MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 19,415
- 40,260
Ninajitahidi kuelewa ila nimeshindwa kabisa kuelewa kwanini wapika keki wasajiliwe na BASATA. Kama sherehe ni matukio ya sanaa inabidi hata BURIAL CEREMONIES nako wahusike pia. Wasajili wapishi, wachimba kaburi, na waendesha ibada za maziko.
Kwangu mimi hii sheria ya BASATA kusajili hadi wapika keki ni ya kipumbavu zaidi kuwahi kutokea. Ikumbukwe hawa ma-DJ na wapika keki wengi wao wamesoma ila ajira ikawa ngumu ndo wakaamua kujitafuta kwa namna yao bila kuvunja sheria. Sasa mnakuja na sheria za kuwadhibiti badala ya kuwapa moyo kusonga mbele??!!!... mnavyowakatisha tamaa mnataka waende kuwa wahalifu?
Ninawasihi wabunge kufanyia marekebisho sheria hii ya kijinga ili kuzuia huu upuuzi wa BASATA unaoendelea.