Kwanini wanawake wengi wetu hatupendani?

Kwanini wanawake wengi wetu hatupendani?

Heloo

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
4,391
Reaction score
3,409
Za jioni.

Kuna msemo usemao adui wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe.
Kwanza tuchukulie mwanamke akiamua kugombea nafasi yoyote ya uongozi, Mfano Urais, Ubunge ama Udiwani sio siri sisi wanawake tutaanza kupiga vita mpaka anaweza acha, uombee sasa huyo mwanamke hajaolewa utasikia mtu mwenyewe hajaolewa atamuongoza nani? Hajazaa, mtu mwenyewe hajazaa atamuongoza nani, vitu vidogovidogo tunapingana.

Mfano mwingine. Mpo njiani wewe na mpenzi au na mume akapita mdada mrembo, au mzuri zaidi yako. Na mume akapiga chabo. Ooh oooh! Ujue wewe naba utanuniwa njia nzima au siku nzima (ila mimi heloo, nikiwa na mpenzi wangu tukapishana na kifaa huwa natoka credits 'mmh msichana au dada bombs huyu sina kinyongo why nisimpe sifa mwanamke mwenzangu mwenye sifa zake?) Kweli huwa natoa sifa.

OK. Tukija Salon hasa za like, mpo wanawake wengi wanaosuka wanaopaka rangi wanaosafisha miguu, uso na mengi mengi, anaongea mnacheka. Akiondoka mmoja kamaliza alichojia huku nyuma wanaanza kumteta huyu aliyeondoka sasa (kuna siku hiyo salon moja nilishangaa sana kila anayeondoka anasimangwa 'hana lolote naye huyu anajifanya ana nywele nzuri sijui pesa wenye pesa wanakuwa hivi? (Kiutani ilibidi niwaombe jamani mimi nikitoka.

Naomba msinitete) waliishia kucheka but sio tabia njema. Mfano mwingine. Inatokea msichana A kampigia simu msichana B. Pengine amemkumbuka na anapenda sana weekend hii amtembelee ashinde huko na wapike wale pamoja, hapo anaongea kwa simu. Akikata tu huyu B ambaye alikuwa anaitikia na kucheka kwanza anaweza sonya na kusema tutaona kama atanikuta 'eti aje kushinda hapa mjinga nini nitaondoka akome.

Kinyume sana kwa wenzetu wa kiume kwa story hiyo juu angefurahi hata haada ya simu na kuhusu jamaa yake amemkumbuka na atahakikisha anamsubilia.
Umbea nao ni dalili ya kutokupendana. Sawa umbeya sio jambo njema hata kidogo lakini kuna wakati watu au palipo na wengi pana neno.

Sasa unafuatwa unasimuliwa jambo Na mwenzio anakusihi sana usiseme Na unaapa kwamba hutasema. Akiondoka tu unatafuta simu ipo wapi na unaongezea na chunvi. Mwanzo wa chuki miongoni mwa sisi wanawake.

Mwenzio ana familia nzuri bora badala uige unaanza kutoa kasoro zote, umehudhuria sherehe ya best ako unaanza kukosoa ukumbi, chakula Mara Nguo rangi sio nzuri lakini wakati yupo ulisifia sana (unafiki)

Jamani wanawake wenzangu kifanyike kitu gani kupunguza chuki hizi ili jamii yetu iwe bora? Maana haya mambo ndo huzaa chuki na watu kuchukiana.

Akhsante.
 
ngoja nisubirie majibu yao hata mimi nilikuwa ninahamu sana ya kujia kwanini jinsia yenu hampendani ?
 
dada yangu nilikuwa namshangaa akiongea na wenzake utaskia, 'kichuna, mpenzi, sissy na maneno yote mazuri' akikata simu utaskia msonyooo. Kinachofuata ni matusi mwanzo mwisho huyu changud.a alikuwa ananitaka nini?

kipindi flani nimepanga nilikuwa nashangaa naombwa sufuria, kinu, ungo wakati kulikuwa na wanawake wengine?

ila wanawake mna matatizo nishatembeaga na wanawake wawili kisa walikuwa wanaugomvi
 
Nikweli, wanawake hatupendani, na kinacho Fanya tusipendane ni kila mmoja anajiona bora, mzuri yeye, kasoma yeye, pesa anazo yeye, kuvaa anajua yeye, mabwana mahandsome wote anayo yy, ndiyo chanzo cha sisi kutopendana tuna wivu wakijinga usio na maana
 
Well said Jovitha, wewe je, hayo mambo unajionaje?! unahisi uko hivyo!!
ntarudi baadaye...
 
Well said Jovitha, wewe je, hayo mambo unajionaje?! unahisi uko hivyo!!
ntarudi baadaye...
Hapana sipo hivyo hata kidogo nahisi Nina roho ya kipekee, coz sijui kuringa, sina nyodo, majigambo, nipo kawaida mnoo nainapotokea mwanamke mwenzangu kafanya jambo zuri nasikia amani mnoo kumpongezaaa,... Hivyo ndiyo jilivyo

Lakini sina rafiki wa kike hata mmoja wala wakiume, mda mwingi napenda kuwa peke yangu, kuepusha mambo yasiyo na ulazima
 
Wewe kama huwapendi wenzio ndo useme kwa nini. Mimi binafsi sinaga hizo aisee mtu yeyote ambae yuko vizuri either kwa nguvu zake au kwa kubarikiwa tu na muumba huwa sisiti kumpa credit zake. Ila huwa sitoi sifa za unafiki na sinaga tabia ya kujipendekeza...siwezi kumsifia mtu eti kwa sababu kila mtu anamsifia. Ni kweli umependeza lakini kupendeza ni subjective waweza kuwa machoni pangu hujapendeza nikusifie uongo? Hapo ndo watu huanza kusema wanawake hatupendani...mimi wanawake wenzangu nawapenda sana hasa wale wasio wambea-wambea na wasio na unafiki.
 
Hapana sipo hivyo hata kidogo nahisi Nina roho ya kipekee, coz sijui kuringa, sina nyodo, majigambo, nipo kawaida mnoo nainapotokea mwanamke mwenzangu kafanya jambo zuri nasikia amani mnoo kumpongezaaa,... Hivyo ndiyo jilivyo

Lakini sina rafiki wa kike hata mmoja wala wakiume, mda mwingi napenda kuwa peke yangu, kuepusha mambo yasiyo na ulazima
Yaleyale. Hapa wewe unajiona ni bora kuliko wenzio....ifahamike kuwa kila binadamu ana tabia yake kama mtu ana maringo, kiburi majigambo hiyo ni tabia yake atakuwa hivyo hata kwa wanaume.
 
Wanawake mko juu sana...mnaweka kasoro mpaka kwenye msosi
 
Hapana sipo hivyo hata kidogo nahisi Nina roho ya kipekee, coz sijui kuringa, sina nyodo, majigambo, nipo kawaida mnoo nainapotokea mwanamke mwenzangu kafanya jambo zuri nasikia amani mnoo kumpongezaaa,... Hivyo ndiyo jilivyo

Lakini sina rafiki wa kike hata mmoja wala wakiume, mda mwingi napenda kuwa peke yangu, kuepusha mambo yasiyo na ulazima
izo kiki tu wanawake wote mwalimu wao kipofu unaweza kuonge maneno kwa nje lakini atujui moyoni pakoje
 
Back
Top Bottom