Kwanini watanzania wengi hawajui/hawafanyi Biashara za Exportation kwenye mazao ya Kilimo? | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini watanzania wengi hawajui/hawafanyi Biashara za Exportation kwenye mazao ya Kilimo?

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Lasway.Jr, Nov 26, 2017.

 1. Lasway.Jr

  Lasway.Jr Senior Member

  #1
  Nov 26, 2017
  Joined: Jul 25, 2015
  Messages: 172
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 80
  Hebu kila mmoja atupe uzoefu wake kwenye Biashara za exportation

  Au useme ni sababu gani zinakufanya ushindwe kufanya exportation

  Mimi nitaeleza kidogo:

  Leo nimeona tujadili kidogo ni kwanini sisi watanzania tunalima na tuna Ardhi nzr sana lakini hatufanyi Biashara kubwa kwenye kilimo yaani exportation , badala yake wakenya ndio wanatupiga Mzinga na kumiliki Biashara hizi Je? Tulichelewa WAP? Au ni nini ambacho hatuji?

  Nitaeleza kwa namna ambavyo nimefanya utafiti wangu na kugundua mambo kadhaaa:

  Kwanza kabisa, watanzania wengi sio wakulima (we a not Farmers rather we are peasants) nikiwa na maanisha kuwa hakuna mtanzania au hata kama wapo ni wachache wanaoweza kulima kuanzia hekari 50+, 100+, 250+ kwa pamoja na kuzalisha bidhaa za kilimo , kwa hyo ni ngumu kufanya Biashara za exportation kwa sababu hatuna vigezo hivyo

  Pili, tulio wengi tumekuwa nyuma sana kwenye matumizi ya teknolojia pamoja na matumizi ya utaalamu kwenye kilimo vitu vya msingi kama soil test, water test, farm planning, post harvesting handling, pack house, ware house management na vingine vingi watanzania wengi hatuvijui na hatuna elimu yake , nimeeleza baadhi ya hivi vitu kwa sababu ili uweze kufanya exportation kwa baadhi ya mazao lazima uwe na certificate za taasisi ya kimataifa ya GAP sasa hawa wana vigezo na masharti yao ambayo yanaendana na vitu nilivyotaja hapo juu

  Nilipokuwa naendelea kufanya utafiti kuona nani ametuloga niligundua kuwa Tanzania hasa wakulima hatuna taarifa sahihi kwenye masoko ya bidhaa za kilimo na pia tumewekuwa watu wa njaa sana na kuuza mazao Yetu Mara tuu tunapovuna kwa kuona fursa ya sisi kuwa wavivu ndio maana wahindi na waarabu ndio nakumbana nao huko masokoni kwenye Biashara kubwa za exportation na wanapata faida kubwa sana sio sana tuu faida kubwa mno (mfano mzr ni kwenye korosho) miaka yote hawa jamaa walikuwa wanapata faida kubwa kiasi gani ? Kwa sababu wakulima wananunua korosho kwa shilingi 500-1500 kwa kilo na sasa korosho hyo hyo inauza 4000 kwa kilo na wananunua just imaging

  Kwa ndugu zetu wakenya matajiri wengi ni wakulima lakini sio ajabu Sana kwa wakenya kutupiga vikumbo kwenye exportation kwa sababu settlers walioanza Kilimo Kenya miaka ya 1885+ mpaka Leo wapo so not bad because their trade back home ndio maana Kenyan wanaexport sana UK, lakini soko lao liko vzr kwa sababu wana certificate za mashamba ambazo hutumika kufanya exportation iwe rahisi hasa kwenye mazao ya matunda na mboga mboga kwa hyo wanachofanya wanakuja Tanzania wananunua mazao Yetu then wana tumia certificate na label zao wanauza ulaya

  Nyingine ni kwamba Tanzania tuna viongozi wengi sana ambao sio wafanyabiasha na wengi ni maskini ndio maana wakienda ulaya wanarudi na laptop na camera na wanasahau kurudi na connection za Biashara , hata wasomi wengi wanaokwenda kusoma wanarudi bila connection yoyote kitu ambacho wakenya wakienda wanarudi na akili ya Biashara kubwa , nafurahia sasa vijana wetu walioenda kusoma China wa nafanya Biashara sasa na jambo jema

  Ukitaka kuanza Biashara ya exportation kwa Tanzania anza na dry food na sio mboga mboga kwa sababu hizi zinahitaji regulations nyingi sana , but grain ziko vzr sana , na pia ukitaka Biashara ya exportation ikae vzr anza na zile nchi ndogo Scandinavian countries, Asian, etc ulaya kuna milolongo Mingi, mm nimeanza kidogo na nitaleta mrejesho hapa mambo yakikaa vzr

  Hebu kila mmoja atupe uzoefu wake kwenye Biashara za exportation

  Au useme ni sababu gani zinakufanya ushindwe kufanya exportation

  =========

  Baadhi ya michango...   
 2. Penelope

  Penelope JF-Expert Member

  #21
  Feb 13, 2018
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 498
  Trophy Points: 80
  Yani hii week nilikua na search juu a hili swala na leo nimejaribu jf ndo nikabahatika kuona uzi huu.. Lasway.Jr
   
 3. wegman

  wegman JF-Expert Member

  #22
  Feb 13, 2018
  Joined: Jan 8, 2016
  Messages: 931
  Likes Received: 803
  Trophy Points: 180
  Mkuu ile site inaitwa Trade Key link yake ni hiyo chini.

  www.importer.tradekey.com

  Ila sasa nilichogundua ni kuwa watu wengi waliojaribu kuitumia hii site wametoa review zao kuwa hii site haipo real ni scam ndio maana nilikuwa napata wasi wasi kuiweka hapa.

  Nimesikia juu juu kuna watu wanatumia Alibaba pia kufanya export ndio nataka nilifanyie uchunguzi nalo nione sababu wote tunajua Alibaba wapo real.
   
 4. i

  iamwhoiam Member

  #23
  Feb 14, 2018
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 5
  Wapo wakulima kutoka Arusha wana export maazao yao kwenda nje, kuna Serengeti fresh, africado na wengineo
   
 5. Ahmed1

  Ahmed1 Member

  #24
  Feb 14, 2018
  Joined: Nov 27, 2017
  Messages: 43
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 25
  Nimependa hii thread ila kama unavyo jua wa Tanzania wengi ni masikini kiuchumi ila tuna resources za kutosha mimi nikiwemo na hizi ishu ya exportation ninaiota kila siku naishia kufarijika tu napoziona hizi threads ila ni nacho kiomba ni pate master plan and full procedures on how to do this mtakua mmenisaidia sana
   
 6. c

  conservative3 JF-Expert Member

  #25
  Feb 14, 2018
  Joined: Nov 12, 2013
  Messages: 666
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  MOSI, HATUPENDI KUTAFUTA TAARIFA, KWA KIFUPI MALEZI NA TABIA ZA KIMAZOEA, TUNATAMANI KILA SIKU SERIKALI ILETE KITU, LABDA KUNGEKUWA NA KODI YA KICHWA TUNGEWAJIBIKA IPASAVYO,TUNAPENDA LAUMU

  PILI, SOKO NI MUDA, TUNAJALI MUDA ILA HATUNA NIDHAMU YA MUDA NA UZALISHAJI, KURASIMISHA BIASHARA NK

  TATU, MZUNGU ANAMWAMINI MZUNGU; AKIKOSA MZUNGU NDO ANAKUJA KWA MWAASIA NA MWAFIRKA.

  KENYA NGOZI NYEUPE NDO ILIANZA KUSHIKA IYO BIASHARA KULIKO NGOZI NYEUSI KUTUKANA NA HISTORIA ZETU ZA MAMBO YA UHURU NA MILENGO YA KISIASA.

  NNE, WATANZANIA HATUNA SHIDA, HAKUNA MWEZI AMBAO HAKUNA MKOA AMBAO HAUZALISHI ZAO,SHIDA HULETA AKILI, AKILI HUONGEZA UBUNIFU NA UGUNDUZI.
   
 7. Mkaruka

  Mkaruka JF-Expert Member

  #26
  Feb 15, 2018
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 9,568
  Likes Received: 6,397
  Trophy Points: 280
  Lasway.Jr unaweza kutusaidia kujua ni mambo gani muhimu na procedure gani huwa zinatumika mpaka export inafanyika ?
   
 8. mzeewangese

  mzeewangese JF-Expert Member

  #27
  Jun 3, 2018
  Joined: Feb 11, 2016
  Messages: 532
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 80
  Nataka kuanzaa ku export karafuu iliki soko lake lipo vipi na procudure zake
   
 9. MBITIYAZA

  MBITIYAZA JF-Expert Member

  #28
  Jun 3, 2018
  Joined: Jan 22, 2017
  Messages: 15,308
  Likes Received: 25,061
  Trophy Points: 280
  binafsi mie nilitafuta soko lakuexport strawberries botswana !dili zuri ..lakin nilinyoosha mikomo mm !kama ulivyosema Lasway.Jr kueport dry foods hapo sawa !mie walisema had wapime water contents ya matunda,plus udongo pia !mambo kibao !
   
