My dear pretty God never said man should do everything, alisema Adam for this sin "the ground will be under your curse. You will have to work hard all your life to produce enough food for you.Na mungu alipoomuumba Eve aliosema nitampa msaidizi (si tegemezi wa kila kitu)
Na tunaona ktk maandiko hayo hayo kwenye proverbs kuna chapter nzima ya capable wife Prov 31:10-31 ntakunukulia few lines
How hard is it to find A capable wife, she is far worth than money.....she keeps herself busy making wool and linen cloth......she is a hardworker,strong and industrous....she is always busy and looks at her family's needs.
Tukirudi kwenye mada nakataa kabisa kuwa Mungu alimuumba mwanamke awe tegemezi, apewe kila kitu bila yeye kuchangia.
Ni jamii zetu na makuzi ndio yametulea kutazama kuwa mwanaume ataprovide kila kitu. Tumekuzwa kuona baba ananunua kila kitu.. kwa kuwa mama alikuwa housewife. Binti aliyeondoka nyumbani na mtazamo huu hata afanikiwe na maisha apate kipato kizuri na mpenzi/mume bado atakuwa na fikra " jamaa atanipa pesa kudhihirisha ananipenda" na hata wakioana ataendeleza fikra hizo, yeye chake ataficha cha mumewe cha wote.
Lakini tungejiuliza, mapenzi ni nini haswa? nafikiri ni kurudhiana kuwa pamoja, kusaidiana, kushirikiana na kutulizana. Sio one way trafik- bali wote msichana na mvulana kila mmoja aonyeshe mapenzi kama kusaidiana wewe ukipew zawadi na wewe toa. Kama unatolewa out na wewe at times umtoe mwenzio out. Nafikiri kwa mwanaume timamu akiona binti yuko responsible na independent atampenda zaidi na kumheshimu.
Kuna mazingira ndio tunakubali kuwa msichana hana labda jamaa anafanya kazi na binti ni mwanafunzi basi kwa kile kidogo cha jamaa anaweza kusaidia mpenzi wake, na binti hapa asiwe ng'ang'anizi ati kila wakati apewe tuuu pesa kisa shoga yake ana kibuzi kinampa laki kila wiki!!!!
Kina dada wana tabia ya kujicompare na wenzao sana , kama ni vyuoni basi watashindana boyfriend wa nani ni bingwa wa kutoa pesa, wakiwa vyumbani husimuliana ohh jana nimepewa Simu kali na pesa, basi wenzie watamwambia eeh anaonyesha anakupendaa ehhh, sasa wale wengine (bila kufikiria other factors za wapenzi wao) huanza kujenga hisia kuwa ahaaa kumbeee kupendwa ndio huku... ni kupewa pesa, zawadi n.k na yeye akikutana na BF wake ataanza kudadisi eti unanipenda, mbona hunipi pesa; Namwambia hisia na fikra hizi zikisha jengeka kwenye akili ya binti basi ndio mwanzo wa balaa. Hata akipata kazi bado atataka apewe kila kitu na hatachangia hata chembe kwenye familia.
Ni wakati muafaka kina dada wakatambua kuwa mapinduzi ya kweli wanayoyahitaji ni pamoja na kujiamini kuwa wanaweza na kwenye mahusiano pia wanachangia na kwenye familia vile vile wanachangia. Ila kutegema kupewa tuuuu mwishowe ni kunyanyaswa na kudhalilishwa.