndio lugha inayoiunganisha dunia. Sasa hivi ni vigumu kwenda mahali popote na kukosa kabisa mtu anayejua Kiingereza. Ni rahisi kupata mtu anayejua Kiingereza kuliko mtu anayejua lugha nyingine yeyote. Hivyo, Kiingereza hakikwepeki.
 • Kwamba watu wetu wanapata shida kumudu lugha hii ni matokeo ya mambo mengi. Yawezekana kwa kiasi kikubwa ni suala la elimu na mfumo wetu wa elimu. Lugha ya Kiingereza nakumbuka ilianza kufundishwa toka darasa la tatu (sijui kama bado ni hivi). Sasa mtu anachukua Kiingereza toka darasa la tatu hadi la kumi na nne na bado hajamudu lugha hii ni shida. Ama walimu wetu, mitaala yetu au mfumo wetu mzima unahitai kuangaliwa. Na hili linahusu pia lugha ya Kiswahili yenyewe. Tumeona watu wanatoka Chuo Kikuu lakini wanapata shida kujieleza kwa Kiswahili hadi unaweza kuwaonea huruma!
 • Lugha kama somo jingine lolote lile linahitaji mtu kujifunza zaidi na kujiendeleza. Kosa kubwa ambalo naweza kuliona ni kuwa watu wanadhaniwa “wanajua” kiingereza kwa sababu wamepata shahada Fulani. Kwamba, kwa vile mtu ameenda chuo kikuu basi anadhaniwa anajua Kiingereza. Na hasa kwa vile anaweza kuandika kwa kutumia “templates” na msaada ya program za kusaidia kuandika. Ni muhimu mtu kujiendeleza yeye mwenyewe. Ikumbukwe kuwa hata kwenye nchi za wazungumzaji wa Kiingereza wa asili pia na wao wanawafundisha watoto wao Kiingereza sahihi. Kiingereza cha kuandika na kuzungumza vina misamiati tofauti na kile cha kisomi. Tuliosoma kwenye hizi nchi za wenzetu tunajua kabisa kuwa hata Chuo Kikuu baadhi ya masomo ya kwanza kwenye kozi ni yale ya kupandisha lugha kidogo. Masomo haya yanaitwa “English 101” ambayo ni kozi ya mhula wa kwanza kwenye vyuo vikuu vingi. Sasa kama wenyewe hawa wanatoa hizi kozi na zinaenda zaidi sisi wengine ambao Kiingereza ni lugha ya tatu au ya nne kwanini tusione umuhimu wa kuhakikisha mtoto kabla ya kwenda Chuo Kikuu anasoma Kiingereza tena? Hadi awe anaonesha uhimili (proficiency) ya lugha?
 • Ni muhimu kuanzia sasa kwa Wizara ya Mambo ya Nje au chombo husika kuhakikisha kuwa Rais anaenda na mkalimani wake ambaye anamudu Kiingereza. Asiwe mtu mwenye “mmh mmh, aah aah” nyingi! Isije kutokea lililotokea juzi Zimbabwe. Kwamba, Wizara na Ikulu hawakumuandaa mtu wa kufanya ukalimani ni jambo la aibu. Kwenye mambo haya ya kimataifa kuna taratibu za kuweza kumtumia mkalimani baada ya kuapa. Kwanini hakukuwa na mkalimani sielewi. Rais Magufuli na yeye asidhanie kuwa watu wataelewa Kiswahili kwa vile tu yeye anazungumza. Ni lazima atoe nafasi kwa mtu kumtafsiria. Japo atakuwa anaweza kuelewa mtu akizungumza kwa Kiingereza yeye bado anaweza kujibu kwa Kiswahili na mkalimani akatafsiri. Wapo Watanzania wengi ndani na nje ambao wanamudu lugha mbalimbali na ambao Rais anaweza kuwatumia.
Itoshe tu mimi kusema kuwa, sijaona tatizo lolote lile kwa Rais kuzungumza lugha ya Kiswahili kwa sababu yoyote ile. Kitu ambacho sikukipenda na hakikuwa na ulazima ni kuonekana kuwa upande wetu hatukujiandaa vizuri na kuwa Rais alizungumza Kiswahili bila kuwaandaa upande wa pili. Kuna teknolojia za kutosha hata za vyombo vya masikioni ambayo Rais anaweza kwenda navyo na wageni wahusika wakapewa wakati anazungumza na watu wetu wakatafsiri moja kwa moja. Kama tumeamua kuyavulia nguo maji, basi tujitumbukize kweli kweli siyo miguu tu! Ni matumaini yangu kuwa uamuzi wa makusudi, wa kina na wenye kuongozwa na sayansi utafanyika ili kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inaendelea kukuzwa lakini vile vile kuinua matumizi ya lugha ya Kiingereza. Si lazima tufanye uchaguzi wa kimojawapo na si kingine. Naamini kwa taifa letu kuendelea hivi viwili vinatakiwa viwe kama mapacha wanaofanana. Naamini katika kuharakisha maendeleo na kujiamini hatupaswi kuonesha uduni au ubora wa lugha moja dhidi ya nyingine na badala tuone kuwa lugha hizi kama walivyofanya nchi nyingine duniani zinaendana. Wachina wanajifunza Kichina na Kiingereza, Waarabu wanajifunza Kiarabu na Kiingereza, hata Wajerumaini na Wafaransa nao wanakifunza Kiingereza vile vile. Sasa kama hawa wenzetu walioendelea wanaona umuhimu wa lugha zao PAMOJA na lugha ya Kiingereza sisi tunachokihofia ni nini?
Magufuli ameonesha njia tu. Tutaifuata au tunaona aibu na kujiona duni?
Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
 
GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,153
Nakupongezs umeandika kitu ambacho ndicho hasa ninachohisi hata mimi. Binafsi siwezi mcheka mheshimiwa Rais kwa kutokufahamu Vizuri Kiingereza. Katika Saikolojia kuna kitu kinaitwa Multi Intelligence. Sitozungumzia sana hii dhana ya Multi Intelligence.

Akili zinatofautiana. Usitegemee mwenye akili ya Hesabu atakuwa na uwezo mzuri pia wa kujieleza au kufaham lugha kirahisi. But pia kuna mwingine ni mzuri wa Kuimba au Kucheza but si mzuri Darasani. Huwezi sema hana akili.

Siwezi mcheka Mh kwa kutofaham kiingereza vizuri. Nafaham hata kiswahili pia kinampa shida.

WITO WANGU.
Aache kabisa kutumia Kiingereza. Atumie Kiswahili na kila anapoenda aende na Mkalimani wa Lugha hiyo. Siyo dhambi. Kama anakuwa comfortable kwenye Kiswahili basi atumie Kiswahili aachane na Kiingereza.

View attachment 1112688

Goldman

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
1,925
2,379
Ni jambo ambalo liko wazi wala halihitaji chumvi hawezi kujieleza kwa lugha ya kiingereza kwa mda mrefu its simple as that, ingawa chuo kasoma uingereza ina maanisha siyo mtu wa kujichanganya na watu. Hajui kitaa kukoje hana washikaji yaani yale mambo ya saigon hajawahi hata kaa kijiwe.
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
20,069
42,915
Member mmoja hapo juu kaongea point ya maana mnooo! Kama lengo ni kukitangaza Kiswahili, itungwe sheria tena kwa HATI YA DHARURA kwamba Kiongozi yeyote ndani ya Serikali akiwa ziarani nje ya nchi lugha rasmi iwe Kiswahili tu na sio vinginevyo na aambatane na wakalimani. Hapo kweli tutaeleweka tunaposema tunakitangaza Kiswahili.
 
Ilu

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
1,183
1,603
Jibu sahihi ni namba mbili hajiamini na hawezi kujieleza kwa ufasaha kwa kingereza. Ingekuwa namba moja au namba tatu basi angeenda huko na wakalimani wakutafsiri kiswahili kwenda kingee apate kueleweka. Kutokuwa na wakalimani ina maana hakuwa na mpango wa kukitangaza kiswahili.

Hv hata Prof Kalamaganda alishindwa kutafsiri au hakuwepo?
 
gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,277
20,634
Mimi kosa kubwa Sana ambalo nawashangaa watu wa ikulu Ni swala moja tuu la kufuata taratibu sahihi. Ni ajabu na kituko kuona rais anaenda kuhutubia kimataifa bila vifaa Wala mkalmani.

Hii haina tofauti na siku moja aliwah kuvaa koti la suti upande. Yaan unajiuliza hakuna watu wanaojua haya Mambo? Hata personal secretary wake hajui? Ama Hana?
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,590
27,713
Sasa kwa nini umeandika kwa Kiswahili na siyo hicho Kiingereza? Kwanza hata ile tu kuonyesha mnapoteza muda kujadili jambo dogo kama hili mnaonyesha jinsi gani msivyokuwa makini na maisha, mnafikiri maisha yote hapa Duniani yanahusu kiingereza tu.

