Kwanini wanawake wakiolewa huvunja urafiki na marafiki?

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,463
Kama huamini basi kaa kimya,ila huu ni ukweli ulio wazi kabisa.

Unakuta msichana alikuwa ni rafiki yako mkubwa ambaye mnaishi kama kaka na dada na mnasaidiana kwenye shida na raha.Ila akishaolewa tu basi na urafiki unaishia hapo,hata simu ukipiga hapokei wala sms hajibu as if kabla ya kuolewa hakuwa na watu anaojuana nao kwanini inakuwa hivi?

NB: Simu hapigiwi usiku wala asubuhi sana,maana ni mke wa mtu.
 
Si mke wa mtu?, sasa na wewe unampigia mke wa mtu usiku unataka nini kama sio kutaka kumuharibia ndoa yake?, unadhani mumewe ataelewa kama wewe ni rafiki yake?, hata wewe ukiwa na mkeo hutokubali ndio maana wanavunja urafiki coz imani inakuwa ndogo kwa mwenza wake
 
Muache atulie kwanza na ndoa, urafiki utarudi baadae halina shaka, mpe nafasi!
 
Moja ya topic kwenye mafunzo kabla ya ndoa inasemaga ''Anza kuchagua marafiki wale waliopo serious, unapoingia kwenye ndoa marafiki wale wasiokuwa na maana na wewe achana nao''...So ukiona hivyo ujue wewe uko kwenye kundi la marafiki wasiokuwa na maana...maana si wote anawachunia ila kuna baadhi tu kama mafundisho ya ndoa yasemavyo..Kuchagua marafiki wale wa maana...
 
Si mke wa mtu?, sasa na wewe unampigia mke wa mtu usiku unataka nini kama sio kutaka kumuharibia ndoa yake?, unadhani mumewe ataelewa kama wewe ni rafiki yake?, hata wewe ukiwa na mkeo hutokubali ndio maana wanavunja urafiki coz imani inakuwa ndogo kwa mwenza wake
Acha papara,soma thread upya
 
Muache aende mkuu na ndoa yake.

Nadhani akishaolewa anakuwa tofauti na majukumu yanaongezeka zaidi akiwa single, hapa anakua anaishi kwa kushirikiana na mwenzake
 
Hata wanaume wakioa pia hupunguza ushirikiano na marafiki. Ukiona mtu anaoa/anaolewa lakini bado anang'ang'ania marafiki zake wa zamani, basi ujue huyo kwenye ndoa yake kuna mgogoro unaofukuta.
 
mtu akishakua mke wa watu bwana inakua ngumu kupatikana
kwasababu anakua chini ya mume wake..
analolitaka mume ndo analolifanya..
na ndege wafananao ndio huruka mti mmoja
kashakua mke wa mtu hamfanani tena!
hamwezi kuruka tawi moja!!
 
Si akiingia kwenye ndoa tu.. Automatically iko hivo binadamu hubadilisha marafiki kila anapopiga hatua flani kwenye maisha..

Mfano hata wewe marafiki zako wa Primary hawakuwa marafiki zako ulipokuwa Sekondari.. Huko ulianzisha urafiki na watu wengine wapya, hivyo hivyo ulipoenda High School baadhi ya marafiki wa Secondary uliwapoteza.. Ulivyotoka High School kwenda Chuoni ulianzisha urafiki na watu wengine huko chuoni na wale wa High School taratibu walianza kuwa strangers tena. Na ulipotoka chuo ukapata kazi huko kazini ulipata wengine wapya na wale wa chuoni wengine ulishapotezana nao.. Ndivyo ilivyo hata kwa mwanamke akiingia kwenye ndoa anaenda kukuta ndugu wapya kwenye familia ya mwanaume, marafiki wapya ambao ni marafiki wa huyo mwanaume na ndio hapo anaanza kuuwa urafiki na rafiki zake kabla ya kuolewa.. Tena kama hukuwa workmate wake ndio usahau kabisa..
 
Kama huamini basi kaa kimya,ila huu ni ukweli ulio wazi kabisa.

Unakuta msichana alikuwa ni rafiki yako mkubwa ambaye mnaishi kama kaka na dada na mnasaidiana kwenye shida na raha.Ila akishaolewa tu basi na urafiki unaishia hapo,hata simu ukipiga hapokei wala sms hajibu as if kabla ya kuolewa hakuwa na watu anaojuana nao kwanini inakuwa hivi?

NB: Simu hapigiwi usiku wala asubuhi sana,maana ni mke wa mtu.
Mkuu mshukuru Mungu kakuepusha na balaa,mme wa huyo binti anaweza kufikiri kitu kibaya unafanya na mkewe,anaweza kuandaa wahuni akawalipa pesa wakaja kupasua MARINDA yako prururururururu,na wakimaliza wanakupiga picha na kuzituma kwenye mtandao.
 
Si akiingia kwenye ndoa tu.. Automatically iko hivo binadamu hubadilisha marafiki kila anapopiga hatua flani kwenye maisha..

Mfano hata wewe marafiki zako wa Primary hawakuwa marafiki zako ulipokuwa Sekondari.. Huko ulianzisha urafiki na watu wengine wapya, hivyo hivyo ulipoenda High School baadhi ya marafiki wa Secondary uliwapoteza.. Ulivyotoka High School kwenda Chuoni ulianzisha urafiki na watu wengine huko chuoni na wale wa High School taratibu walianza kuwa strangers tena. Na ulipotoka chuo ukapata kazi huko kazini ulipata wengine wapya na wale wa chuoni wengine ulishapotezana nao.. Ndivyo ilivyo hata kwa mwanamke akiingia kwenye ndoa anaenda kukuta ndugu wapya kwenye familia ya mwanaume, marafiki wapya ambao ni marafiki wa huyo mwanaume na ndio hapo anaanza kuuwa urafiki na rafiki zake kabla ya kuolewa.. Tena kama hukuwa workmate wake ndio usahau kabisa..
Shikamoo
 
Roho inakuuma ulivyokua nae nilimuona kama mke sasa kapata jamaa we unataka msumbua mwache aende zake,baki pke yko
 
Kama huamini basi kaa kimya,ila huu ni ukweli ulio wazi kabisa.

Unakuta msichana alikuwa ni rafiki yako mkubwa ambaye mnaishi kama kaka na dada na mnasaidiana kwenye shida na raha.Ila akishaolewa tu basi na urafiki unaishia hapo,hata simu ukipiga hapokei wala sms hajibu as if kabla ya kuolewa hakuwa na watu anaojuana nao kwanini inakuwa hivi?

NB: Simu hapigiwi usiku wala asubuhi sana,maana ni mke wa mtu.

Adui mkubwa wa mwanamke ni shoga zake....atakaribisha mashoga nyumbani kwake kumbe wanamyemelea mume wake ili wampindue na kumcheka. Haya maneno nimeyasikia toka kwa mademu wenyewe.
 
Back
Top Bottom