Kwanini wanandoa wengi hawapo "romantic"?

Kwanini wanandoa wengi hawapo "romantic"?

Kisaikolojia, kitu chochote unachowekeza nguvu kukipata, unapokipata akili hudumaa kwa maana ya kuridhika, huwezi kuwa na nguvu ya hisia zilezile kama hapo kabla. Mfano, kama hujawahi kupanda ndege na unatamani kufanya hivyo, si ajabu siku ya kwanza utajipiga ma-selfie kibao kudhihirisha kufurahia jambo ulilotamani. Ikitokea ukawa mpanda ndege mara kwa mara utashangaa kwa nini day one ulikuwa unaji-selfie. Sio tena jambo nafsi kupigania.

Same kwenye kuoana,kila mmoja hufanya jitihada za kumwaminisha mwenza kwamba yeye ndiye bora kuliko wanaume/wake wengine. Katika kufanya hivyo uongo na uraghai ujipenyeza, kuprerend na vitu kama hivyo. Ndoa ikifungwa, kila mmoja amefanikisha hitaji lake, nafsi haioi haja ya kupretend, hakuna jambo la kupigania badala yake unatamani mambo mengine... Huo ndo mwanzo wa kuchuja romantic life yenu. Kumu-hug mwenza anaporudi toka kwenye mishe, ukampokea kwa mahaba huoni sababu! Uchokozi wa kimahaba unapotea mdogo mdogo... Mara sasa mnaanza kuishi na ndugu, wakwe, babies mara kajisaidia mara analia mara anatambaa kuelekea kwenye jiko! Focus ya romance inaisha. Lakini kwa wanaume majukumu yanapofyonza kipato chako na kuanza kuhisi mkeo hajui ku-manage pesa, romance hupotea.

Sasa katika yote hayo, ishu ya mchepuko ikiingilia kati ndo basi kabisa, kwa kuwa ukweli ni kwamba mchepuko is sweet, maana yeye haitatokea kumilikiana, mtaendelea kuhitajiana kisaikolojia mkijaribu kuwa-prove wrong wenza halali... Utamu utamuni.

Anyway, marriage is an art. Lazima awepo mwenye ubunifu kati yenu ili mambo yaende kama mlivyokusudia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mke wangu kabla ya kumuoa tulikuwa tunachat/kupigiana simu mpaka saa saba usiku na kuendelea.
Leo hii tukiingia kitandani saa mbili kamili usiku mpaka saa mbili na dk 1 kashelala siku nyingi.
Hapo kweli utashindwa kutafuta kampani ya mtoto wa chuo jamani?
 
Ndoa ni mchakato kama michakato mingine, kila siku lazima uje na new trick, asa Mama kamzoesha mumewe akirudi lazima aoge, ale ndipo wabanjuane, siku nyingine banjuaneni kwanza, kuleni alafu muoge, siku nyingine muoge, mbanjuane alafu kuleni.

Wanandoa wasizoeane mke lazima amuone mumewe mpya kila siku hali kadharika mume pia kwa mkewe.

COMMENT TAYARI
Kati ya zote hii nimeipenda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina swali kwa mwanaume?
Kwann mwanaume wakishaoa wanashindwa kuhimili game kama mwanzo, nguvu zinawaisha au Hanna mzuka ndan mwaishia kimoja nje kwa mchepuko mnasimamia vidole

Shida nn hapo naomba majibu wanaume

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio nguvu zinaisha.ila tunapiga asubui kimoja jion kimoja.hizo ni game za kawaida tu ila zipo siku za big match au daby hizo ndio mnatundika vitatu fresh.sasa unataka kila siku usiku tatu asubui tatu tutafanya kaz kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoa zinaboa sababu binadamu wengi wanapenda kupata kile ambacho hawana.