Ngoja nikwambie hakuna Binadamu wanaongea na kuthamini kiingereza kama Waafrika Kusini mwa Sahara Dunia hii ukitoa anglo saxon lkn Waafrika ndo watu masikini kuliko binadaamu yoyote yule kwa kipimo chochote kile cha umasikini, hata Afrika Kaskazini hawaongei Kiingereza lkn wako mbele kwa miaka 50 kimaendeleo ukilinganisha na Kusini mwa Sahara mnakoongea Kiingereza.

Korea Kaskazini hawajui Kiingereza lkn ni nuclear power na Raisi wa USA anaomba kukaa meza moja kutatua tatizo, Vietnam hawajui Kiingereza lkn wako miaka zaidi ya 50 mbele ya Afrika Kusini mwa Sahara.

Sasa hicho kiingereza chenu kimeleta nini hapa Afrika?
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
34,230
61,125
 • Ameamua kuitangaza na kuikuza lugha Kiswahili kimataifa.
 • Hajiamini kujieleza kw aufasaha katika lugha ya Kiingereza
 • Sababu zote mbili za a na b.
This is rubbish from a learned person like you! If this so-called "kukitangaza Kiswahili" is done by a person with a very good command of English like Professor "Lumumba" anyway, then your arguments would hold water. But with a person so poor in English, both spoken and written, then your thinking from a person of your level, allow me to call it "professorial" rubbish!
 
Giltami

JF-Expert Member
Feb 23, 2017
801
1,079
Basi tulifute Baraza la kiswahili Tanzania maana watu wanakula mishahara bure huko mkuzaji wa kiswahili ashapatikana.

Usipotoshe watu mtu kufika level ya Phd lugha uliyosomea inakushinda ni tatizo tena wale vijana wa UDOM walioitwa VILAZA waombwe msamaha.

Tatizo pia hata lugha hiyo mnayodai anaikuza hawezi tamka sentesi tano hajakosea.
 
900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
4,444
4,385
View attachment 1112688
(picha na New Zimbabwe.com)​

