Kwanini wanawake wanawafanya wanaume wao zezeta? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini wanawake wanawafanya wanaume wao zezeta?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by God bell, May 14, 2011.

 1. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 581
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Hodi wanaJF mimi ni mgeni humu jukwaani nikiwakwaza mnisamehe. Mada yangu ni kwamba wanawake wengi sana ndo huwa wanawafanya waume zao mazezeta kwa kuwaendea kwa waganga ili waweze kuwapooza wapate nafasi ya kufanya mambo yao wanayotaka wenyewe.Nimetoa hii mada maksudi kwa sababu: Nina rafiki yangu nafanya nae kazi na pia tunaishi mtaa mmoja alipata matatizo km haya. Mke alikuwa anatoka nje ya ndoa jamaa akamfumania live ukawa ugomvi mkubwa sana na jamaa akawatangazia ndugu wa mke na mjirani kila kitu jinsi alivyomfumania na hamtaki tena wa kwanza akiwa mimi kuambiwa. Wakiwa kwenye ugomvi ndani ya cku 2 mke akaondoka asubuh akaenda kuckojulikana. Aliporudi kesho yake akamkuta mzee nyumban yuko kama mbogo aliyefukuzwa na simba, akampikia chakula. Mzee alipokula tu hasira zote zikaisha akasahau kila kitu. Cha kushangaza ni kwamba mke ndo amekolea kutembea nje ya ndo na si mwanaume mmoja. Na sasa hv jamaa anajua kila kitu lakini amepoa kama maji kwene mtungi. Kuna cku alipigiwa cm kuhusu mke wake akajibu 'nyie ndo mnanigombanisha na mke wangu' na jamaa ninavyomuona yuko km amechanganyikiwa. Jamani huyu jamaa c ameshafanywa zezeta tayari? Kwani hata shuguli za mendeleo amesitisha na mke nde mwenye kupokea hela na kujivinjari na mabwana zake wa nje.
   
 2. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nawachukia sana wanawake wanaowafanya wanaume wao mazezeta, kama hamtaki bora aende zake, unamfanya mumeo zezeta afu bdo unaish nae c ujinga huo?
   
 3. B

  Bendera ya bati Senior Member

  #3
  May 14, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tamaa zisizokuwa na msingi ndizo hasa huwaingia baadhi ya wanawake wa namna hiyo ili kuwafanyia mambo maovu kama hayo waume zao.Hii ipo sana katika jamii yetu.
   
 4. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  sina mengi zaidi ya kusema siipendi kabisa tabia hiyo mbaya inayofanywa na baadhi ya akina mama.
  mapenzi mazuri yenye raha na amani ni yale anayoyatoa mtu kwa moyo wake bila shinikizo lolote
  otherwise ni ubatili mtupu!
   
 5. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  watu wanashindwa kuelewa kuwa limbwata ni mwanamke mwenyewe!!!

  ukishajua swty wako anapenda nini, na hapendi nini kwanini usimdatishe mpk ukamlishe mikafara???

  Kutokumjua Mungu nako kunachangia zaidi haya mambo!! lkn kama unahofu ya Mungu tu ukitaka kwenda kwa mganga unasikia sauti inakwambia "Bwana asema hivi, amelaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake na moyoni mwake amemwacha Bwana"
   
 6. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #6
  May 14, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Hivi hizi dawa zipo na za kweli? au tu lijamaa limekolea? nafikiri ukiwa na imani nayo ndio yanakupata. Hao waganga wenyewe mbona waongo tu. Na kama wapo kwa nini msimpeleke huyo jamaa akatibiwe?
   
 7. wilbald

  wilbald JF-Expert Member

  #7
  May 14, 2011
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 1,239
  Likes Received: 626
  Trophy Points: 280
  GAGA kuna mshkaji wangu alishafanyiwa hivyo na demu wake ila baada ya muda jamaa alishtukia mchezo akamtema.
  Wapo na niwajanja mno.
  Yani jamaa aliponea tundu la sindano kwani huyo demu alitaka amuue kabisa.
   
