Kwanini wasomi wengi ndo masikini duniani

  • Thread starter Tangi Tomofu kibiki
  • Start date

Tangi Tomofu kibiki

Tangi Tomofu kibiki

Senior Member
Joined
Mar 31, 2015
Messages
121
Likes
56
Points
45
Tangi Tomofu kibiki

Tangi Tomofu kibiki

Senior Member
Joined Mar 31, 2015
121 56 45
UNALETA USOMI MTAANI? UTAKUFA MASIKINI..!!

Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa. Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa.

Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi na magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!). Wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana.

Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga.

1⃣ Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli. Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio. Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa! Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika.

2⃣ Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani! Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha. Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

Sasa nisikilize:- Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninataka uelewe jambo hili: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani. Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti.

kibikiwoods@gmail.com
 
Zooxathellae

Zooxathellae

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Messages
326
Likes
273
Points
80
Zooxathellae

Zooxathellae

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2015
326 273 80
Subiri wasomi waje!
 
geofreyngaga

geofreyngaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2014
Messages
381
Likes
157
Points
60
geofreyngaga

geofreyngaga

JF-Expert Member
Joined Sep 7, 2014
381 157 60
wasomi wengi si masikini na wala si matajiri, ila wana maisha naweza kusema somehow stable.

Naamini tatizo ni (1)familia na mazingira tuliyotokea wengi wetu hayajiusishi na biashara so hatuna role model anaya tutamanisha kujiusisha na biashara.

(2).Shule na vyuo karibu vyote vinatufundisha tuje kuajiriwa tu na sio kufungua na kuendesha biashara zetu wenyewe. Nakumbuka wkt nipo chuo kimoja hapa tz, maprof, ma-Dr na walimu wengine wote wakiingia darasani kutufundisha mtazamo wao ulikua tusome tupate marks za juu ili tupate kazi nzuri na sio kujiajiri nilikua nachukia sana sbb malengo yangu yalikua kufanya issues zangu and forget about being employed.

(3).Vile vile wasomi wengi hawajiusishi na biashara sbb wanamachaguo(choices) kati ya kufanya biashara au kuajiriwa na mara nyingi hulka ya binadamu ni kupenda vitu rahisi kama kutakua na machaguo, hivyo wengi uona kuajiriwa ni njia rahisi na nyepesi kuliko kuanzisha biashara ambayo kimsingi zimezongwa na risks nyingi. Wkt mtu ambaye hajasoma hana machaguo mengi na yote ni magumu sbb akisema atafute ajira atapata lkn mishahara yao inajulikana kwahiyo ili kujikomboa kwa kipato hana choice yoyote zaidi ya kupambana kufa-kupona ktk biashara tu na sio kwengine.

(4)Lkn kibaya zaidi pamoja na mapungufu yote hapo juu, wasomi wamegoma kubadilika na kuendekeza kuajiriwa wkt jukumu la msomi wa chuo kikuu ni kutengeneza ajira kwa kuanzisha biashara na miradi mbalimbali ktk jamii yake but wasomi wetu imekua kinyume.

(5).Sera mbovu zinazodidimiza biashara zina wakatisha tamaa wasomi hasa ukichukulia kwamba anaweza kuchagua kati ya biashara au kuajiriwa. Mfano; ili uanzishe kiwanda hata kidogo tu utahitaji kuwatembelea wafuatao.

-BRELA
-Serikali ya mtaa
-manispaa kwa ajiri ya leseni
-TRA kwa ajili ya TIN na vitu vingine
-TFDA
-TBS
-OSHA
-NEMC
etc.

Hivyo vyote lazima uvipitie na uvipate ili ufanye biashara kwa amani, mbaya zaidi hivyo vyote vipo maeneo na ofisi tofauti tofauti.

Vile vile maofisa wa ofisi zote hapo juu hawana weledi wa kutosha, ni vigumu kwenda kwenye hizo ofisi ukapewa taarifa iliyo kamilika ni kama hawajui wanachokifanya.(writing from experience)
 
Mwanamayu

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Messages
8,385
Likes
2,448
Points
280
Mwanamayu

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined May 7, 2010
8,385 2,448 280
UNALETA USOMI MTAANI? UTAKUFA MASIKINI..!!

Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa. Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa.

Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi na magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!). Wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana.

Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga.

1⃣ Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli. Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio. Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa! Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika.

2⃣ Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani! Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha. Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

Sasa nisikilize:- Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninataka uelewe jambo hili: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani. Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti.

kibikiwoods@gmail.com
Kwanza ningependa kuelewa maana yako ya usomi. Halafu, ni usomi kwenye fani zote au baadhi? Halafu kwako wewe utajiri unaupima vipi? Na umaisikini unaupima vipi?

Je kwako wewe ukisikia 'information is power' na "knowledge is light" hauamini misemo hii?

Halafu mashuleni na vyuoni tunafundishwa kushirikiana kwani mara nyingi tunapewa group assignments, tunafanya group discussions. Pili mitihani inapima learning outcomes at individual level na sio group level.

Hivi hao matajiri wameajiri wafanyakazi wote ambao hawajasoma? Kodi wanalipa? Halafu wangekuwa wasomi hasa wale wa 'mabasi malori' (mabasi ambayo yanaundwa bongo, na kwenye ajali yanaua asilimia kubwa ya abiria) wasingeyafanyia biashara mabasi hayo.

Kwa kifupi, naona kama wewe upendi shule, au shule ilikupa shida sana!! Halafu hatuendi shule ili tuwe matajiri bali kuweza kuishi vizuri katika nyanja zote kuanzia afya, biashara, uchumi, kilimo katika ngazi zote - mtu mmoja mmoja, familia, mtaa, kijiji mpaka dunia nzima.
 
Z

Zamazamani

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2008
Messages
1,638
Likes
364
Points
180
Z

Zamazamani

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2008
1,638 364 180
maprofesa na madokta hasa wa chuo kikuu huishia kufanya baiashara ya kuuza kuku
 
Amoxlin

Amoxlin

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2016
Messages
3,617
Likes
3,675
Points
280
Amoxlin

Amoxlin

JF-Expert Member
Joined May 30, 2016
3,617 3,675 280
Ndg yangu akilibya darasani na akili ya maisha ni vitu viwili tofauti.
Ni wachache waliojaliwa vyote kwa pamoja ila wengi wao wamegawana kimojakimoja.
 
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
13,181
Likes
9,922
Points
280
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
13,181 9,922 280
Kwanza ningependa kuelewa maana yako ya usomi. Halafu, ni usomi kwenye fani zote au baadhi? Halafu kwako wewe utajiri unaupima vipi? Na umaisikini unaupima vipi?

Je kwako wewe ukisikia 'information is power' na "knowledge is light" hauamini misemo hii?

Halafu mashuleni na vyuoni tunafundishwa kushirikiana kwani mara nyingi tunapewa group assignments, tunafanya group discussions. Pili mitihani inapima learning outcomes at individual level na sio group level.

Hivi hao matajiri wameajiri wafanyakazi wote ambao hawajasoma? Kodi wanalipa? Halafu wangekuwa wasomi hasa wale wa 'mabasi malori' (mabasi ambayo yanaundwa bongo, na kwenye ajali yanaua asilimia kubwa ya abiria) wasingeyafanyia biashara mabasi hayo.

Kwa kifupi, naona kama wewe upendi shule, au shule ilikupa shida sana!! Halafu hatuendi shule ili tuwe matajiri bali kuweza kuishi vizuri katika nyanja zote kuanzia afya, biashara, uchumi, kilimo katika ngazi zote - mtu mmoja mmoja, familia, mtaa, kijiji mpaka dunia nzima.
Don't take it personal against him, amezungumzia mtazamo wake...ambao kwangu mimi naona yuko sahihi.

Ikiwa unaamini tunasoma ili tuishi vizuri, ina maana unaamini katika greatness.upload_2016-7-19_15-25-39-png.367616
upload_2016-7-19_15-25-18-png.367615
 
N

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2012
Messages
1,905
Likes
694
Points
280
N

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2012
1,905 694 280
Andiko lako haliko sahihi.
Mosi ungetupa tafsiri ya maskini. Pili ungetuonyesha kinagaubaga kwa kutupa takwimu sahihi za kidunia. Lakini kwa upande wa pili ungetuonyesha kinagaubaga takwimu za wasio soma kwa uwiano wa walio na mafanikio na wasio.

