Kwanini wanawake na wanaume hawachanganyikani msikitini?

Kama hakuna Aya au hadithi ni wao tu wamejiongeza sasa kwa nini badala ya kuwa na vyumba tofauti isiwe ni chumba kimoja tu ila kila jinsia inakaa upande wake?
Zamani ilifanyika hivyo na hata baadhi ya miskiti inafanyika hivyo...

unajua watu wasichokijua unapotaja uislamu unataka madhehebu mengi sana..Tofauti na mawazo ya watu walio nje
 
Matatizo yataanza pale mwanamke akiinama kuswali, mana hakuna mwanaume atakayekaa mbele ๐Ÿ˜Ž
Wanajaa chumba kimoja, wanaume kushoto na wanawake kulia.
 
Ni kweli Kuna makanisa mengi tu wanawake wanakaa upande tofauti na wanaume, nilikuwa nategemea jambo kama hili pia misikiti badala ya wanawake kutengewa kwenye chumba tofauti kabisa.

Hata hivyo mfano wako wa hekalu sio sahihi kwa sababu Ukristo na Uyahudi ni dini tofauti kabisa.
 
Mkuu unajihangaisha tu kutoa haya majibu,
Aina ya mleta mada lengo lao kuu hua ni kukashifu na sio kuuliza ili kujua.
 
Umeona ile mada wanawake wenu wanashambuliwa kwa kuvaa nusu uchi kanisani ukaja kujifariji huku sio?
Wote ni wanawake wetu, sisi sote ni Waafrika kwanza na tunaunganishwa kama ndugu na Uafrica wetu kwanza, dini ni jambo la pili au la tatu huko kama ilivyo siasa, ushabiki wa mpira n.k
 
hata nyuma wanakaa , hujawai bahatisha swala yeyote ya sikukuu viungani mkuu?
 
Hivi kwa muktadha wa dini, kipimo cha imani si ndio majaribu?

Hivi mtu huitwa mshindi kwasababu amemshinda mpinzani au kwasababu ameepushiwa mshindani?

Utasemaje una imani thabiti ikiwa ni muoga kuya-face majaribu?

Hii inaenda sambamba kwa moja kwa wale wanaomini funga zao zinaweza kuharibika ikiwa tu watu wengine watakuwa huru kula mbele yao.
 
Hakika dini zina contradictions nyingi na kubwa sana, ila ndio hivyo binadamu nao wan cognitive dissonance ya hali ya juu sana.
 
Wanawake wanaweza kuswali chumba kimoja na wanaume ila wataswali nyuma yao
Kuna maeneo kama Msikiti wa Makkah wanawake na wanaume wanaswali eneo moja ila wanatenganishwa tu na na barriers kuonesha mipaka yao
Nia ni kuleta modesty na kutoleta temptation na distraction wakati wa swala

Ukienda mbali zaidi, mafundisho ya dini hayaruhusu mchanganyiko usio wa lazima kati ya wanawake na wanaume ambao hawana mahusiano ya kindugu au ukaribu (mahrim)

Kuna baadhi ya nchi hasa za kiarabu ambazo kwenye public transport kama taxi za mchangio,( kwa Tz ni kama ilivyo bajaj) bus, train wanatenganishwa, kwenye foleni za banks pia wanawake na wanaume wana foleni tofauti, kwenye public schools na colleges pia kuna vyuo au madarasa tofauti
Hata nyumba za waarabu wengi kuna sebule 2, moja ya wanawake na nyingine ya wanaume

Kwa upande mwengine, Makanisa ya Eastern Orthodox mf Ethiopia wanafanya hivyo pia na hata Dar kuna kanisa la Father Nkwera wanafanya hivyo, nimeshuhudia kwa macho yangu wanawake na wanaume wanatenganishwa maeneo
 
Binafsi nadhani waislam wapo sahihi kabisa kutenganisha wanaume na wanawake, kwanza ni ile nature ya ibada yao, kuinama na kuinuka multiple times wakati wa kufanya ibada kunaweza kuwa kigezo cha kwanza kabisa, lakini pia kuondoa vishawishi vya macho. Huku kwa wakristo hata humu watu wengi wamekiri kuondolewa utulivu na usikivu kwa muingiliano wa hizi jinsi mbili.
 
Chukua mfano wa mjane mwenye senti chache.
Hapo ndiyo utajua kwenye sinagogi wanaume na wanawake waliabudu pamoja na walikuwa wanaonana.
hamna haja ya maelezo mengi. ni sheria tu za kibinadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