Kwanini watu hawasemi asante?

Kwanini watu hawasemi asante?

Soma uelewe kwanza kuliko kukimbilia kucomment tu, mleta mada hajasema huyo ndugu yake yupo mkoa wa Mara,ila amesema yupo "mkoa" "mara nyingi hua ananiomba ela..." hilo neno mara limetumika kama "more than once" na sio kama jina la mkoa.
huyu ni wa kike ishi nae kwa umakini maana ni wadhaifu
 
Nilikutana na mzee mmoja kapinda, nikamuuliza uchochoro wa kuelekea nilikokuwa nataka kwenda, akanionesha. Nilivyoshukuru akaniambia: "kumbe ww mstaarabu, njia sahihi kuelekea unakokwenda ni hii, huko nilikokueleza mwanzo siko". Toka siku hiyo nikajifunza kushukuru, sasa nashukuru hata nikimaliza kupiga papuchi. 😛😛🙂
Jf ni nouma [emoji1] [emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hata mimi kuna mtu namtoaga kiana anachofanya anaeka hela mfukoni anapiga kimya!sasa hua najiuliza hana akili ya kusema hata asante?ila dawa nikumuuliza sasa
 
Nadhani ni aina ya maisha ambayo mtu anakuwa ameishi kuna wengine hawajuagi hata ahsante inatumika wapi na wakati gani

Japokuwa mi pia huwa nachukia sana yaani unaweza mtumia mtu hela hawezi kupiga kukwambia ahsante mpaka umuulize na hata ukimuuliza bado hatokwambia ahsante zaidi ya kusema nimeshaipata.
Jamani mi mama mkwe wangu ndo type hiii,hata ujisacrifice vp,huwezi msikia anasema asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wanajionaga kusaidiwa ni haki yao kabisa
 
Tabia moja mbaya kabisa. Wengi wetu waha tuna hiyo tabia. Yaani hadi inakera. Mimi mtu asiposema asante kamwe hanioni tena mkono wangu wa msaada.
 
Yaani,unakuta umejipinda uwanunulie zawadi,yeye anaichukulia poa,hata asante inakuwa ngumu kuitoa,alafu mama mzazi ndo anasema asante ukisitisha kumpa maneno,jamani yataka moyo kuishi na watu wasiojua kushukuru

Sent using Jamii Forums mobile app
Cha muhimu mumy ni kuwazowea tu mana hakuna namna.

Ila kiukweli ahsante ina nafasi jamani mana inapotolewa hata nawe mtoaji unafarijika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom