Kwanini wanandoa wengi hawapo "romantic"?

Kwanini wanandoa wengi hawapo "romantic"?

Wanawake ni mashetani
Wakuu, habar za weekend.

Leo naomba kuuliza wanandoa waliopo humu, hata wale ambao bado mabaharia mnakaribishwa sna maana nyie ndo wahanga wakubwa wa hili suala. Mwanzon munakuwa na mapenzi makubwa kwa wenza wenu lakini baadaye mambo yanaharibika.

Kwanini wakati wa mwanzo wa mahusiano mnakua very romantic mpaka mnapelekea ndoa, na baada ya ndoa wengine hata mwaka hujaisha wameshaanza mipango ya kando na wanabadilika kabisaaa, mapenzi hakuna -- yaani "wanabakana" kwenye ndoa zao.

Hao hao wanandoa kila mmoja akipata mchepuko nje ana-partcipate vizuri lakini akija kwa mumewe au mkewe wanaishi kama wazee.

Hakuna mahaba, hata text tu. Huwezi kuta wanandoa wanachat mambo ya mapenzi, sana sana ni inshu muhimu tu. Hakuna hata nakupenda mpenzi, au I miss u, I love u nk, hakuna hizo vitu, zilishaishaga.

Ndo maana wanawake wanajitahid kutafuta makungwi na kujiunga kwenye magroup ya WhatsApp wanafundishwa namna na kumshika mwanaume akupende, na mwanaume nao wako bize kushinda kwenye mitandao ya kijamii kutafuta company na marafiki wa kike.

Yaan upendo umepoa kabisaa. Yale malovee hakuna kabisa kwenye ndoa zetu. Kabla hamjaoana mlikuwa mnapeana raha mnaridhishana lakini baada ya mwaka mnabaniana unyumba au unapewa kwa masharti huku mkishindwa kuridhishana. Shida nini hapo wakuu?

Wakuu, najua wengi wapo humu na wahanga wa hili tatizo. Je, shida ni nini?

Tunaomba mwanaume zetu mfunguke kero zenu na wanawake wenzangu mfunguke kero zenu ili 2020 tujenge familia bora.

Ndoa bila usaliti, inawezekana. Karibuni!


Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisaikolojia, kitu chochote unachowekeza nguvu kukipata, unapokipata akili hudumaa kwa maana ya kuridhika, huwezi kuwa na nguvu ya hisia zilezile kama hapo kabla. Mfano, kama hujawahi kupanda ndege na unatamani kufanya hivyo, si ajabu siku ya kwanza utajipiga ma-selfie kibao kudhihirisha kufurahia jambo ulilotamani. Ikitokea ukawa mpanda ndege mara kwa mara utashangaa kwa nini day one ulikuwa unaji-selfie. Sio tena jambo nafsi kupigania.

Same kwenye kuoana,kila mmoja hufanya jitihada za kumwaminisha mwenza kwamba yeye ndiye bora kuliko wanaume/wake wengine. Katika kufanya hivyo uongo na uraghai ujipenyeza, kuprerend na vitu kama hivyo. Ndoa ikifungwa, kila mmoja amefanikisha hitaji lake, nafsi haioi haja ya kupretend, hakuna jambo la kupigania badala yake unatamani mambo mengine... Huo ndo mwanzo wa kuchuja romantic life yenu. Kumu-hug mwenza anaporudi toka kwenye mishe, ukampokea kwa mahaba huoni sababu! Uchokozi wa kimahaba unapotea mdogo mdogo... Mara sasa mnaanza kuishi na ndugu, wakwe, babies mara kajisaidia mara analia mara anatambaa kuelekea kwenye jiko! Focus ya romance inaisha. Lakini kwa wanaume majukumu yanapofyonza kipato chako na kuanza kuhisi mkeo hajui ku-manage pesa, romance hupotea.

Sasa katika yote hayo, ishu ya mchepuko ikiingilia kati ndo basi kabisa, kwa kuwa ukweli ni kwamba mchepuko is sweet, maana yeye haitatokea kumilikiana, mtaendelea kuhitajiana kisaikolojia mkijaribu kuwa-prove wrong wenza halali... Utamu utamuni.

Anyway, marriage is an art. Lazima awepo mwenye ubunifu kati yenu ili mambo yaende kama mlivyokusudia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umemaliza
 
Practical guidelines to evaluate a potential wife
Angalia sifa zifuatazo wakati unachagua mke mtarajiwa
Nitaeleza kwa kifupi kama ifuatavyo...
Kumbuka herufi hizi...
A B C D E F

Age=Of about your age
Gape lisizidi miaka 10...
B=Beauty anayekuvutia
C=Character Tabia unazozikubali
D=Dignity anayejiheshimu
E=Education .....of about the same level of education.
F= Family ....Of about the same level of family status

Baada ya ku evaluate hizo sifa on a piece of paper ....l insist uwe very honest!!..mkweli na nafsi yako....
Mpe maksi....mfano labda umempa maksi 65%....sasa angalia udhaifu wake uko wapi?? Wapi amepoteza maksi 35??
Kumbuka huwezi kumpata mwanamke ambaye utampa 100%
Utakuwa unajidanganya.......
MASWALI mawili ya kujiuliza
1.Je nitaweza Kuishi na madhaifu yake??
2.Kama siwezi nitayarekebishaje??

