Kwanini Watanzania wengi hawajui/hawafanyi Biashara za Exportation kwenye mazao ya Kilimo?

mass64

Senior Member
Jul 19, 2016
101
225
Ukweli ni kwamba hatujadedicate resources vya kutosha kwenye uwekezaji wetu.
Hebu kila mmoja atupe uzoefu wake kwenye Biashara za exportation

Au useme ni sababu gani zinakufanya ushindwe kufanya exportation

Mimi nitaeleza kidogo:

Leo nimeona tujadili kidogo ni kwanini sisi watanzania tunalima na tuna Ardhi nzr sana lakini hatufanyi Biashara kubwa kwenye kilimo yaani exportation , badala yake wakenya ndio wanatupiga Mzinga na kumiliki Biashara hizi Je? Tulichelewa WAP? Au ni nini ambacho hatuji?

Nitaeleza kwa namna ambavyo nimefanya utafiti wangu na kugundua mambo kadhaaa:

Kwanza kabisa, watanzania wengi sio wakulima (we a not Farmers rather we are peasants) nikiwa na maanisha kuwa hakuna mtanzania au hata kama wapo ni wachache wanaoweza kulima kuanzia hekari 50+, 100+, 250+ kwa pamoja na kuzalisha bidhaa za kilimo , kwa hyo ni ngumu kufanya Biashara za exportation kwa sababu hatuna vigezo hivyo

Pili, tulio wengi tumekuwa nyuma sana kwenye matumizi ya teknolojia pamoja na matumizi ya utaalamu kwenye kilimo vitu vya msingi kama soil test, water test, farm planning, post harvesting handling, pack house, ware house management na vingine vingi watanzania wengi hatuvijui na hatuna elimu yake , nimeeleza baadhi ya hivi vitu kwa sababu ili uweze kufanya exportation kwa baadhi ya mazao lazima uwe na certificate za taasisi ya kimataifa ya GAP sasa hawa wana vigezo na masharti yao ambayo yanaendana na vitu nilivyotaja hapo juu

Nilipokuwa naendelea kufanya utafiti kuona nani ametuloga niligundua kuwa Tanzania hasa wakulima hatuna taarifa sahihi kwenye masoko ya bidhaa za kilimo na pia tumewekuwa watu wa njaa sana na kuuza mazao Yetu Mara tuu tunapovuna kwa kuona fursa ya sisi kuwa wavivu ndio maana wahindi na waarabu ndio nakumbana nao huko masokoni kwenye Biashara kubwa za exportation na wanapata faida kubwa sana sio sana tuu faida kubwa mno (mfano mzr ni kwenye korosho) miaka yote hawa jamaa walikuwa wanapata faida kubwa kiasi gani ? Kwa sababu wakulima wananunua korosho kwa shilingi 500-1500 kwa kilo na sasa korosho hyo hyo inauza 4000 kwa kilo na wananunua just imaging

Kwa ndugu zetu wakenya matajiri wengi ni wakulima lakini sio ajabu Sana kwa wakenya kutupiga vikumbo kwenye exportation kwa sababu settlers walioanza Kilimo Kenya miaka ya 1885+ mpaka Leo wapo so not bad because their trade back home ndio maana Kenyan wanaexport sana UK, lakini soko lao liko vzr kwa sababu wana certificate za mashamba ambazo hutumika kufanya exportation iwe rahisi hasa kwenye mazao ya matunda na mboga mboga kwa hyo wanachofanya wanakuja Tanzania wananunua mazao Yetu then wana tumia certificate na label zao wanauza ulaya

Nyingine ni kwamba Tanzania tuna viongozi wengi sana ambao sio wafanyabiasha na wengi ni maskini ndio maana wakienda ulaya wanarudi na laptop na camera na wanasahau kurudi na connection za Biashara , hata wasomi wengi wanaokwenda kusoma wanarudi bila connection yoyote kitu ambacho wakenya wakienda wanarudi na akili ya Biashara kubwa , nafurahia sasa vijana wetu walioenda kusoma China wa nafanya Biashara sasa na jambo jema

Ukitaka kuanza Biashara ya exportation kwa Tanzania anza na dry food na sio mboga mboga kwa sababu hizi zinahitaji regulations nyingi sana , but grain ziko vzr sana , na pia ukitaka Biashara ya exportation ikae vzr anza na zile nchi ndogo Scandinavian countries, Asian, etc ulaya kuna milolongo Mingi, mm nimeanza kidogo na nitaleta mrejesho hapa mambo yakikaa vzr

Hebu kila mmoja atupe uzoefu wake kwenye Biashara za exportation

Au useme ni sababu gani zinakufanya ushindwe kufanya exportation

=========

Baadhi ya michango...
 

Lasway.Jr

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
220
500
Je mpka sasa unafahamu makampuni mangapi yanayo export mazao nje ya nchi na umejifunza nini?
 

vidmate

JF-Expert Member
May 7, 2018
456
1,000
Je mpka sasa unafahamu makampuni mangapi yanayo export mazao nje ya nchi na umejifunza nini?
Ndugu tuvunjie nondo hizo, mekuchimba profile yako kuna mengi unayajua fanya kututemea madini wengine wataendeleza
 

Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
9,754
2,000
Uzi mzuri sana lakini sitoshangaa ukiwa na wachangiaji wachache.

Binafsi napenda sana Biashara za Exportation kiukweli zinafaida sana na hizi fursa wanafaidi watu wachache wanaojua ABC za kufanya exportation, Kuna mtandao mmoja jina lake limenitoka kidogo huwa nasikia ni wazuri sana kwa kuunganisha international buyer & seller.

Mkuu vipi wewe umeanza jaribu na zao gani??
Hapo kwa museveni serekali hutafuta masoko nakuweka bayana kwa exporters.
 

Nolasc

Member
May 10, 2012
81
125
Biashara ya export inalipa maana ukiwaona wanunuzi wa avocado wanaponunua njombe mpaka wanagombana hasa ulaya product zikiisha. Hivyo tunapaswa kufuatilia kwa makini ili tujue zinaendaje tuache uoga.
 

vidmate

JF-Expert Member
May 7, 2018
456
1,000
Biashara ya export inalipa maana ukiwaona wanunuzi wa avocado wanaponunua njombe mpaka wanagombana hasa ulaya product zikiisha. Hivyo tunapaswa kufuatilia kwa makini ili tujue zinaendaje tuache uoga.
Sera za nchi yetu zinasupport hii kitu au ndo itahitaji vibali lukuki? Hivi gharama za usafiri zinakuwaje mfano parachichi tuseme unaipeleka UK gharama zipoje?
 

vidmate

JF-Expert Member
May 7, 2018
456
1,000
Hapo kwa museveni serekali hutafuta masoko nakuweka bayana kwa exporters.
Hadi raha aisee inatia hamasa, imagine mtu upo bongo na unataka ku export unaanzia wapi kwa mfano? Hao wanunuzi na nchi zenye demand links tunazipatia wapi? Ebhu tupeane maarifa wadau na wengine tuingie mzigoni, natanguliza shukrani
 

tony92

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
560
1,000
Je mpka sasa unafahamu makampuni mangapi yanayo export mazao nje ya nchi na umejifunza nini?
Mpaka sasa namfahamu Hadija Jabiry,kuna home veg wapo arusha pamoja na Kisangani hawa jamaa wa njombe wanaexport avocados.
Kwanza hawa wote ni vijana wadogo sana kiukweli kitu kikubwa nachokiona kutoka kwao ni uthubutu ukisikiliza story zao zinakupa hamasa ya kutolukata tamaa kabisa.
 

vidmate

JF-Expert Member
May 7, 2018
456
1,000
Mpaka sasa namfahamu Hadija Jabiry,kuna home veg wapo arusha pamoja na Kisangani hawa jamaa wa njombe wanaexport avocados.
Kwanza hawa wote ni vijana wadogo sana kiukweli kitu kikubwa nachokiona kutoka kwao ni uthubutu ukisikiliza story zao zinakupa hamasa ya kutolukata tamaa kabisa.
Wapo kwenye social network yoyote? Kama ndio naomba username zao
 

tony92

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
560
1,000
Wapo kwenye social network yoyote? Kama ndio naomba username zao
Ingia Instagram search hadija jabiry utamuona .
Hata Kisangani nao watafute Instagram andika tu Kisangani utawaona.
Hawa jamaa wa Arusha wacheki YouTube andika home veg.
 

Lasway.Jr

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
220
500
Yapo masoko mengi ya bidhaa za hapa ndani huko nje lakini bado tunashindwa kufanya biashara za export tunazidiwa na Kenya, Uganda na sasa hata Rwanda wametuzidi,
Sababu kubwa ya kwanza kwa sasa ni connection
Still watz wana connection ndogo na masoko ya nje, hatuendi kwenye exbihition, hatuko active sana kwenye matumizi ya internet n.k
 
Top Bottom