 10. r

  ruaharuaha JF-Expert Member

  #29
  Jun 3, 2018
  Joined: Feb 14, 2018
  Messages: 537
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 80
  Hii biashara ni nzuri sana lakini kwa kuanza inabidi kujipanga kama kikundi ili kufuatilia vibali vyote, kutimiza masharti yote na kuwa na mtaji wa kutosha.
   
 11. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #30
  Jun 3, 2018
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 12,067
  Likes Received: 3,678
  Trophy Points: 280
  mleta mada, wataalamu wapo, Ebu Nenda Shule Biashara ya Kilimo (Agricultural Economics and Agribusiness) ipo chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine. Morogoro. wAnazo taarifa za kutosha kuhusu masuala uliyouliza.
  ===
  Hata hivyo Nakushukuru kwa ku'provock' suala hili. Hakuna kipindi nilikasikirikia wizara inayohusu maswala ya biashara kama kipindi cha mwaka Juzi Nyanya zilivyokuwa nyingi sokoni kiasi cha watu kushindwa kuvuna mazao hayo kutokana na bei ndogo, wakati huko Nageria Nyanya mmoja inauzwa shilingi mia tatu za kitanzania. Na mashirika ya utangazaji ya kimataifa yalikuwa yakipiga kelele kuhusu uhaba wa Nyanya nchini Nigeria. Hakuna kilichofanyika kusaidia wakulima wetu. Sidhani kama Nigeria wana mlolongo lukuki wa vibali kuingiza mazao kilimo kama EU wafanyavyo. Hapa nitaomba usaidizi wa taarifa. Kuhusu wizara yetu ya biashara Kama kuna lililofanyika wakati huo wa balaa la bei ya Nyanya naomba kujulishwa.
   
 12. Macho ya panzi

  Macho ya panzi Member

  #31
  Jun 3, 2018
  Joined: May 13, 2018
  Messages: 48
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 25
  Hapa kwetu tatizo kubwa ni sera nzuri kwakila nyanja watu wanaogopa kupoteza unaweza kuangaika na kilimo miaka nenda mika rudi ukatafuta soko ukaanda mzigo mala serekali imepiga marufuku kusafirisha mazo nje kisha serekali inakupangia sehemu ya kuuza mazao yako watu wanaogopa kufelishwa
   
 13. H

  Herr muller Member

  #32
  Jun 3, 2018
  Joined: May 28, 2018
  Messages: 39
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 25
  Hallo i am a kenyan based in the European union, nitajitahidi kuandika na swahili ila munajua sisi wakenya swahili yetu ni ya kuomba maji na pia nafahamu nikiandika na english wemgi hapa hawataelewa, na sisemi hivyo kwa ubaya dada na kaka zangu wabongo na pia masemeji wangu maana nafikiri nitaoa huko kwenu, sasa tuingia kwa hii jambo la export, kweli vile huyu kaka amesema kuexport to european union kuna masariti magumu sana hata kenya iko muda walifunguwa kuexport hapa EU sababu ya kitu tunaita MLI, yaani ni chemicals ngapi ziko kwa hio tunda au mboga, na pia unahitaji hii kitu inaitwa GAP yaani hio inaoyesa vile mazao huaza toka mbegu mpaka inafika kuexport, kazi hio, kenya iko na ardhi dogo sana lakini inatengeneza billions of shillings kila mwaka na export of fresh produce, ila tz mko na ardhi tele rotuba nzuri lakini munatengeneza hela chache sana kutoka export of farm produce, WHY, kwanini, moja elimu ni changamoto huko bongo, 2 hamna viongozi ambao wanajali taifa lenu, 3 wakulima hawana hela na maarifa ya kisasa, kaa irragation, greenhouses , cold stroge facilities, sababu ni nyingi.tz ni taifa mungu aliibariki kabisa, lakini elimu na uongozi ndio changamoto. hebu fikiria tz ndio wenye mifugo mingi nambari 2 africa, lakini munaangiza nyama toka nje ya nchi, mko na over 2,000 coastline, mko na 3,000 rufiji delata acres amazo munaweza kuuza kufunga na kuuza schrimps and crabs, good mashamba ambapo munaweza kuza avocados and hortculture na mutengeneza billions every year, lakini hamna hilo.tz needs a seriuos investor in agriculture ambae atafundisha watu jinsi ya kufanya hii export of produce from tz. mwaka huu naja hapo tz na nitasirikiana na TAHA, and pia sugcot kuona ni vipi, kwahivyo jambo ninalosema kila muda ni kuwa ukasagundua tatizo, iliobaki ni kutafuta suluhiso,so kaa kuna yeyote ambae angehitaji either maarifa zaidi maana niko tayari na connection hapa EU na sio eu to hata asia and australia anaweza wasiliana nami toungee zaidi nikifika tuone vile tunaweza saidiana, mimi naamini kuwa mungu alituweka katika hii dunia tusaidiane, asanteni sana, sijui swahili yangu vipi, ukiwa intrested na hii bussiness get in touch pls, thank you
   
 14. Half Genious

  Half Genious JF-Expert Member

  #33
  Jun 3, 2018
  Joined: Feb 28, 2017
  Messages: 272
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 80
  Mifumo ya elimu hata viongoz hawana uelewa nini kifanyike sababu tangu zaman tulikuwa tunalima ili tusife njaa na wakati kilimo biashara kimeanza miaka ya karibun so tumejikuta wote kianzia viongoz had walimu hawajui wstufundishe nini sababu ns wenyewe hawajui....ila wapo wabonho wanaopekua pekua mambo ndio tunaona umuhimu wa kuuza nje hapo huja,ungumzia mazuio ya kila siku...mi napenda hizo mishe ila vikwazo vingi haswa vya Quality za kimataifa viongoz wanatuambia tu china wanataka muhogo wa Quality gani hawasemi hata nyama kabla ya kuuza wanataka record ya mnyama matibabu na malisho yake anakula majan ya sina gani na amechinjwa vip but unawasikia viongoz majukwaan wanasema tuna mifungo mingi africa kwanini hatuuzi nyama...utamuuzis nani nyama ng'ombe katembea km 50 kutafuta malisho na maji...kikubwa hatuna elimu na wanaotuongoza hawajui wafanye nini!
   
 15. Half Genious

  Half Genious JF-Expert Member

  #34
  Jun 3, 2018
  Joined: Feb 28, 2017
  Messages: 272
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 80
  Qm interested yapo mazao mengi na sehrm nyingi tunaweza kuangalia namna ys kufanya
   
 16. Adolf Hitler Jr

  Adolf Hitler Jr Member

  #35
  Jun 3, 2018
  Joined: Sep 13, 2016
  Messages: 81
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 25
  Hapo ni fitna tu hamna jipya sijui nani katuroga
   
 17. Mr Mwaka

  Mr Mwaka Member

  #36
  Jun 3, 2018
  Joined: Nov 14, 2017
  Messages: 5
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Hakuna kinachoshindikana tukiamaua, tatizo letu wa TZ hatuna uthubutu.....!
   
 18. H

  Herr muller Member

  #37
  Jun 3, 2018
  Joined: May 28, 2018
  Messages: 39
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 25
  Get intouch with me pls, be blessed, yes in tz you have very very large tracks of fertile land sir
   
 19. m

  mbwewe JF-Expert Member

  #38
  Jun 3, 2018
  Joined: Sep 10, 2014
  Messages: 820
  Likes Received: 691
  Trophy Points: 180
  @mbiyitaza dadangu nikupe siri kwenye ujasiriamali kwenye changamoto nyingi hpo ndyo hela ilipo badala ya kukata tamaa unatakiwa utafute solution once utakapopata solution mambo mengine yooote yatakaa kwenye mstari
   
 20. Ramp Agent

  Ramp Agent JF-Expert Member

  #39
  Jun 3, 2018
  Joined: Mar 27, 2013
  Messages: 266
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  Well said Sir! Mchawi wetu ni akili zetu wenye. The way we don't allow our mind to look in big picture and this start from our Tz leaders (government) to citizen. So far am interested with it sir, nahis naweza jifunza kitu
   
 21. Ramp Agent

  Ramp Agent JF-Expert Member

  #40
  Jun 3, 2018
  Joined: Mar 27, 2013
  Messages: 266
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  Well said Sir! Mchawi wetu ni akili zetu wenye. The way we don't allow our mind to look in big picture and this start from our Tz leaders (government) to citizen. So far am interested with it sir, nahis naweza jifunza kitu
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...