Kwanini wanawake ni rahisi zaidi kibiashara kuliko wanaume?

Kwanini wanawake ni rahisi zaidi kibiashara kuliko wanaume?

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,566
Reaction score
28,729
Ni rahisi mwanamke kununua bidhaa asiyoihitaji au ambayo hakupanga kuinunua (impulse buying) kuliko mwanaume. Wafanyabiashara nao wamegundua fursa hii adhimu ya kibiashara na wameanza kuitumia ipasavyo kujitengenezea faida kubwa. Wauzaji wengi sasa wamegeukia uuzaji wa bidhaa za kike kwa kuwa wanaona ndizo 'hutoka' zaidi kuliko bidhaa za kiume. Utafiti nilioufanya unaonyesha kwamba wafanyabiashara wengi huuza bidhaa za kike kama vile nguo, viatu, urembo, losheni, nk kuliko bidhaa za kiume.

Udhaifu mwingine wa kina mama ni kwamba hawajui ku-bargain. Sio rahisi mwanamama/dada kuhoji bei au kuomba punguzo--akitajiwa bei tu, huingia kwenye kipochi chake cha fedha akachomoa noti na kulipia bidhaa au huduma.

Wamachinga wanaotembeza bidhaa za mkononi (hawkers) hujinufaisha zaidi kupitia kwa wanawake. Bidhaa ambayo mmachinga angemuuzia mwanaume kwa Tsh 1,000 huiuza bidhaa hiyo hiyo kwa mwanamke kwa Tsh 10,000--tena bila mnunuzi huyo wa kike kuomba discount!

Ni kwanini hasa hali hii iko hivi? Tujadiliane.
 
Wanawake tunapenda kushop ila kwenye kuomba kupunguziwa nadhan tunaongoza mie huwa naomba punguzo
 
Mmmh Kwa Wanawake Njaa Hawa Wakitanzania Niwajuaye Au Wapi?
Nenda Kachunguze Tena ?
 
Kuna wadada wanajua sana kuomba kupunguziwa. Utawasikia "...ai wewe ai jamani nikupe elfu 10 badala ya 45 jamani we kaka..."
 
Kuna wadada wanajua sana kuomba kupunguziwa. Utawasikia "...ai wewe ai jamani nikupe elfu 10 badala ya 45 jamani we kaka..."

me huwa najifanya kama naondoka hapo kimoyon nakua nakihitaj hapo atakwita haya dada kwan we una sh ngapi tuongee biashara
 
Ngoja nikatafute makande kwanza naona njaa inauma!!
 
Back
Top Bottom