Kwanini wanawake wanapenda kupewa fedha na wanaume?

mie naona hili swala la mwanaume kutoa pesa kwa mwanamke ni wajibu wa mwanaume. Hata kama mkeo au gf ana kipato chake lkn ww mwanaume lazima utoe pesa kwa mkeo. Kumbuka pesa ya mwanaume ni kwa familia yote na pesa ya mwanamke ni ya kwake mwenyewe. Hivyo kama mwanamke akiwa na utu tu ule wa kumpenda mwenzio ndio anaweza kumpa pesa mwanaume wake, au kama mume hana kazi au mgonjwa hapo mwanamke pia anweza kumsaidia mwanaume hivyo ni hiyari ya huyo mwanamke. Lkn mwanaume lazima atoe pesa kwa mwanamke iwapo anazo, haijarishi kama mke ana kazi au lah!
umenena my dear, mwanamme kumpa pesa mwanamke ni wajibu ila kwa sababu ya umasikini wao ndo maana kila siku wanalalamika, mbona wanawake hawalalamiki kwani ni vingapi wanawapa lakini hatulalamiki,. kutwa kucha ni nyie tu, kila siku unachimba Dhahabu kwenye mgodi wa mwenzio halafu ukiombwa pesa unaanza kulalamika! siku unamtaka unamwambia ninakupenda nitakutunza kwa lipi? unaona mwanamke kapendeza eti unatamani ummiliki unafikiri kumiliki mwanamke mrembo ni kazi ndogo? wapo ambao ili mradi kumekucha sh. 500 kwa siku inamtosha maana hajui hata kupaka lotion kutwa nzima ananuka kikwapa, watafuteni hao wanawafaa wanaume wote msiopenda kuwapa pesa wanawake, wanawake wazuri na warembo waachieni wakubwa wafaidi, nyie sio size yenu. na kama mnaona wanawake wanapenda hela basi tongoza wanaume wao hawapendi hela achana na wanawake
 
Sidhani kuna popote imewekwa kuwa mwanamke lazima apewe pesa na mwanaume.Nadhani ni kutokana na unequal power relations ambapo mwanaume anatarajiwa na jamii kuwa juu ya kila kitu na mwanamke kuwa chini ya mamlaka ya mwanaume ndipo tunaona mwelekeo huu.

Na kama tutarudi nyuma katika historia ya maisha yetu miaka ya nyuma ilikuwa ni kama desturi kama si kawaida kwa mwanaume kumiliki mali na kila njia ya uchumi kiasi kuwa ilitarajiwa na kuaminika kuwa mwanamke hana kitu japo alikuwa na mahitaji.Hapo ndipo mwanaume alionyesha uanaume wake kwa kutoa si pesa tu bali hata vitu vingine ikiwa na pamoja na ofa za hapa na pale.

Maendeleo na mchanganyiko wa jamii umebadilisha mambo kwa kiasi japo si sana na ndiyo maana hata sasa kuna wanawake wanawapa wanaume ( waume au wapenzi au marafiki zao) pesa na vitu vingine.

Hii ni kwa kifupi sana ukitaka zaidi utapata kadiri mada itakavyochangiwa.
Umesema kweli, ila hali itabadilika kwani tunaona kwenye nchi zilizoendelea za ulaya na marekani wanawake hawako hivyo tena hasa wenye elimu na kipato, huchukulia mwanaume kama Mtu tu anayehitaji kupendwa na sio chanzo cha kipato. Hata sisi huku Africa ipo siku watafikia uwelewa huo
 
umenena my dear, mwanamme kumpa pesa mwanamke ni wajibu ila kwa sababu ya umasikini wao ndo maana kila siku wanalalamika, mbona wanawake hawalalamiki kwani ni vingapi wanawapa lakini hatulalamiki,. kutwa kucha ni nyie tu, kila siku unachimba Dhahabu kwenye mgodi wa mwenzio halafu ukiombwa pesa unaanza kulalamika! siku unamtaka unamwambia ninakupenda nitakutunza kwa lipi? unaona mwanamke kapendeza eti unatamani ummiliki unafikiri kumiliki mwanamke mrembo ni kazi ndogo? wapo ambao ili mradi kumekucha sh. 500 kwa siku inamtosha maana hajui hata kupaka lotion kutwa nzima ananuka kikwapa, watafuteni hao wanawafaa wanaume wote msiopenda kuwapa pesa wanawake, wanawake wazuri na warembo waachieni wakubwa wafaidi, nyie sio size yenu. na kama mnaona wanawake wanapenda hela basi tongoza wanaume wao hawapendi hela achana na wanawake[/QUOTE Mwanamke mwenye mawazo kama ya kwako haya, kuendelea ni vigumu sana, kumueka mwanaume kama chanzo cha kipato hakika mfumo dume hautaisha. Mwanamke mwenye akiri hushilikiana na mume wake na kujenga maisha. Sio kuficha kuficha pesa zake nakutegemea kupewa kila kitu na mwanaume, kwanza huko nisawa na kujiuza.
 
mie bwana pesa yangu ni yangu tu! wanaume hawatabiriki kabisa, wakati fulani nilikuwa nasaidiana na mr bega kwa bega, kila mwisho wa mwezi 2takaa 2pange mambo ya kimaisha na matumizi ya kifedha, alipokuja kubadilika kidogo nikaona na matumizi ya nyumbani yamepungua sana, hapo ni mie sasa na kila kitu ndani, alipokuja kujirudi alishanipa lesson, nilisema sasa changu ni changu chake kitakuwa chetu kufidia huyo wa nje alivyokuwa anavinjari, na yeye hakudhubutu tena kuniambia mambo ya kukaa chini na kupanga kwa pesa yetu bali tutapanga kwa pesa yake, waiiiiii
Usifanye hivyo kama umesamehe usilipize kisasi, kumbuka wote mnatafutia familia moja. Hayo mambo yako ni yapi?, nawakati yote ni yafamilia moja hata ukijenga nyumba mwenye kisheria inajulikana ni yenu wote. Huyo amekosea kama mwanadamu, lakini sio kwasababu ni mwanaume.
 
mie naona hili swala la mwanaume kutoa pesa kwa mwanamke ni wajibu wa mwanaume. Hata kama mkeo au gf ana kipato chake lkn ww mwanaume lazima utoe pesa kwa mkeo. Kumbuka pesa ya mwanaume ni kwa familia yote na pesa ya mwanamke ni ya kwake mwenyewe. Hivyo kama mwanamke akiwa na utu tu ule wa kumpenda mwenzio ndio anaweza kumpa pesa mwanaume wake, au kama mume hana kazi au mgonjwa hapo mwanamke pia anweza kumsaidia mwanaume hivyo ni hiyari ya huyo mwanamke. Lkn mwanaume lazima atoe pesa kwa mwanamke iwapo anazo, haijarishi kama mke ana kazi au lah!
Mod tuwekeeni na UNLIKE.
 
Nadhani utofauti wetu kati ya wanawake na wanume ni functional in order to maintain species sema watu wa gender saa ingine wanaharibu na kuyakuza mno!

Angalia madem walivyo warembo na wanavyopendeza ili madume wawatamani! Angalia madume walivyo na misuli na nguvu ili wanawake wawazimikie!

Yaani haya mambo ya kinadharia siku hizi na gender kama Scandnavia countries maskini wanaume wamenywea na wamekaliwa hata utawaonea huruma!

Hakuna raha bwana mwanamme ukoao mke wako ..ukamtunza pia ukatoa na pesa kwa familia yako! nakuambia basi hii ni heshima kubwa sana kwa akina baba hata kama mama ana pesa kiasi gani! Mama anaweza kukujibu kwa kujisikia kuwa nae ameolewa na yeye kama mwanamke anapendwa!
Mwanamke atakuheshimu tu hata kama mtasaidiana maisha, heshima hailetwi na wewe kutoa pesa. Kwa hiyo siku ukikosa hizo pesa hatakuheshimu? Mimi nawashauri wanaume usikubali kupendwa na kuheshimiwa kwasababu unatoa pesa utakuwa uko kwenye penzi la uwongo
 
Mwanamke atakuheshimu tu hata kama mtasaidiana maisha, heshima hailetwi na wewe kutoa pesa. Kwa hiyo siku ukikosa hizo pesa hatakuheshimu? Mimi nawashauri wanaume usikubali kupendwa na kuheshimiwa kwasababu unatoa pesa utakuwa uko kwenye penzi la uwongo
madume watabaki kuwa madume na majike watabaki kuwa majike!

Mungu ameumba tofauti!

Heshima ndo hiyo ya kujua tuko tofauti!
 
Kumbuka pesa ya mwanaume ni kwa familia yote.na ya mwanamke ni ya kwake mwenyewe. NIMEIPENDA
 
Imekuwa ni kawaida wanaume kuwapa wanawake fedha aidha kwa kuwa ni marafiki au wachumba au wanandoa.Mwanamke katika ndoa hupenda kutumia fedha zake kwa mambo binafsi na mambo kama hayo.Je kama wanawake hawatabadilika si ni ngumu katika harakati za mapinduzi ya mambo ya jinsia?
"sasa wewe ulitaka wawaombe akina nani? mwanamke ni kiumbe tegemezi kuanzia kihisia hadi maumbile.. ni jukumu lao kuomba lakin wengi wao wanatumia fursa hii vibaya"
 
Back
Top Bottom