kanali mstaafu
JF-Expert Member
- May 17, 2015
- 4,318
- 4,098
Habari za asubuhi bandugu,
Kama ilivyo desturi yangu ya kujaribu kudodosa vitu vilivyo mtambuka japo yawezekana umri wangu ukawa bado haujafikia kuwaza hayo masuala niliona yafaa kuyajua kwa kina masuala kama haya kwa faida ya baadae.
Katika pitapita zangu nimekuwa nasikia baadhi ya watu waliooa wanasema eti ishu ya kuoa hutokea kama emergency na kwa mara chache sana watu huoa watu waliopanga kuwa nao na kwa muda waliojipangia.
Lakini kwa wengi imekuwa tofauti sana kwani wanasema huwa inatokea tu mtu anaoa msichana ambaye hana vigezo alivyovihitaji/alivyojipangia tangu kitambo na tena kwa muda ambao hakupanga.
Lakini ninapowauliza sababu ya suala la wengi wao kuoa kwa emergency huwa wanaishia tu kusema kuwa inatokea tu mawazo yanabadilika ndani ya siku moja na mtu anaamua kuoa.Je sababu hii inajitosheleza kweli au huwa kuna sababu nyingine zaidi zinazochangia hili suala?
Kwa wale mliopo katika ndoa naomba mtupe mbivu na mbichi juu ya hili jambo