Na. M. M. Mwanakijiji
Inawezekana zipo sababu kubwa tatu ambazo zimemfanya Rais Magufuli kuanza kutumia lugha ya Kiswahili anapokutana na wageni wa kigeni pale Ikulu au anaposafiri kwenda ng’ambo. Sababu hizo zikieleweka zinaweza kutudokeza kidogo kwanini yumkini Rais amefikia uamuzi huo. Naomba kupendekeza tu kuwa tunaweza tusizikubali sababu hizi na inawezekana zikaonekana si za msingi lakini zinaweza kuwa na maana kubwa kitaifa.
Sababu hizi tatu zaweza kuwa ni:
 • Ameamua kuitangaza na kuikuza lugha Kiswahili kimataifa.
 • Hajiamini kujieleza kw aufasaha katika lugha ya Kiingereza
 • Sababu zote mbili za a na b.
Kwa vile hakuna chombo chochote cha serikali kilichotoa taarifa za uamuzi na sababu ya Rais kutumia lugha ya Kiswahili kwa namna hii basi ni haki ya Watanzania kukisia sababu hizi hadi itakavyoelezwa vinginevyo. Ni bahati mbaya na makosa kuwa vyombo ambavyo vingeweza kutoa taarifa hizo hajifanya hivyo. Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Wizara ya Habari na Utamaduni, au hata Ofisi ya Rais wenyewe wangeweza kuwaeleza tu Watanzania sababu ya uamuzi huu. Kwa vile hawajafanya hivyo, na sidhani kama wanampango wa kufanya hivyo basi sisi wengine tumejipa uhuru na haki ya kudhania. Naomba niziangalie sababu hizi tatu na maana yake kwa taifa.
 • Ameamua kuitangaza na kuikuza lugha ya Kiswahili kimataifa.
Lugha ya Kiswahili ni lugha kubwa, inayoeweka na watu wengi zaidi Afrika kuliko lugha nyingine yeyote ya Kiafrika. Karibu nchi 14 za Kiafrika zina wazungumzaji wa aina ya lugha ya Kiswahili. Ukichukulia tu kwa haraka haraka kuwa watu wa Tanzania na Kenya peke yake ambao wanaelewa Kiswahili kwa kiasi unaona kuwa tayari karibu watu milioni 100 wanaelewa kwa namna Fulani lugha ya Kiswahili. Miaka ya karibuni tayari mataifa mengine ya Kiafrika yameanza kukipokea Kiswahili kama lugha rasmi mojawapo.
Hivyo, Rais anapotumia lugha ya Kiswahili anakipa jukwaa kubwa zaidi kuliko huko nyuma. Tulizoea kwa muda mrefu kuwa marais wetu wanapoenda nje hata kwa majirani zetu wanalazimika kuzungumza lugha ya Kiingereza. Kwamba, sisi Waafrika hatuna lugha inayotuunganisha watu (lingua franca) wote isipokuwa zile lugha za kigeni. Kiswahili kama lugha ya Kiafrika ni rahisi kutamkika kwani misingi yake ya maneno iko karibu katika lugha zote za kibantu na kwa kiasi kikubwa lugha nyingine za Kiafrika.
Kwa kutumia lugha ya Kiswahili Rais anaipa heshima lugha yetu; heshima ambayo inastahili. Hivi majuzi wakati Rais Donald Trump wa Marekani alipoenda Japan tuliona jinsi Waziri Mkuu wa Japan Abe Shinzo akizungumza Kijapani. Hili limetokea hata kiongozi huyo wa Marekani alipokutana na Rais wa China au wa Urusi. Kibarua ilikuwa ni kwa wakalimani kutafrisi kutoka lugha moja kwenda nyingine. Hili halikuwa jambo la ajabu.
Hivyo, pamoja na kuitangaza na kuikuza lugha hii Magufuli anaipa heshima ambayo inastahili. Kwamba, wazungumzaji wa Kiswahili hata wakiwa na vyeo vya juu kabisa wasijione duni mbele ya wageni. Mmoja wa washairi wakubwa kabisa – kama siyo mkuu kabisa – katika historia ya nchi yetu marehemu mzee Shaaban Robert aliwahi kuandika utenzi wake mashuhuri wa “Titi la Mama li Tamu”. Ubeti wake wa kufungulia Shaaban Robert aliandika:
Titi la mama litamu,hata likiwa la mbwa,
Kiswahili naazimu,sifayo iliyofumbwa,
Kwa wasiokufahamu,niimbe ilivyo kubwa,
Toka kama mlizamu, funika palipozibwa

