Kwanini wanawake wengi wanapenda kuolewa na wanaume wenye degree+?

Markomx

JF-Expert Member
Apr 23, 2016
701
701
Ukipitia post nyingi za wadada hata kwenye vipindi vya redio wadada wanaotafuta wanaume kigezo chao kikuu ni mwanaume awe kasoma kuanzia ngaz ya degree nakuendelea.

Napenda kuuliza hivi hizo degree zina issue sikuizi?

Mbona hao wenye degree tunachoma nao mahindi mtaani sikuhizi na kufanya nao kazi za mtaani za kawaida kama kuuza mkaa,kulima matango ,kuzibua vyoo,kuuza ndara ,kubeba zege sawa na sisi tulioishia la Pili B.

Wadada degree sikuizi sio issue sana.Maana kila nyumba sikuizi inagraduate wa degree nk.Natunapiga nao kazi za kubeba zege kama sisi .

Hichi kigezo cha degree kinawasaidia nini wadada

Nashindwa kuelewa

nawasilisha
 
Iko hivi.

●Mtu mwenye degree ana probability kubwa ya kutusua maisha kutokana na uwezo wa kusoma mazingira aliyopo, uwezo wa kudadisi na kufahamu fursa, exposure, flexibility ya fikra na mawazo nk. Hivyo mwanamke anaamini mtu mwenyw degree ataweza kuyamudu maisha kwa wepesi kuliko std 7.

●Mtu mwenye degree ana level fulani ya civilisation, yani kustaarabika. Mwanamke Anaamini ni rahisi mtu mwenye jiwe kuwa open minded kuliko darasa la 7. Mtu mwenye degree hataona ajabu kumruhusu mkewe kumiliki biashara nk, tofauti na darasa la 7 ambae atahisi anaeza zidiwa kipato hivyo hatompa mkewe uhuru nk...

●Mtu mwenye degree anakua na network fulani... hata kama yeye bado hajatusua lkn mwanamke anaBet kua huyo mtu anaeza kua na marafiki kwenye circle yake ambao wanaweza kutoa misaada ya kueleweka kipindi kigumu, tofauti na darasa la 7 ambae utakuta marafiki zake ni mafundi wa kuchomelea vyuma, kuuza korosho nk.

All in all mapenzi hayaangalii umri, Dini, elimu, kipato nk... lakini lkn mtu anaetafuta maisha lazima aangalie hivyo vitu, sasa unapoingia kwenye ndoa unatafuta mapenzi na maisha at the same time, so vitu kama elimu, dini, kipato vinamatter sn, kwasababu ndoa si kitu cha kuingia na kutoka, ni life long thingy.

Usitafute kisingizio kua kwasababu unabeba zege na wenye degree basi degree ni takataka... mtu unaebeba nae zege leo atakuacha ghafla unashangaa unakuja kubeba zege kwenye nyumba yake. So bro rudi shule mzee upate hiyo kitu.
 
Back
Top Bottom