Kwanini watu hugombania kuzika maiti?

Dexta

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
1,756
4,144
Habari za mchana wanajamii forums.?
Nisiwapotezee muda, niende moja kwa moja kwenye mada.

Kuna swali huwa ninajiuliza sana lakini bado sijawahi kupata jibu halisi, ninaomba mwenye uelewa wa hili swali anipe majibu.

Ni mara nyingi huwa tunaona ama kusikia matukio ya aina hii, watu kugombea maiti. Unakuta wengine wanataka marehemu azikwe kimila wengine wanataka azikwe kidini au wengine wanataka akazikwe kwao wengine wanataka azikwe alipofariki yani unakuta ni vurugu mwanzo mwisho.

Faida yake huwa ni nini.?
Mshana Jr
Rakims
jerryempire
 
Njoo huku milimani uone...
Ukiumwa hutaona mtu subiri ufe sasa utabebwa hadi na V8 utazikwa kwa heshima zote hadi majirani watashangaa.
Faida yake huwa ni nini sasa?
 
Habari za mchana wanajamii forums.?
Nisiwapotezee muda, niende moja kwa moja kwenye mada.

Kuna swali huwa ninajiuliza sana lakini bado sijawahi kupata jibu halisi, ninaomba mwenye uelewa wa hili swali anipe majibu.

Ni mara nyingi huwa tunaona ama kusikia matukio ya aina hii, watu kugombea maiti. Unakuta wengine wanataka marehemu azikwe kimila wengine wanataka azikwe kidini au wengine wanataka akazikwe kwao wengine wanataka azikwe alipofariki yani unakuta ni vurugu mwanzo mwisho.

Faida yake huwa ni nini.?
Mshana Jr
Rakims
Hilo swali hata Mimi sipati jibu!
 
Faida yake huwa ni nini sasa?
Michango mfano aliyekufa ni ndugu wa kigogo mfano mbunge nk atataka msiba uwe kwake wabunge watoe mchango wa mamilioni afaidi

Mara ingine ni kuogopa kudharaulika mfano mdogo wake Raisi au waziri tumbo moja.kafariki lofa wa kutupwa anayeishi maisha duni sana .Mtu anabeba huo msiba ufanyike kwake kuficha siri asionekane huwa hajali ndugu nk

Wengine mirathi anayezika ndiye atasimamia mirathi

Wengine wachawi anachotaka ni yake maji ya kuoshea maiti ayachukue kwa mambo ya kishirikina

Kifupi ukiona mtu anagombea maiti zaidi ya mke mume,au wanawe jua kuna jambo

Mume,mke na watoto pekee ndio wenye maamuzi kama ni mtu hajawahi kuwa na mke au mume au watoto hapi wazazi wKe ndio hutakiwa kutoa maamuzi ila kama ana watoto wakubwa wao ndio hutakiwa kufanya maamuxi ya kuzika na kushika msiba

Sio vinginevyo
 
Michango mfano aliyekufa ni ndigu wa kigogo mfano mbunge atakomslia msiba uwe kwake wabunge watoe mchango wa mamilioni afaidi

Mara ingine ni kuogopa kudharaulika mfano mdogo wake Raisi au waziri tumbo moja.kafariki lofa wa kutupwa anayeishi maisha duni sana .Mtu anabeba huo.msiba ufanyike kwake kuficha siri asionekane huwa hajali ndugu nk

Wengine mirathi anayezika ndiye atasimamia mirathi

Wengine wachawi anachotaka ni yake maji ya kuoshea maiti ayachukue kwa mambo ya kishirikina

Kifupi ukiona mtu anagombea maiti zaidi ya mke mume,au wanawe jua kuna jambo

Mume,mke na watoto pekee ndio wenye maamuzi kama ni mtu hajawahi kuwa na mke au mume au watoto hapi wazazi wKe ndio hutakiwa kutoa maamuzi ila kama ana watoto wakubwa wao ndio hutakiwa kuzika

Sio vinginevyo
Duh! Dunia ina mengi sana.
 
Kizaa zaa chenyewe kipo pale ambapo umeoa binti ya watu na akafa wakati hujamtolea mahari, Aisee utaona Cha Moto Sana haya mambo yapo vijijini watu wanapigana mapanga kiss tu ugomvi wa maiti.
 
Back
Top Bottom