Kwanini wanaume wengi waliooa hawapendi kuvaa pete ya ndoa?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,850
155,800
Nimechunguza, nimetafiti na nimegundua na kuvumbua kuwa wanaume wengi hawapendi kuvaa pete zao za ndoa kwa visingizio mbalimbali, na kuna kundi lingine ndio huwa linatoka nyumbani wakiwa na pete zao za ndoa na wakifika mitaani huzivua na kuzitupia mifukoni.

Cha ajabu ni kwamba, dada zetu wao wanapenda sana kuvaa pete za ndoa, hata ambao hawajaingia kwenye hiyo taasisi takatifu hujivisha wenyewe pete zao za ndoa na kudundika mitaani.

Nauliza tena wenzangu, kwa nini wanaume wengi walio oa hawapendi kuvaa pete zao za ndoa?
 
Mie nijibu kwa upande wa wanawake. Ukiwa na pete ya ndoa unajipandisha grade, kitu ambacho wanaume waliooa hawajastukia manake wao interest yao ni kitoto vya chuo.
Afu wewe umeibukia wapi? Habari za jela?
 
Kwa mwanamke ndoa ni heshima na huwakoga wenzake kuwa kuna mtu kafika bei.

Kwa sisi wanaume ni something else. Si lazima kila mtu ajue kukunja kwako uso na mawazo tatizo ni binadamu uliyemuacha nyumbani

.....kwani nyie wanaume cyo bnadamu pia..?
 
Kuvaa pete it is just a formality. Wangapi wanavaa pete ya ndoa lakini matendo yao ni balaa? Wanaume wengine wanadiriki hata kusema wazi kwa vimada wao kuwa, '' hii pete niliyovaa isikuogopeshe, au nivue ufurahi?''
 
Hahahahaha, hii kali. Kuna rafiki yangu kaoa ila kila saa anapenda kutoa pete na kuichezea. Kuna siku ilipotea ikawa issue kwa madame! bahati ilipatikana, but mke wake akajua tu alivua sababu alikua anawinda (which was not even true).
 
Mie nijibu kwa upande wa wanawake. Ukiwa na pete ya ndoa unajipandisha grade, kitu ambacho wanaume waliooa hawajastukia manake wao interest yao ni kitoto vya chuo.
Afu wewe umeibukia wapi? Habari za jela?

Alaaa kumbe!!
 
Ni huluka ya mtu tu!

Mbona karibia marafiki wangu wote wenye ndoa zao wote wanavaaga?

Tabia ya mtu mwenyewe!
 
sio kweli kwamba 'wengi' hawavai. Wengi wanavaa. Nadhani kuna maeneo ambayo wasiovaa pete zao hupenda kutembelea (mbugani, kwenye wanyama). Nijuavyo mimi kidume ukiwa na pete mawindoni unaashiria 'responsible/matured person' ambayo inaongeza scoring chances.
 
Sina mila ya kuvaa pete yeyote............ !!!!!!!!!!!!!

Thank god Simoooooooo !!!!!!!!
 
Back
Top Bottom