Kwanini wanawake hawapendi wanaume wenye mapenzi ya dhati?

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,128
8,648
Habari,

Leo ningependa kushare nanyi kitu kidogo hasa kupitia mahusiano jambo ambalo sikuwahi kabla huenda nikapata ushauri na hata wengine kujifunza.
Kitabia naweza kusema ni moja kati ya wale wanaume ambao ukiwa nae una uhakika wa kuwa upo salama na upo peke yako.

Kwani uwapo na mahusiano nami uko huru kuja muda wowote kwangu kuhusu simu hata ukisema uondoke nayo we nenda nayo inshort ni muwazi mno,yote inatokana na maisha niliyoyaishi ya bila wazazi especially kwenye uyatima,hivyo nimekuwa nikithamini mno mahusiano ambayo nitaingia kwani huwa nawaonea mno huruma wanawake hasa ukizingatia tabu alizozipata mama yangu kabla ya kufariki nikiwa na miaka 7.

Hivyo nilijiapiza kuwa sitaumiza mwanamke au kumnyanyasa na niliweka kiapo kama nitapata mtoto sitopenda aishi maisha kama niliyoyaishi mimi.
Miaka mitano nyuma nilifanikiwa kuanzisha mahusiano na msichana kutoka mkoa wa Mbeya,kiukweli nilitokea mno kumpenda na nilikuwa loyal kwenye mapenzi yetu,baada ya miezi 6,tulifanikiwa kufungua biashara ya duka.

Biashara ilikwenda vizuri kutokana na uzoefu nlokuwa nao katika biashara,biashara ilivyokuwa nzuri nikapata bahati ya kwenda kujiongeza kielimu huku nikimuacha mwenzangu aendelee na biashara kwa minajili ya nikimaliza mwaka wa kwanza nikirudi tumalizie hatua nyingine za posa.

Kufupisha tu story ndani ya ile miezi minne ya mwanzo mwenzangu alikuwa ameanza kubadilika mno kiasi kilichoanza kunipa mashaka likizo ya kwanza ilipokwisha nilivyorudi hakuwa yule ambae ninamfahamu kimavazi na hata tabia.Kama mwanaume machale yakanicheza katika kuchunguza chunguza nikagundua kuwa mwenzangu tayari yupo na mtu mwengine nilimtafuta nikaongea nae kuhusu hilo alikataa kata kata pia akawa na jeuri mie bkasema siyo mbaya nikapotezea.

Likizo ilivyokwisha nikarudi zangu masomoni,miezi miwili baada ya kurud masomoni akawa hapatikani wala hana mawasiliano na mimi,Nilivyorudi nikakuta mali za duka zote zimeuzwa kiwanja tulichonunua kauza inshort alikuwa ameuza investment zote tulizokuwa tumeanzisha pamoja.

Hakika nilikonda na kutokea kukonda mno maana nilihisi future yangu imeharibika kabisa zaidi nilipopata habari kuwa anaishi na mwanaume mwengine na ni mjamzito,kutokana na company niliyokuwa nayo kwa dada zangu na hata familia niliteseka na nikakaa sawa nikaamua ku move on.

Aliendelea na maisha yake nami nikaendelea na maisha yangu hadi siku ya juzi nilipokutana nae kariakoo akiuza nyanya na mtoto mgongoni kariakoo.

Sikubahatika kumuona ila yeye ndiye aliyeniona kiukweli alikuwa akilia mno na kuwa kama movie pale sokoni huku akinisihi nimsamehe,kwa ambae ananifahamu ni mtu mwenye huruma mno lakini kila alivyokuwa akilia na kuniomba msamaha nilikuwa namuona kama katuni mbele ya macho yangu watu walinisihi sana nimchukue tukae sehemu tuongee ili kuepusha ile aibu pale,nikafanikiwa kumchukua mpka kwenye kimgahawa hakika aliyapitia mengi sana mateso na hata misukosuko na huyo aliyekuwa nae.

