Kwanini watu huoa na kuolewa?

Kwanini watu huoa na kuolewa?

msaidizi wa kufanana naye ni jukumu tofauti kabisa na kuoa/kuolewa swali linataka sababu za kuoa/kuolewa
Kuoa/kuolewa kuna kukamilisha...

Wewe una ubavu mmoja,mkeo ubavu wapili mnaungana kua mwili mmoja,kutengeneza familia,muweze kusaidiana,kufarijiana na kufanya mambo yote kwa umoja na furaha
 
Inajionesha dhahiri kabisa uko mbali na Biblia Takatifu na Kanisa kwa ujumla

hilo sio jibu
pia swala la kuoa/kuolewa halichagui dini wakisto/waislam wote wanaoa
 
Samahani ndugu kwa kuwa upande mmoja. Nilimaanisha kuyasoma Maandiko Matakatifu. Kila kitu kimo humo

kwa mfano wasiokua na imani kaika ukristo/uislam ukusa kutokuoa?
 
Binafsi nimeolewa ili kutimiza kusudio la kuletwa duniani.
Kujaza dunia
 
hayo ni mambo ya asili ndo maana MUNGU alipomuumba ADAM akaona ADAM atakuwa ajakamilika bila kupata msaidizi hivyo MUNGU alimuumba HAWA ili asaidiane majukumu na ADAM...hivyo mtu anaoa au kuolewa ili tu apate mwenza wa kusaidiana nae katika maisha.
kwani adam na hawa walioana...?hebu nisaidie nimepoteza kumbukumbu...?
 
Wana jf naomba kujuzwa sababu hasa inayotufanya kuoa/kuolewa au kwa wale walio kwenye ndoa kwa nini umeoa/kuolewa?, mimi ni kijana mwenzenu ambaye nipo katika mchakato wa kutafuta mwenza, lakini kutokana na mabandiko kadha wakadha hapa jf inaonesha ndani ya ndoa kuna misigishano mingi mno inayopelekea watu kuchit, kulea watoto wasio wao pia wakati mwingine na mengine mengi sasa ule upendo ninaousikia huwa umeenda wapi?

Kwa hali ya kawaida mtu unaweza fikiri nina matatizo kuleta uzi huu ila kuna watu wameoa/kuolewa wasijue kwa nini walifikia maamuzi hayo? (kuoa/kuolewa) kama umeoa/kuolewa naomba sababu ya:-

i) Kwanini umeoa? Kwanini unafikiri kuoa?

ii) Kwanini umeolewa? Kwanini unafikiri kuolewa?

Tafadhali fikiri kabla ya kujibu then unisaidie kwa namna ya kunijenga na siyo kunibomoa ili vijana wengine wafaidike pia.

View attachment 417422

Ni kitu ambacho pia nimekuwa nikijiuliza siku nyingi. Nimekuwa nikijiuliza kwa nini ndoa zimekuwa ni mojawapo ya kitu ambacho kimekuwa kama vile adhaa kwa wanandoa mda mfupi baada ya kuoana? ili hali asilia kubwa wanaoana kwa hiari yao wenyewe?.Huwa nafika mbali kwa kujiuliza ni kitu ambacho huwafumba macho watu kiasi kwamba kabla yakuoa/kuolewa hawaoni kile ambacho huwa wanakiona baada ya kuingia kwenye ndoa nakuanza kuzua varangati licha ya mambo mengi yahusuyo maisha ya ndoa kuwa wazi ?

Nilichokuja kugundua ni kwamba wengi wanaoa/kuolewa pasi na kukaachini na kufikiria kwanini waoe/kuolewa,ni vitu gani wanavifata katika ndoa,na je wapotayari kwa dhati kuyavumilia watakayo yakuta huko?
Badala yake wengi wanafikia maamuzi hayo kwa sababu tu umri unawatupa mkono,tamaa za mda mfupi (pasipo kuhusisha ubongo kwa kiasi kikubwa),kwa kushawishiwa na ndugu na jamaa ,wengine wanaiga na pia kutaka sifa tu.Kama mtu ameingia kwa sababu hizo nithahiri ndo maana ndoa nyingi haziishi mizozo kwa vile wanandoa wamekutana na vitu ambayo hawakuvifikiria kabla.Mwanandoa hataona shida kuchepuka kwa vile hajajicomit hicho kwa mwenza wake wala hicho hakikuwa kipaumbele chake kuingia kwenye ndoa.

