Kwanini watawala hawataki kutoa ajira?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,553
44,722
Mbona mapesa yako mengi tunatoa Kodi na bado Kuna pesa kutoka nje zinakuja kwanini Sasa viongozi hawataki kukubali kwamba maendeleo Ni watu.haiwezekani daktari asomeshwe halafu aje aambiwe ajiajiri kwa kufungua hospitali.

Mbona madini ya thamani yapo mengi huko mererani si mchimbe muyauze kwa mwekezaji ili hio pesa iwe mshahara.Nahisi undugunazition unataka urudi kimya kimya kwenye hizi ishu za ajira.
 
Siyo kazi ya serikali pekee kutoa ajira kwa wananchi. Bali ni wajibu wa wananchi kutengeneza ajira ili kuisadia serikali kutoa ajira.

Wasomi ndiyo mnatuletea shida nchi hii. Mmepewa mikopo na serikali mkasoma halafu mnataka serikali huyo hiyo iwape na ajira? Duuh!!

Mlienda kusoma ili muwe wajinga? Mbona hamtatui changamoto ktk jamii, badala yake ninyi ndiyo changamoto kwa jamii?
 
Huna lolote. Ulianza kulalamika ajira tangu kipenzi chako jiwe akiwa madarakani.
 
Jamani muwe mnamwaga CV zenu hadharani, tunaziona, halafu piga kelele za ajira. Sio ooh!! yule beki wa Yanga pale alizembea, ilitakiwa amkabe yule namba nane! Nenda kakabe wewe.
 
Siyo kazi ya serikali pekee kutoa ajira kwa wananchi. Bali ni wajibu wa wananchi kutengeneza ajira ili kuisadia serikali kutoa ajira.

Wasomi ndiyo mnatuletea shida nchi hii. Mmepewa mikopo na serikali mkasoma halafu mnataka serikali huyo hiyo iwape na ajira? Duuh!!

Mlienda kusoma ili muwe wajinga? Mbona hamtatui changamoto ktk jamii, badala yake ninyi ndiyo changamoto kwa jamii?
Nitajie changamoto mbili zilizopo kwenye jamii unayoishi wewe ambazo zinaweza kuwa fursa kwa vijana kujiajiri ambazo zinahitaji mtaji mdogo ambao kijana asiye na kipato anaweza kumudu.
 
Nitajie changamoto mbili zilizopo kwenye jamii unayoishi wewe ambazo zinaweza kuwa fursa kwa vijana kujiajiri ambazo zinahitaji mtaji mdogo ambao kijana asiye na kipato anaweza kumudu.
Mkuu mimi na bibi yangu Mpitimbi hatujawahi kutaafuta kitu kinaitwa ajira. Tinalima na kufuga kwa gharama sifuri kqbisa hapa kijijini.

Mungu ametujalia nchi hii ardhi tele yenye rutuba. Hapa kijinini kwetu ardhi unapewa bure. Narudia tena unapewa bure! Sasa unataka nn?

Uza hiyo simu yako ununue mbegu na jembe la mkono uungane nasi huku upige maisha.

Wasomi fake kabisa ninyi!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom