Kinyungu
Platinum Member
- Apr 6, 2008
- 21,581
- 42,891
Ukichunguza kwa makini mwenendo wa uwekezaji wa Watanzania wazawa (weusi), kuna swali la msingi ambalo tunapaswa sisi kama wazawa wa nchi hii kujiulizwa kwa ujasiri na kutafuta majibu yenye mantiki ya kijamii, kiuchumi na kihistoria. Swali hili la muhimu linatokana na ukweli kwamba wanaoshikilia uchumi wa Tanzania ni kwa sehemu kubwa jamii ya watu Wachache wa asili ya Asia Kusini, Kiarabu na Wazungu.
Swali la kujiuliza ni "Kwa nini Watanzania wazawa wengi weusi, wawe ni wale waliosoma, viongozi wa serikali na chama wenye uwezo wa kifedha, diaspora huwekeza zaidi kwenye biashara ndogondogo kama maduka, migahawa, Usafirishaji wa Abiria na mizigo, lodge na guest house, badala ya kuanzisha viwanda vya kuzalisha bidhaa?
Wakati wahindi, waarabu na hata jamii ya wachache wa kizungu walioko nchini wamejikita katika viwanda vya usindikaji, utengenezaji bidhaa, na biashara zenye mtandao mkubwa wa thamani, wazawa wengi bado wanabaki kwenye sekta isiyo na mchango mkubwa katika kuongeza ajira au pato la taifa. Hata ukiangalia hali ya kilimo chetu jamii hiyo ya wageni ndiyo wenye kulima mashamba makubwa na wanaopeleka kwa wingi bidhaa zao nje ya nchi
Ukiuliza wasomi na viongozi wa serikali wanatoa sababu kuu za hali hii ni pamoja na urithi wa kihistoria wa mfumo wa kikoloni na wa baada ya uhuru, ambapo wazawa walinyimwa fursa za kiuchumi kwa miongo kadhaa.
Wakati wa ukoloni wazawa hawakuwa na mitaji; na wale wachache waliokuwa na mitaji hawakuwa na uthubutu wa kuwkeza katika Viwanda. Mara baada ya uhuru nchi iliingia kwenye siasa za Ujamaa ambayo iliona utajiri wa mtu binafsi, familia au mkoa kuwa kama aina ya unyonyaji na hivyo wengi waliona aibu kutafuta mali kwa bidii ili wasije wakaonekana matajiri mbele ya jamii.
Hali hii ilisababisha vizazi vyao kukosa urithi wa mitaji, elimu ya biashara ya viwanda, na mifumo ya urithi wa viwanda (industrial inheritance). Zaidi ya hayo, mfumo wa elimu na uongozi wa sasa haujajikita katika kujenga maono ya kimkakati ya kizalendo ya kuwekeza kwenye sekta ya uzalishaji kama ilivyo kwa mataifa yaliyoendelea. Watanzania wengi wanaogopa kuanzisha viwanda kutokana na ukosefu wa maarifa ya kiufundi, kutokuwepo kwa mifumo ya kusaidia wenye ndoto kubwa, pamoja na ukosefu wa mitaji ya kati na mikubwa. Badala yake, wanakimbilia “biashara salama” zisizo na hatari kubwa kama maduka na migahawa.
Hata wale waliofanikiwa kifedha – wakiwemo viongozi wa kisiasa, watumishi wakubwa wa umma, na wasomi – bado wana tabia ya kuwekeza katika maeneo ya matumizi ya haraka (maduka, nyumba za kupanga, magari, na guest house) badala ya viwanda vya kuongeza thamani ya malighafi zetu kama mazao ya kilimo, ngozi, madini na hata taka.
Hali hii ni matokeo ya mfumo wa kisiasa na kijamii usiowajibika kuhimiza uwekezaji wa kimkakati. Pia, kuna hofu ya kuonekana umefanikiwa zaidi ya inavyokubalika kijamii (social intimidation), ambapo baadhi ya watu huogopa kuwekeza katika viwanda vikubwa kwa kuhofia kuhusishwa na ufisadi au kudhaniwa kuwa ‘wamejilimbikizia mali.’ Hii inanyima taifa kizazi cha wazalishaji wakubwa wazawa, hali ambayo ni hatari kwa uhuru wa kiuchumi wa muda mrefu.
Ni wakati muafaka sasa kwa serikali ya Tanzania na vyombo vyake – pamoja na vyama vya siasa na taasisi za kifedha – kuhamasisha mabadiliko ya fikra kwa kusaidia kwa makusudi Watanzania weusi kuwekeza katika viwanda. Serikali inaweza kuanzisha sera maalum za usaidizi wa mitaji, upatikanaji wa teknolojia, pamoja na urahisishaji wa masoko kwa wale wanaotaka kuingia katika sekta ya viwanda. Viongozi walioko madarakani, ambao wengi wao wana rasilimali kubwa, hawapaswi kuwekeza kwenye anasa tu bali waonyeshe mfano kwa kuwekeza kwenye viwanda vya msingi kama vya usindikaji wa mazao, vifaa vya ujenzi, vifaa vya kielektroni, vifaa vya hospitali, mitambo na vifaa vya shule. Hii si tu kwamba itaongeza ajira na mapato ya taifa, bali pia itawawezesha Watanzania wazawa kujiamini, kudhibiti uchumi wao na kusitisha utegemezi wa bidhaa kutoka nje.
Kujenga taifa imara kiuchumi kunahitaji mapinduzi ya fikra, ujasiri wa kuchukua hatua kubwa, na ushawishi kutoka kwa serikali, vyombo vya fedha, na wasomi. Wazawa hawapaswi kuona viwanda kama ndoto za matajiri wa nje bali kama njia halisi ya ukombozi wa kiuchumi wa nchi yao. Serikali na taasisi zake ziwafikie wenye ndoto hizi, ziwaandalie mazingira, na waweke mikakati ya kuona hadi viongozi wa kisiasa na kiuchumi wanakuwa miongoni mwa waanzilishi wakuu wa viwanda vya kimkakati nchini. Huu ndio msingi wa kujitegemea kiuchumi na kupunguza pengo kati ya matajiri wa kihindi, kiarabu na kizungu na Watanzania wazawa.
Serikali yetu isione aibu kuiga sera za Serikali ya nchi zilizofanikiwa kama Korea Kusini, Taiwan, Singapore ama Malysia,.ikiwezekana icopy sera hizo ili kuwezesha nchi yetu kujikwamua katika hali ngumu tuliyonayo. Nchi haitaweza kuendelea kwa uchuuzi wa bidhaa za kutoka nje bali kwa sera madhubuti zitakazo wawezesha watanzania wazawa na wageni kuzalisha nchini kupitia mtandao wa viwanda vitakavyoongeza thamani ya mazao yetu pamoja na malighafi zinazopatikana nchini