Kwanini watahiniwa hawaruhusiwi kufanya haya wakiwa kwenye chumba cha mtihani?

PRINCEd

JF-Expert Member
Dec 14, 2015
860
619
Wakati nchi iko katika hoja nzito ya uhalali wa vyeti vya mh RC
Kuna kitu nimekikumbuka ambacho nimeshindwa kupata majibu...

"Hakuna mtahiniwa anayeruhusiwa kutoka nje ya chumba cha mtihani nusu saa baada ya mtihani kuanza au nusu saa kabla ya mtihani kumalizika""

"Hakuna mtahiniwa anayeruhusiwa kuingia chumba cha mtihani nusu saa baada ya mtihani kuanza"

Makatazo hayo au sheria au utaratibu huo ulenga nini au ukwepa kitu gani???
Naomba kuwasilisha...
 
Sio nusu saa baada ya mtihani kuanza bali ni nusu saa kabla ya mtihani kuanza,maana ukitoka kabla ya nusu saa kumbuka unaweza kutana na wale ambao wanaruhusiwa kuingia kabla ya nusu saa kupita...hivyo ili kuzuia mtu aliyetoka ndani yA chumba cha mtihani na aneyekuja kukutana.... Hakuna mwanafunzi ambaye anaruhusiwa kutoka kabla ya nusu saa ila wanaruhusiwa kuingia na pia baada ya nusu saa kupita mwanafunzi anaruhusiwa kutoka nje na wanje haruusiwi kuingia ndani hivyo hata wakipeana maswali au majibu haita saidia chochote maana wanje hatoruhusiwa kuingia ndani.
 
Nina mashaka kama una uzoefu na sheria za mitihani!
 
Thread imeisha maelezo yamejitosheleza kabisa
 
Na watahiniwa hawaruhusiwi kutoka nusu saa kabla ya mtihani kuisha ili kuwepo na mashuhuda wa tukio la uhesabuji na ufungwaji wa mitihani kwenye zile bahasha, na pia mmoja wa watahiniwa aweze kutia sign kwamba amehahakisha idadi ya mitihani iko sawa, na imewekwa na kufungwa kwenye bahasha.
 
Sijakulazimisha... Mimi nimeandika nachofahamu kama kuna kosa ni bora ungefuunguka ili ukweli ufahamike nasikujifanya unamashaka juu yangu bila kuja na reasons.
Kama ungekuwa mwl uliyewahi kusimamia mtihani ungejua tu. Haihitaji argument yoyote hapa
 
Na watahiniwa hawaruhusiwi kutoka nusu saa kabla ya mtihani kuisha ili kuwepo na mashuhuda wa tukio la uhesabuji na ufungwaji wa mitihani kwenye zile bahasha, na pia mmoja wa watahiniwa aweze kutia sign kwamba amehahakisha idadi ya mitihani iko sawa, na imewekwa na kufungwa kwenye bahasha.
Hivi kama nitakamatwa na tumbo baya la kuhara baada ya nusu saa Je siruhusiwi kwenda chooni. .
 
Nadhani wasimamizi nao watatumia busara,kama kweli mtu umeshikwa kweli watakuruhusu tu uende.
Nakumbuka kipindi tunafanya mtihani wa form IV,kuna jamaa alikua anaumwa walimruhusu atoke nusu saa la mwisho
 
Sisi kina dada walikuwa anapandisha majini,alipiga pepa ya Civics baada ya sisi kutoka,maana toka pepa ianze mpaka inaisha yeye walikuwa kapandisha tu.majini mabaya sana Mshanajr
 
Kwaiyo majin yakafanyaje sasa hapo kwenye nusu saa ya mwisho ya mtihan na nusu saa ya mtihan kuanza
 
Na watahiniwa hawaruhusiwi kutoka nusu saa kabla ya mtihani kuisha ili kuwepo na mashuhuda wa tukio la uhesabuji na ufungwaji wa mitihani kwenye zile bahasha, na pia mmoja wa watahiniwa aweze kutia sign kwamba amehahakisha idadi ya mitihani iko sawa, na imewekwa na kufungwa kwenye bahasha.
mitihani gani ya hivyo?
 
mitihani gani ya hivyo?
Sina kumbukumbu nzuri kuhusu mtihani wa darasa la Saba,ila kuanzia mtihani wa form 2,form 4 na form 6 huo ndo utaratibu unaotumika
Mitihani hua inahesabiwa kabla ya kufungwa kwenye bahasha na mmoja wa watahiniwa lazima atie sign kwamba ameshuhudia mitihani ikihesabiwa na imetimia kulingana na idadi ya watahiniwa
 
Back
Top Bottom