Mimi bado sijaoaWana jf naomba kujuzwa sababu hasa inayotufanya kuoa/kuolewa au kwa wale walio kwenye ndoa kwa nini umeoa/kuolewa?, mimi ni kijana mwenzenu ambaye nipo katika mchakato wa kutafuta mwenza, lakini kutokana na mabandiko kadha wakadha hapa jf inaonesha ndani ya ndoa kuna misigishano mingi mno inayopelekea watu kuchit, kulea watoto wasio wao pia wakati mwingine na mengine mengi sasa ule upendo naousikia huwa umeenda wapi?
Kwa hali ya kawaida mtu unaweza fikiri nina matatizo kuleta uzi huu ila kuna watu wameoa/kuolewa wasijue kwa nini walifikia maamuzi hayo? (kuoa/kuolewa) kama umeoa/kuolewa naomba sababu ya:-
i) Kwanini umeoa? Kwanini unafikiri kuoa?
ii) Kwanini umeolewa? Kwanini unafikiri kuolewa?
Tafadhali fikiri kabla ya kujibu then unisaidie kwa namna ya kunijena na siyo kunibomoa ili vijana wengine wafaidike pia.
Kwa nini nitaoa, naamini Mungu ameweka kusudio hilo maisha yangu.
Ameniumba nna uwezo wa kupenda, nna uwezo wa kuongoza, nna uwezo wa kusimama kwa ajili ya imani yangu
Kuoa kunanipa nafasi ya kudhihirisha ule uwezo ambao Mungu ameweka ndani yangu
Uwezo wa kumpenda mtu kwa moyo wote, kukubali mapungufu yake na kumpenda hivyo. Yaani najifunza Unconditional love
Uwezo wa kusimama katika yale ninayoyajua kiroho, kitaaluma, kimaisha,
Niweze kumshirikisha na yeye aweze kujua na yeye aweze kukua nami na hata tukipata watoto tuweze kuwapa hizi hazna
Uwezo wangu wa kupigana na vikwazo mbalimbali kimaisha, kifedha, kiimani na kuweza kupigania wale nnaowapenda
Kuoa inatimiza kusudi ambalo Mungu ameweka rohoni mwangu.
Kuakisi tabia yake kama alivyoidhihirisha kupitia Yesu Kristo: Kupenda unconditionally, kujitoa kwa ajili ya wengine, kuwavumilia na kuwawezesha nao waweze kufikia kusudi lao Mungu alilowawekea