 8. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #8
  May 14, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Duh! sijui kwa nini siamini kama kuna dawa za mapenzi, najua shetani yupo na anakazania kazi zake pia nahisi kama ukiamini ndio yanakupata au ni aje? na kama wapo wa hivo wawafanyie dawa na wao watulie basi, sasa unamfanyia dawa mtu awe zezeta kwako halafu wewe unatafuta mwengine tena? yaani hata nashindwa kuelewa
   
 9. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #9
  May 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  sred klosed:
  hakuna limbwata wala mchumbaake limbwata, hilo lijamaa linaientertain huo uzembe halaf linaleta habar za limbwata. hiyo kitu ni myth imewekwa kuwaprotect wanaume wazembe tu. Ukiangalia background za wanaume wote tunaoambiwa wamewekewa limbwata utagundua tayari ni weak tangu primary school.
   
 10. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #10
  May 14, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Susy una jicho tamu wewe.....
   
 11. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #11
  May 14, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  klorokwini umekosea, ni ma weak toka Kindergaten mzee, mie nalijua moja wala hamna LIMBWATA ila jamaa ni LAME hadi nguo zake za ndani....
   
 12. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #12
  May 14, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Wanawake wanateseka sana hasa kwenye mahusiano, kama kuna mjanja anajua hayo ya kumfanya zezeta mwanaume mmoja mwache alipize kwa ajili ya wanawake wote wanaonyanyaswa na kuchitiwa na wanaume wao,na waeleze hapa kuna dawa ya mapenzi? hakuna kwa hiyo huyo jamaa kawaka mwenyewe tu kwa huyo mkewe
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  May 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Huihitaji mganga kumtuliza mwanaume wako wala huhitaji nyumba ndogo kumuondoa nyumbani!!Matendo yako mwanamke ndo yanaweza either kumuweka sawa au kumhangaisha!!!

  Na hata kama kweli hilo limbwata lipo...utapata raha yani kujua hayupo pale kwasababu anakupenda ila ni kwasababu umekorofisha akili yake???Ile raha ya kupendwa inaondoka kabisa ila nadhani wanaohangaika na haya mambo ni wale wasiojiamini na wanaopenda kukontrol watu wengine ila hawawezi!
   
 14. A

  Aisha Adam JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nafikiri 2muogope mungu na tuwe tunajiuliza 2tajibu nini mbele za haki, mi binafsi hiyo tabia siipendi jamani wanawake wenzangu mnaofanya hivyo muache, kumfanya mtoto wawatu zezeta bora uondoke zako ukiona anakukera.
  Lkn na wanaume muache kuwanyanyasa wake zenu make kuna wanaume mapenzi anakuonyesha wakati wa uchumba akishakuoa anageuka mbogo hata hataki kukusikiliza ye anachojua nikukukaripia, jamani wanaume acheni hizo tabia na zenyewe zinachangia katika hilo.
   
 15. A

  Aisha Adam JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna baadhi ya wanaume wanakuwa na mapenzi kwa wake zao wakati wa uchumba wakishafunga ndoa wanageuka kuwa mbogo ndani ya nyumba hawataki wanawake zao wawaulize lolote na hawataki kuwasikiliza na hiyo inachangia sana.
  Lkn na sisi wanawake 2we 2najiuliza 2tajibu nini mbele za haki kumfanya mtoto wa mwanamke mwenzio zezeta. Tafadhari ukiona yamekushinda ondoka kuliko kumfanya mwenzako zezeta na kwa hli naomba 2muogope mungu sio vzr na wewe jiulize angukuwa kaka yako ungefanyaje?
   
 16. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #16
  May 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Mie dume langu sijaliendea kwa mganga, huwa nalikuna panapotakiwa, halioni halisikii. Tena linaona raha nikiliita "my msukule".
   
 17. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #17
  May 15, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  FaizaFoxy bwana! yaani ukimkuna mwanaume wako vilivyo ndio umwite your msukule? sidhani kama ni jina zuri
   
 18. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #18
  May 15, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kufanywa zezeta kwa faida ya familia ni nzuri na inafaa sana maana wanaume wengine bila hivyo mshahara haufiki home.
   
 19. s

  shosti JF-Expert Member

  #19
  May 15, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  mhh huwa linaisha baada ya muda fulani.....hahahaha wanawake wengine machachari sana ndo nini sasa
   
Loading...