Wakuu, habar za weekend.
Leo naomba kuuliza wanandoa waliopo humu, hata wale ambao bado mabaharia mnakaribishwa sna maana nyie ndo wahanga wakubwa wa hili suala. Mwanzon munakuwa na mapenzi makubwa kwa wenza wenu lakini baadaye mambo yanaharibika.
Kwanini wakati wa mwanzo wa mahusiano mnakua very romantic mpaka mnapelekea ndoa, na baada ya ndoa wengine hata mwaka hujaisha wameshaanza mipango ya kando na wanabadilika kabisaaa, mapenzi hakuna -- yaani "wanabakana" kwenye ndoa zao.
Hao hao wanandoa kila mmoja akipata mchepuko nje ana-partcipate vizuri lakini akija kwa mumewe au mkewe wanaishi kama wazee.
Hakuna mahaba, hata text tu. Huwezi kuta wanandoa wanachat mambo ya mapenzi, sana sana ni inshu muhimu tu. Hakuna hata nakupenda mpenzi, au
I miss u, I love u nk, hakuna hizo vitu, zilishaishaga.
Ndo maana wanawake wanajitahid kutafuta makungwi na kujiunga kwenye magroup ya WhatsApp wanafundishwa namna na kumshika mwanaume akupende, na mwanaume nao wako bize kushinda kwenye mitandao ya kijamii kutafuta company na marafiki wa kike.
Yaan upendo umepoa kabisaa. Yale malovee hakuna kabisa kwenye ndoa zetu. Kabla hamjaoana mlikuwa mnapeana raha mnaridhishana lakini baada ya mwaka mnabaniana unyumba au unapewa kwa masharti huku mkishindwa kuridhishana. Shida nini hapo wakuu?
Wakuu, najua wengi wapo humu na wahanga wa hili tatizo. Je, shida ni nini?
Tunaomba mwanaume zetu mfunguke kero zenu na wanawake wenzangu mfunguke kero zenu ili 2020 tujenge familia bora.
Ndoa bila usaliti, inawezekana. Karibuni!
Sent using
Jamii Forums mobile app