Wachache wanaweza jikaza kubaki na walichonacho. Mfano Unanunua simu mpya na kuweka alarm ili uamke mapema, kesho yake alfajiri ikikupigia kelele unaamka unaizima kistaarabu na kufurahia uwepo wake sababu imekuamsha, baada ya miezi tisa simu Ile Ile ikikupigia kelele uamke unavunja protector na screen yake, unajua kwanini? Sababu ushaona haina jipya'. na ndoa ndo hivyo hivyo'

ndoa zinakosa vitu vipya ambavyo wanandoa hawana au hawavipati. Hata kama nyimbo unaipenda sana, ukishaikariri ukaiimba Weeee asubuhi mchana jioni kinachofata ni kuichoka.
 
Tamaduni Za Kiafrika Ndo Kiini Cha Tatizo Mkuu, Dume Ukiwa Romantic Sana Kwa Mkeo Unaonekana Bwege, Unaendeshwa Na Mke Or Umepewa Limbwata.. . Na Utasemwa Kila Kona Ya Mtaa
Ndo Maana Hata Wale Wachache Wanaokua Romantic Huonekana Waajabu Katika Jamii
Kiafrika Ili Uonekane Kidume Lazma Uishi Kibishi Na Mke Tofauti Na Wazungu Wao Kujipendekeza Kwa Wake Zao Na Kuonekana Mabwege Ni Sehem Ya Kushow Love
 
Nilitaka nichangie huu uzi kwa kuunga mkono baadhi ya hoja zilizoletwa, au kwa kutoa mapovu na kuponda kama kawaida, ila badala yake nimeona nizitafakari kwa kina kuona ni jinsi gani mimi binafsi zinaniathiri. Nilichogundua;
1. Nimekua simtendei haki mke wangu. Namchukulia poa sana siku hizi yaani simjali kiviile kama mwanzo. Saa hizi ndio nakumbuka yeye pia alishaniambia hivyo.
2. Mawasiliano yetu yamepungua sana siku hizi. Sisi wote ni wafanyakazi, lakini inaweza kupita siku nzima hatujawasiliana kabisa tukishaachana asubuhi ni mpaka tukutane jioni!
3. Ni kweli majukumu kwa sasa ni mengi, kwahiyo muda wa ku socialize kama zamani hatutengi.
4. Michepuko inanipotezea muda wangu bure na hela, na nafikiri ndio inanipa kichwa cha kutomjali mke wangu kama mwanzo.
5. Nimegundua bado nampenda sana mke wangu. Nimemuangalia weeeeee... (yeye amelala saiz) nimegundua bado nampenda sanaa. Nahisi na yeye bado ananipenda.
6. Nimegundua wote wawili mimi na mke wangu tuna maeneo ambayo tunahitaji kuyafanyia kazi ili kurudisha hadhi ya mahusiano yetu kama mwanzo.

MAAZIMIO
Mimi binafsi naazimia kujirekebisha na kurudisha moyo wangu kwa mke wangu kuanzia LEO! Nimewaza jinsi nilivyomchukua mtoto wa watu kwao kwa ahadi kedekede za kumpenda na kumtunza, kumjali na kuwa nae ktk shida na raha kwakweli naona simtendei haki kabisa! Naahidi kubadilika hatua kwa hatua na kuwa mume bora kabisa kwa siku zijazo. Ee Mwenyezi Mungu nisaidie. 🙏

Asanteni.


Wakuu, habar za weekend.

Leo naomba kuuliza wanandoa waliopo humu, hata wale ambao bado mabaharia mnakaribishwa sna maana nyie ndo wahanga wakubwa wa hili suala. Mwanzon munakuwa na mapenzi makubwa kwa wenza wenu lakini baadaye mambo yanaharibika.

Kwanini wakati wa mwanzo wa mahusiano mnakua very romantic mpaka mnapelekea ndoa, na baada ya ndoa wengine hata mwaka hujaisha wameshaanza mipango ya kando na wanabadilika kabisaaa, mapenzi hakuna -- yaani "wanabakana" kwenye ndoa zao.