 • Hajiamini katika kujieleza katika lugha ya Kiingereza
Kwa wale ambao tumepata nafasi ya kumsikia Rais Magufuli akizungumza Kiingereza ni wazi kuwa tunaweza kuona akifanya makosa ama katika matamshi, muundo au fasihi ya lugha ya Kiingereza. Makosa ambayo Magufuli anayafanya wengi ambao wanajifunza lugha ya Kiingereza au wamejifunza lugha hiyo ukubwani wanaweza kujikuta wakiyafanya. Hili ni kweli pia kwa wazungumzaji wa asili wa lugha ya Kiingereza. Makosa haya yanaitwa “common mistakes” au “Common errors” katika lugha ya Kiingereza.
Makosa haya ya lugha si ya kipekee kwa lugha ya Kiingereza. Kwa mtu anayejifunza lugha ya Kiswahili au lugha nyingine yeyote anaweza kujikuta akiyafanya mara kwa mara. Ama katika kutamka maneno au katika muundo na sarufi ya lugha hiyo. Kwa mfano kwa watu wengi wanaojifunza Kiswahili wanaweza kushangaa kuwa lugha yetu haina sana msisitizo katika herufi Fulani kama ilivyo katika lugha nyingine nyingi.
Sasa Magufuli inawezekana ameona watu wanamsema au anaonekana kama kituko kwa wageni pale anapovunja lugha ya Kiingereza hasa kwa vile ni msomi wa PhD. Hili linatuleta kwenye hoja nyingine ndani ya hoja hii kuwa kuwa msomi wa eneo Fulani haina maana mtu anaimudu lugha ya Kiingereza. Kiingereza cha kisomi (academic writing) mara nyingi si kigumu kama kile cha kujieleza. Hii ni kwa sababu lugha ya kisomi ina maneno yake na ni rahisi kufuata. Si kila msomi anaweza kuandika riwaya ya Kiingereza au insha ya kijamii kwa Kiingereza bila kupata shida ya maneno. Hili linatokea hata kwa wasomi kutoka nchi nyingine ambazo hawazungumzi Kiingereza kwa asili (native English speakers).
Sasa kama Magufuli anaona hajiamini kwa sababu ya makosa ya mara kwa mara – ambayo si ya ajabu sana – inawezekana kuamua kuzungumza Kiswahili ni salama na bora kwake kuliko kujionesha udhaifu wake wa lugha.
Ikumbukwe hili si tatizo la Magufuli tu. Wapo watu wetu wengi tu ambao wanaweza kuchanganya maneno ya Kiingereza kwenye Kiswahili (Kiswakinge) lakini hawawezi kuunda kauli zinazoeleweka za lugha ya Kiingereza. Na wengine hata Kiswahili kilichonyoka (kisichonganyana) na Kiingereza hawawezi kukitumia. Tumeona mambo haya Bungeni ambapo sharti mojawapo ni kuwa mgombea awe anaweza kujua lugha ya Kiingereza au Kiswahili. Tumeona watu wanaoomba kugombea Bunge la Afrika ya Mashariki wengine wakivunja maneno hadi unasikia kujing’ata ulimi! Lakini watu wale wale wanaweza kujieleza kwa Kiswakinge!
 • Mchanganyiko wa Sababu 2 za Kwanza
Inawezekana kabisa kuwa Rais ameamua kufanya hivi kutokana na sababu zote mbili kwamba anataka kuienzi, kuiheshimu na kuipa jukwaa kubwa lugha ya Kiswahili lakini vile vile yeye mwenyewe hayuko mzuri sana (kama Watanzania wengine wengi) kutumia lugha ya Kiingereza kwenye hadhara. Kama hili ni kweli basi hakuna aibu katika yote mawili; yote mawili yanaweza kuwa sababu za kutosha tu.
Hii ina Maana gani kwa taifa?
Swali kubwa la msingi ni je jambo hili lina maana gani kwetu kama taifa? Je, ina maana sasa Watanzania wasijifunze Kiingereza kabisa na wote wajifunze kila kitu kwa Kiswahili? Je, ina maana lugha ya Kiingereza si muhimu tena? Naomba kupendekeza mambo yafuatayo:
 • Ikumbukwe kuwa kama taifa na kama mtu mmoja mmoja hatuwezi kukwepa matumizi ya lugha ya Kiingereza. Kwanza kwa sababu mfumo wetu wa kiserikali unafuata kwa kiasi kikubwa mfumo wa Kiingereza lakini pili ni kuwa kwa vile lugha ya Kiingereza ndio lugha inayoiunganisha dunia. Sasa hivi ni vigumu kwenda mahali popote na kukosa kabisa mtu anayejua Kiingereza. Ni rahisi kupata mtu anayejua Kiingereza kuliko mtu anayejua lugha nyingine yeyote. Hivyo, Kiingereza hakikwepeki.
 • Kwamba watu wetu wanapata shida kumudu lugha hii ni matokeo ya mambo mengi. Yawezekana kwa kiasi kikubwa ni suala la elimu na mfumo wetu wa elimu. Lugha ya Kiingereza nakumbuka ilianza kufundishwa toka darasa la tatu (sijui kama bado ni hivi). Sasa mtu anachukua Kiingereza toka darasa la tatu hadi la kumi na nne na bado hajamudu lugha hii ni shida. Ama walimu wetu, mitaala yetu au mfumo wetu mzima unahitai kuangaliwa. Na hili linahusu pia lugha ya Kiswahili yenyewe. Tumeona watu wanatoka Chuo Kikuu lakini wanapata shida kujieleza kwa Kiswahili hadi unaweza kuwaonea huruma!