Baada ya maelezo mengi nilimsamehe na aliniomba turudiane tuwe kama mwanzo,Baada ya kuona yuko serious na hilo la kurudiana nikamuomba niende mara moja toilet nilivyofika toilet kuna jamaa nikamuagiza ampelekee elf 10 pale alipo ili alipie bili ya chakula mimi nilivyompotea wala hakujua wala sikumuaga.Kiuchumi siko vizuri sana but huwa najiuliza tu ni kwanini dada zetu mnapopata wabaume wenye mapenzi ya dhati huwa mnatuona kama wajinga?

Tambueni wengine tupo hivyo sababu ya maisha tuliyoyaishi.
 
mkuu upo fresh Sana ingekuwa Kama Mimi ni lazima alipe kwa kile alichonitendea maana nachofahamu Kila ufanyacho kina matokeo fulani Hivyo ambacho ningemfanya ingekuwa ni matokeo ya kile alichonitendea!!.. maana Kuna binadamu wanajifunza kuishi badala ya kuishi.
 
kiukweli niliisha hakuna kitu kinauma kama kugundua unasalitiwa ilihali unajizuia kwa ajili ya mwenzako na mwisho hakuna kitu kinauma kama kutapeliwa kama ilivyontokea kwenye kiwanja changu na duka
 
Habari,

Leo ningependa kushare nanyi kitu kidogo hasa kupitia mahusiano jambo ambalo sikuwahi kabla huenda nikapata ushauri na hata wengine kujifunza.
Kitabia naweza kusema ni moja kati ya wale wanaume ambao ukiwa nae una uhakika wa kuwa upo salama na upo peke yako.

Kwani uwapo na mahusiano nami uko huru kuja muda wowote kwangu kuhusu simu hata ukisema uondoke nayo we nenda nayo inshort ni muwazi mno,yote inatokana na maisha niliyoyaishi ya bila wazazi especially kwenye uyatima,hivyo nimekuwa nikithamini mno mahusiano ambayo nitaingia kwani huwa nawaonea mno huruma wanawake hasa ukizingatia tabu alizozipata mama yangu kabla ya kufariki nikiwa na miaka 7.

Hivyo nilijiapiza kuwa sitaumiza mwanamke au kumnyanyasa na niliweka kiapo kama nitapata mtoto sitopenda aishi maisha kama niliyoyaishi mimi.
Miaka mitano nyuma nilifanikiwa kuanzisha mahusiano na msichana kutoka mkoa wa Mbeya,kiukweli nilitokea mno kumpenda na nilikuwa loyal kwenye mapenzi yetu,baada ya miezi 6,tulifanikiwa kufungua biashara ya duka.

Biashara ilikwenda vizuri kutokana na uzoefu nlokuwa nao katika biashara,biashara ilivyokuwa nzuri nikapata bahati ya kwenda kujiongeza kielimu huku nikimuacha mwenzangu aendelee na biashara kwa minajili ya nikimaliza mwaka wa kwanza nikirudi tumalizie hatua nyingine za posa.

Kufupisha tu story ndani ya ile miezi minne ya mwanzo mwenzangu alikuwa ameanza kubadilika mno kiasi kilichoanza kunipa mashaka likizo ya kwanza ilipokwisha nilivyorudi hakuwa yule ambae ninamfahamu kimavazi na hata tabia.Kama mwanaume machale yakanicheza katika kuchunguza chunguza nikagundua kuwa mwenzangu tayari yupo na mtu mwengine nilimtafuta nikaongea nae kuhusu hilo alikataa kata kata pia akawa na jeuri mie bkasema siyo mbaya nikapotezea.

Likizo ilivyokwisha nikarudi zangu masomoni,miezi miwili baada ya kurud masomoni akawa hapatikani wala hana mawasiliano na mimi,Nilivyorudi nikakuta mali za duka zote zimeuzwa kiwanja tulichonunua kauza inshort alikuwa ameuza investment zote tulizokuwa tumeanzisha pamoja.

