Kwanini watanzania wengi hawajui/hawafanyi Biashara za Exportation kwenye mazao ya Kilimo? | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini watanzania wengi hawajui/hawafanyi Biashara za Exportation kwenye mazao ya Kilimo?

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Lasway.Jr, Nov 26, 2017.

 1. Lasway.Jr

  Lasway.Jr Senior Member

  #1
  Nov 26, 2017
  Joined: Jul 25, 2015
  Messages: 172
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 80
  Hebu kila mmoja atupe uzoefu wake kwenye Biashara za exportation

  Au useme ni sababu gani zinakufanya ushindwe kufanya exportation

  Mimi nitaeleza kidogo:

  Leo nimeona tujadili kidogo ni kwanini sisi watanzania tunalima na tuna Ardhi nzr sana lakini hatufanyi Biashara kubwa kwenye kilimo yaani exportation , badala yake wakenya ndio wanatupiga Mzinga na kumiliki Biashara hizi Je? Tulichelewa WAP? Au ni nini ambacho hatuji?

  Nitaeleza kwa namna ambavyo nimefanya utafiti wangu na kugundua mambo kadhaaa:

  Kwanza kabisa, watanzania wengi sio wakulima (we a not Farmers rather we are peasants) nikiwa na maanisha kuwa hakuna mtanzania au hata kama wapo ni wachache wanaoweza kulima kuanzia hekari 50+, 100+, 250+ kwa pamoja na kuzalisha bidhaa za kilimo , kwa hyo ni ngumu kufanya Biashara za exportation kwa sababu hatuna vigezo hivyo

  Pili, tulio wengi tumekuwa nyuma sana kwenye matumizi ya teknolojia pamoja na matumizi ya utaalamu kwenye kilimo vitu vya msingi kama soil test, water test, farm planning, post harvesting handling, pack house, ware house management na vingine vingi watanzania wengi hatuvijui na hatuna elimu yake , nimeeleza baadhi ya hivi vitu kwa sababu ili uweze kufanya exportation kwa baadhi ya mazao lazima uwe na certificate za taasisi ya kimataifa ya GAP sasa hawa wana vigezo na masharti yao ambayo yanaendana na vitu nilivyotaja hapo juu

  Nilipokuwa naendelea kufanya utafiti kuona nani ametuloga niligundua kuwa Tanzania hasa wakulima hatuna taarifa sahihi kwenye masoko ya bidhaa za kilimo na pia tumewekuwa watu wa njaa sana na kuuza mazao Yetu Mara tuu tunapovuna kwa kuona fursa ya sisi kuwa wavivu ndio maana wahindi na waarabu ndio nakumbana nao huko masokoni kwenye Biashara kubwa za exportation na wanapata faida kubwa sana sio sana tuu faida kubwa mno (mfano mzr ni kwenye korosho) miaka yote hawa jamaa walikuwa wanapata faida kubwa kiasi gani ? Kwa sababu wakulima wananunua korosho kwa shilingi 500-1500 kwa kilo na sasa korosho hyo hyo inauza 4000 kwa kilo na wananunua just imaging

  Kwa ndugu zetu wakenya matajiri wengi ni wakulima lakini sio ajabu Sana kwa wakenya kutupiga vikumbo kwenye exportation kwa sababu settlers walioanza Kilimo Kenya miaka ya 1885+ mpaka Leo wapo so not bad because their trade back home ndio maana Kenyan wanaexport sana UK, lakini soko lao liko vzr kwa sababu wana certificate za mashamba ambazo hutumika kufanya exportation iwe rahisi hasa kwenye mazao ya matunda na mboga mboga kwa hyo wanachofanya wanakuja Tanzania wananunua mazao Yetu then wana tumia certificate na label zao wanauza ulaya

  Nyingine ni kwamba Tanzania tuna viongozi wengi sana ambao sio wafanyabiasha na wengi ni maskini ndio maana wakienda ulaya wanarudi na laptop na camera na wanasahau kurudi na connection za Biashara , hata wasomi wengi wanaokwenda kusoma wanarudi bila connection yoyote kitu ambacho wakenya wakienda wanarudi na akili ya Biashara kubwa , nafurahia sasa vijana wetu walioenda kusoma China wa nafanya Biashara sasa na jambo jema

  Ukitaka kuanza Biashara ya exportation kwa Tanzania anza na dry food na sio mboga mboga kwa sababu hizi zinahitaji regulations nyingi sana , but grain ziko vzr sana , na pia ukitaka Biashara ya exportation ikae vzr anza na zile nchi ndogo Scandinavian countries, Asian, etc ulaya kuna milolongo Mingi, mm nimeanza kidogo na nitaleta mrejesho hapa mambo yakikaa vzr

  Hebu kila mmoja atupe uzoefu wake kwenye Biashara za exportation

  Au useme ni sababu gani zinakufanya ushindwe kufanya exportation

  =========

  Baadhi ya michango...   
 2. MBITIYAZA

  MBITIYAZA JF-Expert Member

  #41
  Jun 3, 2018
  Joined: Jan 22, 2017
  Messages: 15,308
  Likes Received: 25,061
  Trophy Points: 280
  umesema kweli aisee!
   