NB: Hata umasikini wa FIKRA ni umasikini.
 
Ngongo

Ngongo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2008
Messages
12,432
Likes
4,114
Points
280
Ngongo

Ngongo

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2008
12,432 4,114 280
Kusema maskini unawaonea kabisa.. Ungesema ni wa kiwango cha kati.. Hakuna msomi mwenye huo umasikini unaousema.
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro anawakilisha wasomi wengi sana.Wasomi ukiwaondoa makazini ni sawa na kutengeneza mstari wa umaskini wa kutopea.Usomi haujawasaidia kitu zaidi ya kufunga tai na umardadi tu.
 
K

kiliochangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Messages
1,161
Likes
837
Points
280
K

kiliochangu

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2012
1,161 837 280
UNALETA USOMI MTAANI? UTAKUFA MASIKINI..!!

Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa. Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa.

Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi na magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!). Wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana.

Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga.

1⃣ Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli. Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio. Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa! Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika.

2⃣ Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani! Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha. Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

Sasa nisikilize:- Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninataka uelewe jambo hili: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani. Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti.

kibikiwoods@gmail.com
Naona unajitahidi justify kushindwa kwako na kuandika mambo husiyoyaelewa. Wanaolalamika maisha magumu humu ni wasomi au? Kimbia shule uone mwisho wake. Mwl Nyerere mwenyewe alisema elimu ndio mwanzo wa maendeleao. Elimu pia ni Zaidi ya darasani kuna formal na informal education. Waweza kuwa na elimu na ukafanya yote. Maelezo marefu ila hautambui unajenga hoja gani hasa. Cases chache zilizoshindwa ku-achieve kwa sababu zao zisikufanye uka generalize maisha ya wasomi wote
 
totolito

totolito

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2016
Messages
607
Likes
357
Points
80
Age
48
totolito

totolito

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2016
607 357 80
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro anawakilisha wasomi wengi sana.Wasomi ukiwaondoa makazini ni sawa na kutengeneza mstari wa umaskini wa kutopea.Usomi haujawasaidia kitu zaidi ya kufunga tai na umardadi tu.
Alafu wasomi wengi wanaongozaa kwa ubishii
 
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Messages
44,923
Likes
12,875
Points
280
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2011
44,923 12,875 280
Wasomi wengi wapo kwenye middle income stage.
 
G'taxi

G'taxi

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Messages
3,386
Likes
2,801
Points
280
G'taxi

G'taxi

JF-Expert Member
Joined Sep 15, 2013
3,386 2,801 280
Kuna msomi m1 alikua ofcn kwetu na aliamua kulima vitunguu kijiji cha mbele kidogo na eneo tulipo,alipokua anaenda kuangalia watumishi wake shambani wanaendeleaje unaweza ukacheka mpaka ukazimia...kazi ya shamba au biashara haimtegemei mtu msomi wa madarasani maana ina namna zake. na usomi wake unategemea kupambana kwa bidii na kuizoea kazi,ndo mana unaweza kuta afisa kilimo anatoa training ya nguvu kwa watu juu ya mafanikio ya kilimo na yeye hana hata kitalu cha mchicha.ukweli ni kwamba msomi uliemmaanisha mtoa mada hua anawaza mshahara pekee na hua amebeba aibu ya kuchafuka,kuonekana hawezi kuuza maembe au ubuyu,yaani vitu vinavyoweza kumtajilisha mtu kifedha hua anavionea aibu kuvifanya,anapomuona mtu ana duka la spare za magari au ujenzi anataka na yeye aanzie hapo hapo bila kujua anaetaka kumuiga alianza kufanyia biashara kwenye meza pembezoni mwa barabara,na si kwa kukosa mtaji bali kwa kutaka kuizoea kazi.mtoa mada waache wasomi wavae mokasini na suti bana...
 
Mlaleo

Mlaleo

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Messages
10,554
Likes
4,017
Points
280
Mlaleo

Mlaleo

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2011
10,554 4,017 280
Unamaanisha Villaza ndio watu wenye Fwedha
 
Forum statistics

Threads 1,237,560
Members 475,562
Posts 29,293,587