Hakika nilikonda na kutokea kukonda mno maana nilihisi future yangu imeharibika kabisa zaidi nilipopata habari kuwa anaishi na mwanaume mwengine na ni mjamzito,kutokana na company niliyokuwa nayo kwa dada zangu na hata familia niliteseka na nikakaa sawa nikaamua ku move on.

Aliendelea na maisha yake nami nikaendelea na maisha yangu hadi siku ya juzi nilipokutana nae kariakoo akiuza nyanya na mtoto mgongoni kariakoo.

Sikubahatika kumuona ila yeye ndiye aliyeniona kiukweli alikuwa akilia mno na kuwa kama movie pale sokoni huku akinisihi nimsamehe,kwa ambae ananifahamu ni mtu mwenye huruma mno lakini kila alivyokuwa akilia na kuniomba msamaha nilikuwa namuona kama katuni mbele ya macho yangu watu walinisihi sana nimchukue tukae sehemu tuongee ili kuepusha ile aibu pale,nikafanikiwa kumchukua mpka kwenye kimgahawa hakika aliyapitia mengi sana mateso na hata misukosuko na huyo aliyekuwa nae.

Baada ya maelezo mengi nilimsamehe na aliniomba turudiane tuwe kama mwanzo,Baada ya kuona yuko serious na hilo la kurudiana nikamuomba niende mara moja toilet nilivyofika toilet kuna jamaa nikamuagiza ampelekee elf 10 pale alipo ili alipie bili ya chakula mimi nilivyompotea wala hakujua wala sikumuaga.Kiuchumi siko vizuri sana but huwa najiuliza tu ni kwanini dada zetu mnapopata wabaume wenye mapenzi ya dhati huwa mnatuona kama wajinga?

Tambueni wengine tupo hivyo sababu ya maisha tuliyoyaishi.
Brother pole sana universal rule says that opposite attracts maana take no kwamba if you are decent you are more prone to land on hopeless woman and viceversa
 
pole mkuu ,sijui km nimeilewa hii topic ila sometimes tunapenda wanaume physically aggressive as its a sign of security/protection.....ukiwa mpole ni sign ya weakness....

niliona mahali pia wanawake tunapenda bad boys sababu ya personalities zao..dont care attitude shows bad boy is not scared of life,which strangely this appeals to us..lol
 
Kawaida sana,wanawake wengi wanawapendaga wale pasua kichwa,mwisho wa siku wanaangukaga sehemu mbaya sana.

Mimi nina mtoto wa Mama yangu mdogo ,tulikuwa tunakaa nae home,alitaka kufanya upuuzi kama huo,kulikuwa na vijana wawili mmoja jamaa namjua ni fighter hana hela nyingi kivile lkn anajua kutafuta hela wapili jamaa mmoja sharobaro sound nyingi full vimodo.

Sasa yy alikuwa anampenda huyu mvaa vimodo,nilivyoona kwanza nika kaa nae chini nikamwambia katika wale wanaume wawili anayekupenda kweli ni yule fighter,huyu mvaa vimodo atakuharibia maisha na nilibidi niwe KUWADI kwa yule jamaa figher huku nikimkazia yule mvaa vimodo asipate nafasi za kuonana na dada yangu mixer kumpiga mikwala.

Kweli nilifanikiwa na jamaa baada ya mwaka kaleta mahari,wamefunga ndoa.Sasa huyu mvaa vimodo kaenda kuvunja ndoa ya mtu,jamaa kamwacha mke wake,yule mke akaenda kupanga na kuendelea na maisha yake,yule dogo akaamua akaseleleke ,kwa kuhamia kwa yule mke wa mtu na kasha mzalisha.Mtu mwenyewe kazi hana yupo yupo ana kazi ya kubadilisha nguo kama mkongo.