Hao hao wanandoa kila mmoja akipata mchepuko nje ana-partcipate vizuri lakini akija kwa mumewe au mkewe wanaishi kama wazee.

Hakuna mahaba, hata text tu. Huwezi kuta wanandoa wanachat mambo ya mapenzi, sana sana ni inshu muhimu tu. Hakuna hata nakupenda mpenzi, au I miss u, I love u nk, hakuna hizo vitu, zilishaishaga.

Ndo maana wanawake wanajitahid kutafuta makungwi na kujiunga kwenye magroup ya WhatsApp wanafundishwa namna na kumshika mwanaume akupende, na mwanaume nao wako bize kushinda kwenye mitandao ya kijamii kutafuta company na marafiki wa kike.

Yaan upendo umepoa kabisaa. Yale malovee hakuna kabisa kwenye ndoa zetu. Kabla hamjaoana mlikuwa mnapeana raha mnaridhishana lakini baada ya mwaka mnabaniana unyumba au unapewa kwa masharti huku mkishindwa kuridhishana. Shida nini hapo wakuu?

Wakuu, najua wengi wapo humu na wahanga wa hili tatizo. Je, shida ni nini?

Tunaomba mwanaume zetu mfunguke kero zenu na wanawake wenzangu mfunguke kero zenu ili 2020 tujenge familia bora.

Ndoa bila usaliti, inawezekana. Karibuni!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila kitu na wakati wake..kuna urafiki, uchumba, ndoa na maisha kwa ujumla..mfano kulea watoto etc....
Kuna mambo yanaingiliana hapa..bila shaka mtazamo wa maisha..life style ya kipindi cha uchumba ni tofauti na ndoa yenyewe..majukumu yanaongezeka, mnazoeana zaidi, mapungufu ya mwenzako unayajua zaidi, ndugu, jamaa, etc....ndo maana tunaambiwa HISIA zinawezapotea au zikayumba lkn upendo wa kweli unabaki palepale tu....Kama uliingia kwenye mahusiano sababu ya hisia ukihisi ndo upendo ndo imekula kwako hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hbr wapendwa
Binafsi nafikiri tunafanya makosa ya kuishi pamoja kabla ya ndoa.(Kuzini).

Tufahamu kuwa maisha ya zinaa siyo halisia,ni ya kuigiza ili kupata kinachotafutwa na pande zote mbili(ke/me).

Baada ya kupata kilichodhamiriwa ,kila mmoja anarudi upande wa uhalisia wa maisha yake ambapo ndipo sintofahamu inapoanzia.

Kinachotokea baada ya kila mmoja kurudi upande wake,ni kuitafuta ile raha iliyokuwa inapatikana before hivyo kwa kuwa wakati wa kabla ya ndoa kulikuwa na mwingine ndipo anapotafutwa na kuendeleza mahusiano.

Ili kuepuka matokeo mabaya na hasa kutesa familia na kutofikia malengo ,ni vyema kujitahidi kumkubali mwenza wako na kuziona kasoro au madhaifu ya mwenza kama maumbile na hivyo kuyakubali kuishi nayo.

Ndoa ni agano,watu wakishaoana watambue kuwa kuna Mungu kati yao na ndiye shahidi wa hilo hivyo usaliti humuudhi Mungu.Hatuna ahadi ni lini tutarejea kwa Mungu hivyo tutathmini matendo yetu kabla ya kurejea kwa Muumba wetu.

Tuishi kwa matamanio na si kwa kuvumilia.Mwenza atamani kuona mwenzi wake akiishi kwa faraja na si kuvumilia maswahibu ya mateso.
Mungu abariki ndoa zetu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chagua chakula kile ukipendacho sana, au hata nguo ile ikupendezayo sana kisha ivae hiyo hiyo kila siku.... ila cha ajabu POMBE haijawahi kukinai hata uipige kila siku kila wakati.
 
Back
Top Bottom