Mtazamo wangu ndoa siyo lazima kwa vile vingi ambavyo watu wanadhamiria na kuvifata katika ndoa unaweza kuvipata hata ukiwa nje ya ndoa(hujaoa/kuolewa).Sioni sababu ya kuchepuka wakati una mke au mme ambaye anaweza anaweza kukupa hicho unachokifata huko kwenye mchepuko.Tunatakiwa tuingie katika ndoa kwa sababu tuko tayari kukaa na kuiishi ndoa, tuko tayari kwa dhati (wote wawili) kwenye ndoa , tunahaja ya kuyatambua mapungufu yetu ili kisiwe kikwazo kwa wengine(wenza wetu)
inatosha kwa leo
 
Ili kuanzisha familia. Na kupata watoto waliozaliwa ndani ya ndoa
 
Nilichokuja kugundua ni kwamba wengi wanaoa/kuolewa pasipo kukaachini na kufikiria kwanini waoe/kuolewa,ni vitu gani wanavifata katika ndoa,na je wapotayari kwa dhati kuyavumilia watakayo yakuta huko?

haya ni baadhi ya mambo ya msingi kabisa kujiuliza kabla ya kufanya maamuzi ya kuoa/kuolewa
 
Ili kuanzisha familia. Na kupata watoto waliozaliwa ndani ya ndoa

sijawahi sikia utofauti kati watoto waliozaliwa ndani na nje ya ndoa, anaweza kuwa tahira kazaliwa ndani au nje ya ndoa
 
1. Kummiliki mwenza katika unyumba na kumhalalisha kijamii, kiserikali na kidini.

2. Kuanzisha milki yetu mimi na mwenza kiunyumba.

3. Kutafsiri hisia za upendo katika ulimwengu wa matendo halisi.
 
Ni kitu ambacho pia nimekuwa nikijiuliza siku nyingi. Nimekuwa nikijiuliza kwa nini ndoa zimekuwa ni mojawapo ya kitu ambacho kimekuwa kama vile adhaa kwa wanandoa mda mfupi baada ya kuoana? ili hali asilia kubwa wanaoana kwa hiari yao wenyewe?.Huwa nafika mbali kwa kujiuliza ni kitu ambacho huwafumba macho watu kiasi kwamba kabla yakuoa/kuolewa hawaoni kile ambacho huwa wanakiona baada ya kuingia kwenye ndoa nakuanza kuzua varangati licha ya mambo mengi yahusuyo maisha ya ndoa kuwa wazi ?

Nilichokuja kugundua ni kwamba wengi wanaoa/kuolewa pasi na kukaachini na kufikiria kwanini waoe/kuolewa,ni vitu gani wanavifata katika ndoa,na je wapotayari kwa dhati kuyavumilia watakayo yakuta huko?
Badala yake wengi wanafikia maamuzi hayo kwa sababu tu umri unawatupa mkono,tamaa za mda mfupi (pasipo kuhusisha ubongo kwa kiasi kikubwa),kwa kushawishiwa na ndugu na jamaa ,wengine wanaiga na pia kutaka sifa tu.Kama mtu ameingia kwa sababu hizo nithahiri ndo maana ndoa nyingi haziishi mizozo kwa vile wanandoa wamekutana na vitu ambayo hawakuvifikiria kabla.Mwanandoa hataona shida kuchepuka kwa vile hajajicomit hicho kwa mwenza wake wala hicho hakikuwa kipaumbele chake kuingia kwenye ndoa.

Mtazamo wangu ndoa siyo lazima kwa vile vingi ambavyo watu wanadhamiria na kuvifata katika ndoa unaweza kuvipata hata ukiwa nje ya ndoa(hujaoa/kuolewa).Sioni sababu ya kuchepuka wakati una mke au mme ambaye anaweza anaweza kukupa hicho unachokifata huko kwenye mchepuko.Tunatakiwa tuingie katika ndoa kwa sababu tuko tayari kukaa na kuiishi ndoa, tuko tayari kwa dhati (wote wawili) kwenye ndoa , tunahaja ya kuyatambua mapungufu yetu ili kisiwe kikwazo kwa wengine(wenza wetu)
inatosha kwa leo

Mkuu ukichunguza kwa makini utagundua kuna vitu vingi sana ambavyo havina maana yoyote lakini watu tumekua tukivifanya bila hata kuwa na sababu za msingi. Ni mila tuu na mazoea tuliyorithishwa
 
Mkuu ukichunguza kwa makini utagundua kuna vitu vingi sana ambavyo havina maana yoyote lakini watu tumekua tukivifanya bila hata kuwa na sababu za msingi. Ni mila tuu na mazoea tuliyorithishwa

Apa mkuu ndo nmeanza kupata sababu kwako kwamba ni MILA TU
 
1. Kummiliki mwenza katika unyumba na kumhalalisha kijamii, kiserikali na kidini.

2. Kuanzisha milki yetu mimi na mwenza kiunyumba.

3. Kutafsiri hisia za upendo katika ulimwengu wa matendo halisi.

Hivi inaruhusiwa kummiliki binadamu mwenzio..??
 
binafsi mimi n mvivu wa kazi za nyumban hasa kufua na pia huwa napenda kugonga daileee
 
Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na siyo umpende mwanadamu
Kwani kupenda mwanadamu mwingine kunanizuia kumpenda Mungu

Maandiko si yamesema
Mpende Mungu kwa moyo wote, akili zote, nguvu zote

Na mpende jirani yako kama unavyojipenda??

Maandiko pia yanasema
Waume wapendeni wake zenu,
Wanawake waheshimuni waume zenu

Sasa point yako ni nini hasa?
 
Back
Top Bottom