Kwanini wanandoa wengi hawapo "romantic"?

Kwanini wanandoa wengi hawapo "romantic"?

Madam vivian original

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2018
Posts
503
Reaction score
998
Wakuu, habar za weekend.

Leo naomba kuuliza wanandoa waliopo humu, hata wale ambao bado mabaharia mnakaribishwa sna maana nyie ndo wahanga wakubwa wa hili suala. Mwanzon munakuwa na mapenzi makubwa kwa wenza wenu lakini baadaye mambo yanaharibika.

Kwanini wakati wa mwanzo wa mahusiano mnakua very romantic mpaka mnapelekea ndoa, na baada ya ndoa wengine hata mwaka hujaisha wameshaanza mipango ya kando na wanabadilika kabisaaa, mapenzi hakuna -- yaani "wanabakana" kwenye ndoa zao.

Hao hao wanandoa kila mmoja akipata mchepuko nje ana-partcipate vizuri lakini akija kwa mumewe au mkewe wanaishi kama wazee.

Hakuna mahaba, hata text tu. Huwezi kuta wanandoa wanachat mambo ya mapenzi, sana sana ni inshu muhimu tu. Hakuna hata nakupenda mpenzi, au I miss u, I love u nk, hakuna hizo vitu, zilishaishaga.

Ndo maana wanawake wanajitahid kutafuta makungwi na kujiunga kwenye magroup ya WhatsApp wanafundishwa namna na kumshika mwanaume akupende, na mwanaume nao wako bize kushinda kwenye mitandao ya kijamii kutafuta company na marafiki wa kike.

Yaan upendo umepoa kabisaa. Yale malovee hakuna kabisa kwenye ndoa zetu. Kabla hamjaoana mlikuwa mnapeana raha mnaridhishana lakini baada ya mwaka mnabaniana unyumba au unapewa kwa masharti huku mkishindwa kuridhishana. Shida nini hapo wakuu?

Wakuu, najua wengi wapo humu na wahanga wa hili tatizo. Je, shida ni nini?

Tunaomba mwanaume zetu mfunguke kero zenu na wanawake wenzangu mfunguke kero zenu ili 2020 tujenge familia bora.

Ndoa bila usaliti, inawezekana. Karibuni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nadhani wengi wetu hufunga ndoa bila kuwa na uhakika kuwa huyu ndie nimpendae kupita wote.

na baadae kuanza kutizama pembeni,
Cha pili ni kupenda vitu vya kidunia kwa mwenza wako na sio akili na mwili wake.

Mfano mali au umaarufu zikiisha unaanza kumuona mbaya.
 
Kwahiyo hapo mkuu ni tamaa, kwamba ametaman mtu wa nje na Kwann ataman kama ww unacheza part zako zote vzr mkuu
Mimi nadhani wengi wetu hufunga ndoa bila kuwa na uhakika kuwa huyu ndie nimpendae kupita wote.

na baadae kuanza kutizama pembeni,
Cha pili ni kupenda vitu vya kidunia kwa mwenza wako na sio akili na mwili wake.

Mfano mali au umaarufu zikiisha unaanza kumuona mbaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana sababu zako zikawa 1% ila sababu kubwa ni wanaume kushindwa kuwaelewa wanawake. Women are very complicated beings. Hasa akishika mimba mpaka kujifungua wanawake wengi huugua ugonjwa wa kichaa cha mimba. Hata baada ya kujifungua wengi ile hali huendelea na wanaume huona wanawake wanajifanya. Iwapo wanaume wangefahamu basi wangeishi na wake zao kulingana na hizo hali na baadaye hurudia ile hali ya kawaida.
Hapana na ndoa zinazovunjia bila watoto?

Kila mmoja anapaswa kumsoma mwenzie na sio mwanaume peke yake.

Bahubali (Prabbas)
Anakwambia mapenzi ni kupenda kile anachokipenda mwenza wako na wewwatakiwa kujifunza kukipenda.

Pia hata kutofautiana kiimani, hufanya mapenz kupungua.
 
Inawezekana sababu zako zikawa 1% ila sababu kubwa ni wanaume kushindwa kuwaelewa wanawake. Women are very complicated beings. Hasa akishika mimba mpaka kujifungua wanawake wengi huugua ugonjwa wa kichaa cha mimba. Hata baada ya kujifungua wengi ile hali huendelea na wanaume huona wanawake wanajifanya. Iwapo wanaume wangefahamu basi wangeishi na wake zao kulingana na hizo hali na baadaye hurudia ile hali ya kawaida.
Mkuu bado point yko haijashiba kwamba mwanaume wanacheat sababu wanawake wanapokua ktk hali ya ujauzito, sasa ujauzito c jambo jema mnakua mnafuraha ya kusubir kijacho ili muitwe baba na mama na mtoto ndio huongeza furaha ya ndoa au unasemaje hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana wengi wanakuwa walishatoa mimba, ukichaa unaendelea kuwepo
Siamini kama mimba inabadili tabia ya mwanamke.
Kisayansi husema hata ikitokea hali hiyo huisha akijifungua.
Na kibiblia hakuna sehemu nimesoma,
wanasema mwanamke hubadilika tabia kisa mimba
 
Uzuri google ina kila kitu, tafuta kichaa cha mimba. Na wewe inawezekana unacho tayari
Mkuu hicho kichaa cha mimba nimekisoma darasani.
Kuhusu vya Google hakuna nisicho kijua,
Hadi tiba yake.
 
Ndoa ili idumu kwanza lazima mkubali kujishusha, kuwajibika nyote wawili pale inapotakiwa, kusikilizana, kushauriana, na mengineyo mengi tu

Hivo vitu vinavyofanyika kabla ya ndoa wengi hufanya tu wakishaolewa huacha sababu aliitaka ndoa na si kuitumikia ndoa sababu amepata ndoa haoni tena haja ya kuendeleza yale

Kuna wengine hujisahau tu ni kiasi cha kurekebishana arudi kwenye reli kwa ufupi ndoa inataka kutumikiwa na kuheshimiwa ili idumu na iwe na amani

Ndoa ina mambo mengi sana ila nyinyi wawili mkiwekeana taratibu za kuishi nayo bas mtaishi vizur tu, kupishana kupo ila ni namna vile wenyewe mnamaliza tofauti zenu

Ndoa ni ya wawili tu unapokosewa mke au mume na mwenzio heri umweleze yan usiwekw kitu rohoni ukalala nacho ukaenda hadithia kwa best au mshikaj unamvua nguo mwenzio

Na tuache kuishi kwa mazoea kwenye ndoa zetu mazoea hujenga tabia ambayo mwisho wa siku n ngumu kuibadili.
 
Hata Mimi huwa nashangaa sana kuhusu mwanamke kubadilika tabia kisa mimba Mimi huwa naona ni maigizo tu,Nina watoto lkn sijawahi kukutana na ujinga kama huo
Siamini kama mimba inabadili tabia ya mwanamke.
Kisayansi husema hata ikitokea hali hiyo huisha akijifungua.
Na kibiblia hakuna sehemu nimesoma,
wanasema mwanamke hubadilika tabia kisa mimba

Sent by Diaspora
 
Back
Top Bottom