 • Lugha kama somo jingine lolote lile linahitaji mtu kujifunza zaidi na kujiendeleza. Kosa kubwa ambalo naweza kuliona ni kuwa watu wanadhaniwa “wanajua” kiingereza kwa sababu wamepata shahada Fulani. Kwamba, kwa vile mtu ameenda chuo kikuu basi anadhaniwa anajua Kiingereza. Na hasa kwa vile anaweza kuandika kwa kutumia “templates” na msaada ya program za kusaidia kuandika. Ni muhimu mtu kujiendeleza yeye mwenyewe. Ikumbukwe kuwa hata kwenye nchi za wazungumzaji wa Kiingereza wa asili pia na wao wanawafundisha watoto wao Kiingereza sahihi. Kiingereza cha kuandika na kuzungumza vina misamiati tofauti na kile cha kisomi. Tuliosoma kwenye hizi nchi za wenzetu tunajua kabisa kuwa hata Chuo Kikuu baadhi ya masomo ya kwanza kwenye kozi ni yale ya kupandisha lugha kidogo. Masomo haya yanaitwa “English 101” ambayo ni kozi ya mhula wa kwanza kwenye vyuo vikuu vingi. Sasa kama wenyewe hawa wanatoa hizi kozi na zinaenda zaidi sisi wengine ambao Kiingereza ni lugha ya tatu au ya nne kwanini tusione umuhimu wa kuhakikisha mtoto kabla ya kwenda Chuo Kikuu anasoma Kiingereza tena? Hadi awe anaonesha uhimili (proficiency) ya lugha?
 • Ni muhimu kuanzia sasa kwa Wizara ya Mambo ya Nje au chombo husika kuhakikisha kuwa Rais anaenda na mkalimani wake ambaye anamudu Kiingereza. Asiwe mtu mwenye “mmh mmh, aah aah” nyingi! Isije kutokea lililotokea juzi Zimbabwe. Kwamba, Wizara na Ikulu hawakumuandaa mtu wa kufanya ukalimani ni jambo la aibu. Kwenye mambo haya ya kimataifa kuna taratibu za kuweza kumtumia mkalimani baada ya kuapa. Kwanini hakukuwa na mkalimani sielewi. Rais Magufuli na yeye asidhanie kuwa watu wataelewa Kiswahili kwa vile tu yeye anazungumza. Ni lazima atoe nafasi kwa mtu kumtafsiria. Japo atakuwa anaweza kuelewa mtu akizungumza kwa Kiingereza yeye bado anaweza kujibu kwa Kiswahili na mkalimani akatafsiri. Wapo Watanzania wengi ndani na nje ambao wanamudu lugha mbalimbali na ambao Rais anaweza kuwatumia.
Itoshe tu mimi kusema kuwa, sijaona tatizo lolote lile kwa Rais kuzungumza lugha ya Kiswahili kwa sababu yoyote ile. Kitu ambacho sikukipenda na hakikuwa na ulazima ni kuonekana kuwa upande wetu hatukujiandaa vizuri na kuwa Rais alizungumza Kiswahili bila kuwaandaa upande wa pili. Kuna teknolojia za kutosha hata za vyombo vya masikioni ambayo Rais anaweza kwenda navyo na wageni wahusika wakapewa wakati anazungumza na watu wetu wakatafsiri moja kwa moja. Kama tumeamua kuyavulia nguo maji, basi tujitumbukize kweli kweli siyo miguu tu! Ni matumaini yangu kuwa uamuzi wa makusudi, wa kina na wenye kuongozwa na sayansi utafanyika ili kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inaendelea kukuzwa lakini vile vile kuinua matumizi ya lugha ya Kiingereza. Si lazima tufanye uchaguzi wa kimojawapo na si kingine. Naamini kwa taifa letu kuendelea hivi viwili vinatakiwa viwe kama mapacha wanaofanana. Naamini katika kuharakisha maendeleo na kujiamini hatupaswi kuonesha uduni au ubora wa lugha moja dhidi ya nyingine na badala tuone kuwa lugha hizi kama walivyofanya nchi nyingine duniani zinaendana. Wachina wanajifunza Kichina na Kiingereza, Waarabu wanajifunza Kiarabu na Kiingereza, hata Wajerumaini na Wafaransa nao wanakifunza Kiingereza vile vile. Sasa kama hawa wenzetu walioendelea wanaona umuhimu wa lugha zao PAMOJA na lugha ya Kiingereza sisi tunachokihofia ni nini?
Magufuli ameonesha njia tu. Tutaifuata au tunaona aibu na kujiona duni?
Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
2020 nampango wa kugombea ubunge chama changu kikinipitisha,ngoja nianze kupiga brashi lugha ya Malkia
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
56,997
210,784
This is rubbish from a learned person like you! If this so-called "kukitangaza Kiswahili" is done by a person with a very good command of English like Professor "Lumumba" anyway, then your arguments would hold water. But with a person so poor in English, both spoken and written, then your thinking from a person of your level, allow me to call it "professorial" rubbish!
How did he write and defend his thesis?
 
40 Reactions
Reply
Top Bottom