Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 34,961
- 80,247
Afadhali alikuskia akakuelewa huyo....Kawaida sana,wanawake wengi wanawapendaga wale pasua kichwa,mwisho wa siku wanaangukaga sehemu mbaya sana.
Mimi nina mtoto wa Mama yangu mdogo ,tulikuwa tunakaa nae home,alitaka kufanya upuuzi kama huo,kulikuwa na vijana wawili mmoja jamaa namjua ni fighter hana hela nyingi kivile lkn anajua kutafuta hela wapili jamaa mmoja sharobaro sound nyingi full vimodo.
Sasa yy alikuwa anampenda huyu mvaa vimodo,nilivyoona kwanza nika kaa nae chini nikamwambia katika wale wanaume wawili anayekupenda kweli ni yule fighter,huyu mvaa vimodo atakuharibia maisha na nilibidi niwe KUWADI kwa yule jamaa figher huku nikimkazia yule mvaa vimodo asipate nafasi za kuonana na dada yangu mixer kumpiga mikwala.
Kweli nilifanikiwa na jamaa baada ya mwaka kaleta mahari,wamefunga ndoa.Sasa huyu mvaa vimodo kaenda kuvunja ndoa ya mtu,jamaa kamwacha mke wake,yule mke akaenda kupanga na kuendelea na maisha yake,yule dogo akaamua akaseleleke ,kwa kuhamia kwa yule mke wa mtu na kasha mzalisha.Mtu mwenyewe kazi hana yupo yupo ana kazi ya kubadilisha nguo kama mkongo.
Sasa siku ndio nikamwita dada yangu nikamwambia kuhusu yule mvaa vimodo aliyekuwa anampenda,akabaki anacheka.
Dada zangu wanatuumiza wanapotembea na watu wa ajabu ajabu tabu tunapata sisi wajomba,bibi na babu, yaani mpaka hivi sasa kuna watoto wawili wa sister tuna walea sisi na ndio maana sikutaka itokee kwa mama yangu mdogo kwani maisha yake yenyewe na familia yake magumu.
Saa nyingine kaka unafanya kazi isiyo kuhusu ya UKUWADI ili umnusuru dada yako na ww usije beba majukumu yasiyo kuhusu.
Badilikeni muombeni Mungu awape jicho la kuwajua wanaume wa kweli,kwani vijana wengi siku hizi wanapenda NGONO na hawapendi MAJUKUMU.
Ukutane na sharobaro anayejua kudanganya na anapulizia unyunyu na anapata sehemu ya kukopa pesa ya chipsi mayai....
Utatoa ushauri hadi utaambiwa unamtaka mdogo wako maana hata kuskia....