 3. T

  Turnkey JF-Expert Member

  #42
  Jun 3, 2018
  Joined: Jul 9, 2013
  Messages: 2,626
  Likes Received: 1,402
  Trophy Points: 280
  Mchawi namba moja CCM...wanajuwa mkiwa na fedha mtawakataa..tajiri hatishiwi nyau na wenyewe wanawafanya wananchi masikini ili waendelee kuwatawala
   
 4. H

  Herr muller Member

  #43
  Jun 4, 2018
  Joined: May 28, 2018
  Messages: 39
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 25
  Welcame sir get in touch with me, thanks
   
 5. H

  Herr muller Member

  #44
  Jun 4, 2018
  Joined: May 28, 2018
  Messages: 39
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 25
  Umenena kaa mfalme suleiman, i mean king solomon, if you want to control people, deny them 2 thnaings EDUCATION and WEALTH, na ndio tz watu wengi huchagua ccm ,nandio tz itabaki nyuma kabisa, barikiwa mkuu
   
 6. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #45
  Jun 4, 2018
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,100
  Likes Received: 717
  Trophy Points: 280
  Good thread
   
 7. M

  Mass63 Member

  #46
  Jun 4, 2018
  Joined: Dec 31, 2016
  Messages: 12
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 5
  Thanks ndugu for your inputs. Machache umeongea lakini yametufungua kichwa.
   
 8. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #47
  Jun 4, 2018
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 11,342
  Likes Received: 3,383
  Trophy Points: 280
  Najifunza
   
 9. titimunda

  titimunda JF-Expert Member

  #48
  Jun 4, 2018
  Joined: Nov 26, 2014
  Messages: 5,602
  Likes Received: 6,114
  Trophy Points: 280
  Changamoto nilizoziona kwa upande wangu ni 1.sera mbovu za serikali,wakati wenzetu wanapambana kuwatafutia na kulinda masoko ya bidhaa za nchi zao,sie huku tunafanyiana roho mbaya tu na kila siku kuwekeana mazuio,
  2.vibali,kuvipata mpaka uhonge sana,usumbufu na ukiritimba mwingi mno,again ROHO MBAYA.
  3.Uelewa na mwamko mdogo,ingawa tunaanza kupata akili taratibu
  4.kutokuwa na viwanda vya kutosha,hususani vidogovidogo vya kuongeza thamani.
   
 10. genius17

  genius17 New Member

  #49
  Jun 4, 2018
  Joined: Jun 2, 2018
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  kha
   
 11. Comrade 01

  Comrade 01 JF-Expert Member

  #50
  Jun 4, 2018
  Joined: Feb 27, 2015
  Messages: 257
  Likes Received: 190
  Trophy Points: 60
  Changamoto ni nyingi sana.Lakini sera pia ni mbovu,unaweza ukaenda wizara ya viwanda na biashara wale maafisa wa masoko nao wanataka wawe madalali ili kupata connection ya soko na ABC zake.
  Kuna kipindi nilikuwa nafanya biashara ya nyama ya mbuzi nimekutana na hivi vitu.
  Kuna mtu kaongelea nyanya,hapo Angola kuna soko zuri tu la nyanya.Wanauza kwa kilo na hufikia hadi US dola kumi kwa kilo kulingana na msimu.

  Ukienda Makete,kuna matufaa(apples) mazuri tu tena makubwa kama yale ya South Africa tena ni ya asili sio GMO.Lakini hayana soko.
   
 12. Lady Ra

  Lady Ra JF-Expert Member

  #51
  Jun 4, 2018
  Joined: Mar 23, 2014
  Messages: 755
  Likes Received: 638
  Trophy Points: 180
  Mi nadhani kua Mazao kwanza yamegawanyika katika makundi makuu mawili, ya matunda na nafaka (kunaweza kuwepo makundi mengine).
  Mazao ya matunda ni perishable so yanahitaji extra utunzaji ili yaweze kufika salama huko yaendako. Huu utunzaji wa extra ni gharama, pengine uwe na friji au friza so ndio maana wengi hushindwa hizi gharama za kuyatunza.