Sasa siku ndio nikamwita dada yangu nikamwambia kuhusu yule mvaa vimodo aliyekuwa anampenda,akabaki anacheka.

Dada zangu wanatuumiza wanapotembea na watu wa ajabu ajabu tabu tunapata sisi wajomba,bibi na babu, yaani mpaka hivi sasa kuna watoto wawili wa sister tuna walea sisi na ndio maana sikutaka itokee kwa mama yangu mdogo kwani maisha yake yenyewe na familia yake magumu.

Saa nyingine kaka unafanya kazi isiyo kuhusu ya UKUWADI ili umnusuru dada yako na ww usije beba majukumu yasiyo kuhusu.

Badilikeni muombeni Mungu awape jicho la kuwajua wanaume wa kweli,kwani vijana wengi siku hizi wanapenda sana NGONO,lakini hawapendi MAJUKUMU.
 
Mimi pia ilinitokea ishu kama hiii. Lakini nilishindwa kumsamehe, tulipotezana miaka 4 hivi, naye alinifanyia mambo ya ajabu yakutisha mno! Ni mtu wa mbeya.
Siku ya siku akanitafta kwa kuulizia mpaka akafika kazini kwangu, amechakaaa ameisha na watoto pacha wawili!!!analia turudiane!!
 
Pole sana mkuu, ningependa kufahamu nini kilimtokea huyo dada mpaka kufikia hapo alipo
baada ya kumdanganya wakauza kila kilichopo dukani na kiwanja pamoja na mali nyingne wakaenda kuishi mwanza alipokuwa anakaa jamaa,baada ya miezi miwili akampa mimba mwanamke katika maisha yao yote hela walokuwa nayo mwanaume alikuwa anatumia tu bila ya kuinvest kwa chochote baada ya miezi mitano mwanaume alianza kubadilika kiasi cha kumletea mpaka wanaume wengine humo humo walipokuwa wamepanga basi kuna mengi sana alikuwa akimfanyia mwisho wa siku akamkimbia huku akimuacha kodi ya nyumba wakiwa wanadaiwa,aliongea vizuri na mwenye nyumba akapewa chumba cha uani awe anapanga huku akiwa amebakia na kitanda tu kwani kabla mwanaume hajamkimbia aliuza kila kitu kasoro kitanda wakati anarudi anakuta hakuna kitu na jamaa hapatikani,basi baada ya kupewa chumba cha uani akawa ni mtu wa kufanya kazi za kumwagilia matofali na hata kulima huku akiwa na mtoto wa mchanga mambo yalivyozidi ikabidi tu aombe msaada wa lori kurudi kwao baada ya kurudi kwao wazee wake wakawa hawamtaki maana alivyoondoka alitoroka kutokana na wazaz wake walikuwa wananitambua na walimkataa huyo mwanaume akiyekuwa nae.inshort ni mengi nashndwa kuyaelezea yote
 
Mimi pia ilinitokea ishu kama hiii. Lakini nilishindwa kumsamehe, tulipotezana miaka 4 hivi, naye alinifanyia mambo ya ajabu yakutisha mno! Ni mtu wa mbeya.
Siku ya siku akanitafta kwa kuulizia mpaka akafika kazini kwangu, amechakaaa ameisha na watoto pacha wawili!!!analia turudiane!!
dah mimi mwenyewe ni wa mbeya kyela alikuwa jeuri mno but ndo hvyo ameshakosa yote
 
pole mkuu ,sijui km nimeilewa hii topic ila sometimes tunapenda wanaume physically aggressive as its a sign of security/protection.....ukiwa mpole ni sign ya weakness....

niliona mahali pia wanawake tunapenda bad boys sababu ya personalities zao..dont care attitude shows bad boy is not scared of life,which strangely this appeals to us..lol
you're absolutely right Rebbie,

Jaby'z pita hapa mdogo wangu..!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom