Kwanini wanawake wanaamini wanaume ndio watakaonza kufa?

Akili yao huwa unawaza vya bure. Ss Ole wako ukishamaliza kukusanya mali uchelewe kufa
 
Upo sahihi kabisa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni kweli.
Ukitaka kuamini mwambie nataka kuuza hii Nyumba..

Utaskia "ukifa me na watoto tutakaa wapi "??

Wanawake MUNGU anawaona
 
Sawa mke akitangulia kufa, lakini wewe humalizi hata miaka mitano, ujiulizi kwanini wagane ni wachache kuliko wajane, kwa sababu wengi hufa kwa stress ingawa atajipoza lakini wapi.

Miaka karibia 10 toka Baba afariki, Mama yupo tu anadunda
 
Ni kweli kabisa ndio maana wajane ni wengi kuliko wagane
Jr[emoji769]
 
Sababu mojawapo ni life style.Mwanaume anaacha pesa ya kununua nyama mara mbili kwa wiki.Nyama ambayo mke na watoto wanakula finyango tatu kula mmoja.Siku 5 kati ya saba kwa wiki familia wanakula maharage,dagaa na mboga za majani.Baba yeye akienda kazini breakfast ni chai ya maziwa,supu ya ng'ombe Na chapati.Lunch Ugali nyama au ndizi nyama au wali nyama ya ng'ombe.Akitoka kazini anapitia mahali ili kuongea na marafiki wanaagiza bia,nyama choma ya mbuzi na ndizi choma.Akirudi nyumbani anakula tonge mbili za ugali ili mama Manka asishtuke kama kala mahali.Hivi kwa mtindo huo wa maisha nani atatangulia kufa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ahahahah akili zao ni copy. Original ni Eve
 
ngoja tuwazalishe kwasaaana,ili tukifa tuwaachie majukumu ya kulea watoto na majina yetu yasisahaulike,
muone huyu mtooto alivyofanana na marehemu baba yake
 
[emoji16][emoji16] ni kweli wanaume ndio wako kwenye hatari ya kufa kulingana na mazingira yao ya utafutaji. Sababu nyingine ni kwamba wanaume wengi si watu wa kujali sana afya zao ukilinganisha na wanawake
Hayo yote sio ya msingi ila sababu ya msingi ya mtu kusema hivyo ni mfumo wa jamii zetu, siku zote mwanamke huwa hana chake kwa hiyo ikitokea mumewe amekufa kama ameolewa jamii ya watu wasiostaarabika cha moto lazima akione tofauti na upande wa mwanaume....umeshawahi kuona mgane ananyanyaswa na ndugu wa mke? Akitangulia kufa mke hapatakuwa na shida yoyote ishu inakuja akitangulia mume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…