  Mazao ya Nafaka ni Durable ila sasa return yake sio kivile, mpaka uweze ku export mazao mengi.

  Lakini tatizo jingine ni soko au taarifa za soko. Wengi hawajui wapi yalipo masoko ya mazao mbali mbali huko kwengineko duniani
   
 13. M

  Massanda OMtima Massanda JF-Expert Member

  #52
  Jun 4, 2018
  Joined: Jun 27, 2017
  Messages: 842
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 80
  Muda mwingi tumekuwa tukijikita kwenye kilimo cha kujikimu (subsistence farming) ambacho mara nyingi hakizalishi ziada ya kutosha.
  Pili, taifa letu kwa muda mrefu halijawa na sera ya kuwawezesha wakulima kuona kilimo kama chachu ya kujikomboa kiuchumi. Wala kuweka mazingira ambayo wakulima wanaweza kutumia ardhi yao kama mdhamana kaika kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha (mabenki) ili kuimarisha mitaji yao.
  Tatu, balozi zetu za nje na zile zinazowakilishwa hapa kwetu, zimechelewa kuwa na economy deplomacy. Mabalozi wetu wa pande zote hawajajiingiza kwenye kutafuta masoko na kuwaunganisha wakulima na masoko hayo, ukiachilia mbali yale yanayouzwa moja kwa moja na serikali.
  Nne, wengi wenye fedha hufikiria namna ya kuzungusha fedha yao kwa njia za haraka haraka zisizokuwa na usumbufu (low risk). Kwa maana nyingine hawako na moyo wa ujasiliamali na ubunifu.
  Tano, ukosefu wa elimu na ufahamu mdogo wa lugha ya mawasiliano.
  Sita, maafisa ugani wetu wamekuwa wa maofisini. Hawatembelei wakulima ili kuwapa maarifa, ili hata kwa kilimo cha jembe, walime kwa tija!
   
 14. M

  Mzee Mukaruka JF-Expert Member

  #53
  Jun 4, 2018
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Well said shemeji, yote uliyosema ni KWELI NA KWELI TUPU. Lakini sasa TUFANYEJE ili tupone!?
   
 15. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #54
  Jun 4, 2018
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,468
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Will get in touch. I have just started greenhouse farming for vegetables.
   
 16. H

  Herr muller Member

  #55
  Jun 4, 2018
  Joined: May 28, 2018
  Messages: 39
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 25
  WAITTING FOR YOU SIR GET INTOUCH PLEASE, be blessed
   
 17. M

  Mzuru Member

  #56
  Jun 4, 2018
  Joined: May 17, 2018
  Messages: 19
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Tutaelewa ndugu
   
 18. Lasway.Jr

  Lasway.Jr Senior Member

  #57
  Jun 4, 2018
  Joined: Jul 25, 2015
  Messages: 172
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 80
  Well said Sir , Mimi kama mtoa mada niliona tatzo kubwa sana kwenye hii biashara na nikaamua kuandika uzi huu hapa
  Mimi ni mtaalamu wa kilimo na nafanya kazi na wakulima wengi sana kwa sasa na ni Imani yangu kuwa kama masoko ya nje yataimarika nitakuwa na soko kubwa sana na nitafurahi Zaidi kuona wakulima wangu wakiwa na hali nzuri ya kifedha na kupata faida kubwa na biashara yangu itakuwa kubwa Zaidi

  Nimejaribu kuzunguka maeneo mengi .... unlocking the potential na nikagundua kwa kweli watanzania tuna kazi ya ziada ya kufanya ili tuweze kuwa na maisha bora Zaidi

  Naomba tuwasiliane tuyajenge
   
 19. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #58
  Jun 4, 2018
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 5,106
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Tanzania ni nchi ya maneno mengi vitendo nill.
  Kumbuka hasara waliyopata wakulima kuzuia kuuza mazao nje.
  Hakuna fidia wala kujali ni story tuu!!
   
 20. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #59
  Jun 4, 2018
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 5,106
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Vikwazo vingi na sera mbovu ni vikwazo vya uchumi.
  Maua na mboga kuexport kupitia Nrb, cargo flights zinakwepa gharama!!
   
 21. M

  Malila JF-Expert Member

  #60
  Jun 5, 2018
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,483
  Likes Received: 893
  Trophy Points: 280
  kwema kaka,
  asante kwa kutukumbusha umuhimu wa kufanya biashara kimataifa kupitia kilimo. Yote yaliyosemwa yapo, ila hayataondoka kwa porojo. Vitendo vitaondoa hizi changamoto.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...