NB: kama hayarekebishiki na huwezi kuishi na madhaifu yake...achana naye!!!!! Tafuta mwingine......WAKE WA KUOA WENYE SIFA WAPO...
Nakaribisha MASWALI.. .nitajibu kadri ya uwezo wangu.....lengo ni kuwasaidia wale walio ktk hatua ya kutafuta wake watakao dumu ktk ndoa zao....
shukrani mkuu
 
Mke wangu kabla ya kumuoa tulikuwa tunachat/kupigiana simu mpaka saa saba usiku na kuendelea.
Leo hii tukiingia kitandani saa mbili kamili usiku mpaka saa mbili na dk 1 kashelala siku nyingi.
Hapo kweli utashindwa kutafuta kampani ya mtoto wa chuo jamani?
pole mkuu
 
Nilitaka nichangie huu uzi kwa kuunga mkono baadhi ya hoja zilizoletwa, au kwa kutoa mapovu na kuponda kama kawaida, ila badala yake nimeona nizitafakari kwa kina kuona ni jinsi gani mimi binafsi zinaniathiri. Nilichogundua;
1. Nimekua simtendei haki mke wangu. Namchukulia poa sana siku hizi yaani simjali kiviile kama mwanzo. Saa hizi ndio nakumbuka yeye pia alishaniambia hivyo.
2. Mawasiliano yetu yamepungua sana siku hizi. Sisi wote ni wafanyakazi, lakini inaweza kupita siku nzima hatujawasiliana kabisa tukishaachana asubuhi ni mpaka tukutane jioni!
3. Ni kweli majukumu kwa sasa ni mengi, kwahiyo muda wa ku socialize kama zamani hatutengi.
4. Michepuko inanipotezea muda wangu bure na hela, na nafikiri ndio inanipa kichwa cha kutomjali mke wangu kama mwanzo.
5. Nimegundua bado nampenda sana mke wangu. Nimemuangalia weeeeee... (yeye amelala saiz) nimegundua bado nampenda sanaa. Nahisi na yeye bado ananipenda.
6. Nimegundua wote wawili mimi na mke wangu tuna maeneo ambayo tunahitaji kuyafanyia kazi ili kurudisha hadhi ya mahusiano yetu kama mwanzo.

MAAZIMIO
Mimi binafsi naazimia kujirekebisha na kurudisha moyo wangu kwa mke wangu kuanzia LEO! Nimewaza jinsi nilivyomchukua mtoto wa watu kwao kwa ahadi kedekede za kumpenda na kumtunza, kumjali na kuwa nae ktk shida na raha kwakweli naona simtendei haki kabisa! Naahidi kubadilika hatua kwa hatua na kuwa mume bora kabisa kwa siku zijazo. Ee Mwenyezi Mungu nisaidie. 🙏

Asanteni.
PONGEZI KWAKO MKUU
 
Ukweli ni kuwa asilimia 90% za ndoa nyingi hazina upendo wa kweli,
Wengi wameowana kwa sababu flani flani za maisha ila si mapenzi!
 
Anyway, marriage is an art. Lazima awepo mwenye ubunifu kati yenu ili mambo yaende kama mlivyokusudia.

“Lazima awepo mwenye ubunifu kati yenu ili mambo yaende kama mlivyokusudia”.

Umeongea madini sana nimekubaliana nawe ila hitimisho lako sio suluhisho, hiyo ya ‘ubunifu’ wa mmoja ndio huleta kukinai kwa kukosa ushindani.... huyo mmoja ambaye ‘si mbunifu’ mwanzo alikuwa mbunifu na akichepuka anasifiwa kwa ubunifu.
 
unashauri vipi
Tukishaoana tunatakiwa kwenda sawa na mahitaj ya kila mmoja maana kama tutabak vile km tulivo tutachokana na hvo kuanza kutafuta substitute nje so ni muhimu kuwa mbunifu ili kufanya ndoa iwe paradiso ndogo km maneno matakatifu yasemavyo
 
“Lazima awepo mwenye ubunifu kati yenu ili mambo yaende kama mlivyokusudia”.

Umeongea madini sana nimekubaliana nawe ila hitimisho lako sio suluhisho, hiyo ya ‘ubunifu’ wa mmoja ndio huleta kukinai kwa kukosa ushindani.... huyo mmoja ambaye ‘si mbunifu’ mwanzo alikuwa mbunifu na akichepuka anasifiwa kwa ubunifu.
Ubunifu si kwenye mapenzi tu, kwa kila jambo, mfano, malezi, imani, kukwepa kulipizana nk. Inatakiwa nyote muwe wabunifu ila ni ngumu kutokea ndo maana anabaki mbuñifu mmoja ambaye dhamira yake ni kulinda ndoa idumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani kikubwa ni kuzoeana mnapokua ndani ya Ndoa hata ambao hawajaoana wakaishi kinyumba tu unakuta mapenzi yanakua hayapo tena.

Mnapokaa nyumba moja na kulala chumba kitanda kimoja kuna hali ya kuzoeana na kila mmoja anamchukulia mwenzie wa kawaida tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukishaoana tunatakiwa kwenda sawa na mahitaj ya kila mmoja maana kama tutabak vile km tulivo tutachokana na hvo kuanza kutafuta substitute nje so ni muhimu kuwa mbunifu ili kufanya ndoa iwe paradiso ndogo km maneno matakatifu yasemavyo
nimekupata
 
Back
Top Bottom