Kwanini Wasanii wanaamini Live show bila kelele wala fujo haiwezekani?

Kwanini Wasanii wanaamini Live show bila kelele wala fujo haiwezekani?

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
1,152
Reaction score
1,696
Nimehudhuria baadhi ya matamasha na LIVE SHOWS za Wasanii wetu. Ila sikuwahi kufurahia tamasha hizo kutokana na kelele zisizo na mpangilio kutoka kwa wasanii wenyewe. Mara , Kushoto Kulia, mko wapi? mara Ruka juu!, mara mnataka niendelee au niwaachie? Yote haya yanaonekana kuwa ni sehemu ya onyesho lakini kwa mtazamo wa mtu anayelipia shilingi elfu 50 au zaidi hiyo siyo burudani bali ni kero.

Ni kweli kuna mashabiki wanaofurahia mihemko na nderemo hizo, lakini si kila mpenzi wa muziki anataka kurushwa kama mpira wa kona. Wapo ambao wanapenda kufurahia sauti safi, upigaji wa vyombo, mashairi yenye maana na utulivu wa kimuziki. Siyo lazima kila onyesho liwe kama uwanja wa mpira au ukumbi wa mazoezi ya Zumba.

Swali linakuja .Je, wasanii wetu wanaelewa tofauti ya SHOW na BURUDANI? Maana ya show siyo kupiga kelele tu jukwaani. Show nzuri ni ile inayosimuliwa na ubora wa muziki, mawasiliano ya moja kwa moja na mashabiki, utunzi wa maudhui na hata mionekano ya kisanii. Siyo kulazimisha mashabiki kuruka kila dakika tano.

Ni wakati sasa wasanii waelewe kuwa kuna kundi kubwa la mashabiki makini, wanaothamini sanaa yenye utulivu, usanii wa kina na burudani ya kipekee. Wakiwa wabunifu, wanaweza kutengeneza aina mbalimbali za shows zenye nishati kwa mashabiki wa nguvu na za utulivu kwa wale wanaopenda kufurahia muziki bila kelele za ziada.

Mwisho,

Wasanii tafadhali chukueni muda kujifunza hadhira yenu. Siyo kila mtu anapenda ENERGY ya kulazimishwa kucheza. Kuwa na vipengele tofauti vya burudani kutawasaidia kuvutia watu wa aina zote. La sivyo, mtapoteza kundi la mashabiki makini, wanaolipia ili wasikilize muziki, siyo kupigiwa kelele.

KONDE BOY, SIMBA LA MASIMBA DANGOTE, MARIOO ujumbe huu uwafikie nimemaliza.
 
Honestly mm siwezani na kelele, hivyo siend japo wengine wanafurahia sana.
 
Mwakajuzi, Mkesha wa mwaka mpya
Tulikua na Alikiba Pale Moshi.
Aise, Huwezi jutia kamwe
 
Utuache kiongozi wenzio tuenjoy

 
Back
Top Bottom