Kwanini Watanzania walio ughaibuni wanafanya vizuri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Watanzania walio ughaibuni wanafanya vizuri?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kitumbo, Dec 23, 2011.

 1. Kitumbo

  Kitumbo JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 547
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Katika Rai ya Jenerali Ulimwengu ya "Miaka 50 ya Tanganyika, maswali hamsini ya kujiuliza" (Raia Mwema no.218), swali la 32 Jenerali ameuliza; "Ni kwa nini Watanzania walio ughaibuni wanafanya vizuri kutumikia nchi nyingine lakini wakiwa nyumbani wanakuwa hawafai?"
  Wana JF, nimevutwa sana na swali hili na nitashukuru kama nitapata maoni yenu kutoa majibu au mitazamo.
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Labda system ya ughaibuni inawafanya kutumikia vizuri kulinganisha na system ya nyumbani. Tuchukulie kwa mfano ulikuwa unafanya kazi CNN halafu ukaamua kurudi kufanya kazi TBC. Sio kwamba hawafai, bali system yenyewe. Hata Tido Mhando yalimshinda.
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  A chain is as strong as it's weakest link. Hata uwe mzuri vipi, kama system unayofanyia kazi haikupi support ukaweza kufanya at your best, huwezi kufanya at your best.

  Wewe umerudi na midegree yako, unataka kuja kuendesha mambo kisomi, unakuta kuna vizee vimekalia ofisi vinaiendesha miaka nenda miaka rudi kwa uzoefu tu, halafu havitaki hata kusikia habari zako za usomi.Tena vimekalia kulogana na kufungiana safari Mlingotini.

  Unafikiri unaweza kuleta mabadiliko hapo?
   
 4. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Umeongea kwa uchungu mdau! Hili linakera kwa kweli
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Poor system. Msomi gani atakalia ofisi kufukizia ufumba kuziba uozo wa viongozi kila kukicha, na kusimama majukwaani kusifia kana kwamba mtu huna akili vile? Walio nje wajapo home wanashtukia sana hilo na wengine wanadiriki hata kurudi walikotoka kwani hawakutupa jongoo na mti wake.

  Kashfa nzito za akina Jairo katu hata siku moja haziwezi kufumbiwa macho kwa mataifa yenye kufuata taratibu, sheria na nidhamu ya kazi. Pamoja na kuanikwa hadharani na vyombo mbalimbali licha ya mhimili wa bunge kulivalia njuga hakuna kinachoendelea na pale magogoni wanaendelea kumlinda mjasiriulaji na wanyonge tunabaki kunyongeka.
   
 6. U

  Uwilingiyimana Member

  #6
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunayo matatizo mengi, makubwa, hapa nyumbani. Moja ya matatizo hayo ni kwamba hapa kwetu siasa ndiyo injini, na utaalam ndiyo ''lubricating oil''. Kwa wenzetu, utalaam ndiyo injini, siasa na upuuzi mwingine wa namna hiyo ni lubricant tu!
   
 7. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  ukiwa nje utafanya kazi chini ya uongozi, ukirudi tz utafanya kazi chini ya utawala
   
 8. V

  Victor Jeremiah Member

  #8
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nchi yetu inaendeshwa kisiasa zaidi. michango yetu mingi haithaminiki sababu haiendi ktk ratiba ya kisiasa.
  mfano kukiwa na mpango mzuri wa kimaendeleo,ambao utachukua muda mrefu kuliko kipindi atachokaa waziri/mbunge/diwani madarakani,basi utapigwa chini bila kujali umuhimu/uthamani wake ktk nchi.
  Mambo yatakayopewa kipaumbele niyale yatakayoweza kufanikiwa ndani ya kipindi cha uongozi flani,ili wapate sababu ya kuwaita waandishi wa habari na kuzungumza.
   
 9. B

  Bi Mashavu Member

  #9
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijaelewa Swali, Wanafanya vizuri kwenye kitu gani? Labda utupe na mfano wa kilichofanywa vizuri na watanzania huko ughaibuni ndo tuchangie mada. If you are being told what to do, how to do it and when to do it tena under absolute supervision huwezi kuthubutu kusema unafanya vizuri kama akili yako iko sawa.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280

  Huu ndio ukweli wa mambo Mkuu.
   
Loading...