Kwanini wanafunzi wa shule za Secondari wanavaa Suruali za rangi tofauti wakati nembo zao zinatosha katika kuwatambulisha? What's the logic behind?

Kampuni binafsi za ulinzi zinazoendesha shughuli zake hapa nchini zimetakiwa kuvaa sare za aina moja.
hii inahusiana nini na wanafunzi?? machinga mbona hawavai unifom kama makondakta?kwahyo wanafunzi na makondakta waache kuvaa unifom wavae vitambulisho kwasababu machinga wameambiwa hivyo?
 
Wakati nasoma O level Azania,Kibasila,Pugu na shule nyingi walikuwa wanavaa khaki. Hawa label zilisaidia kujua shule gani wanatoka.
Tambaza pekee walikuwa na grey shorts. Label zao green na red zilikuwa zinatofautusha group 1 na 2 ambazo wanaingia shule kwa shift.
Ingawa unaona hizo nguo ni rangi tofauti kwa shule mbili tatu ila utakuta rangi hio hio mfano blue ya Azania hata Jitegemee wanavaa blue hio hio kwa mantiki hii label inawatambulisha.
 
Sababu kubwa ni kwamba suala la uteuzi wa sare za shule limeachwa ndani ya mamlaka ya shule na sio la kitaifa. Shule zimepewa mamlaka ya kuchagua rangi za sare kulingana na mazingira huku ikifuata muongozo wa sare pasipo kuwa na masharti ya rangi.
 
All in all , Kila shule ina culture zake....

Hii ishu imekuwepo MIAKA na MIAKA...

Sio Tanzania pekee Ni worldwide....

MY OPINION TUIACHE KAMA ILIVYO....

Nakumbuka MIAKA ya nyuma nikiwa secondary school TULIITWA KUNGURU

TULIVAA SURUALI NYEUSI SHATI NYEUPE

WENZETU WALIVAA SURUALI BLUE SHATI NYEUPE....
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini wanafunzi wa shule za secondary za serikali wanavaa suruali/sketi za rangi tofauti wakati nembo zao zinatosha kabisa katika kuwatambulisha?

View attachment 1657563

Nini mantiki ya kuwa na namna mbili ya kuwatofautisha yaaani kuwatofautisha kwa rangi ya suruali zao pamoja na nembo ya shule husika? Kwanini kusiwe na aina mbili tu ya suruali/sketi za wanafunzi wa secondary.

(1) Sare za wanafunzi wa shule za serikali - Mashati/blauzi zikiwa na nembo ya shule husika.

(2) Sare za wanafunzi wa shule za binafsi - Mashati/blauzi zikiwa na nembo ya shule husika.

View attachment 1657565

MARCH 2018: KAMPUNI BINAFSI ZA ULINZI KUWA NA SARE MOJA
==========
Kampuni binafsi za ulinzi zinazoendesha shughuli zake hapa nchini zimetakiwa kuvaa sare za aina moja ifikapo Januari Mosi mwakani kwa lengo la kuondoa sare ambazo zimekuwa zikifanana na zinazovaliwa na askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Agizo hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii, Mussa Alli Mussa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa kikao kilichowakutanisha wamiliki wa kampuni binafsi za ulinzi.

Kamishna Mussa amesema sare zilizokubaliwa kwa pamoja kati ya Jeshi la Polisi na wawakilishi wa kampuni binafsi za ulinzi zinatakiwa ziwe na rangi ya bluu nyeusi (Dark blue), nyeusi pamoja na mashati meupe kulingana na mazingira ya kampuni inapofanyia ulinzi.

View attachment 1657564
==========

NINAOMBA KUELIMISHWA: Kuna mantiki gani ya wanafunzi kuvaa suruali/sketi za rangi tofauti wakati nembo zinawatofautisha?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Kijana mdadisi sana wewe
 
Shule zingine kila kidato kina uniform rangi tofauti na kingine mfano Ugwasi secondary. Ukimuona hata kwa mbali tu unajua yule ni form one wa shule fulani hivyo tu
 
Huyu mwamba itakuwa kaishiwa madini.Siku hizi sizielewi nyuzi zake
Mkuu, JF ina members zaidi ya 550,000 hivyo siwezi kumfurahisha wala kueleweka na kila mtu boss wangu. Kuna 50% watanielewa na wengine 50% hawatanielewa kama wewe...
 
Huyu mwamba itakuwa kaishiwa madini.Siku hizi sizielewi nyuzi zake mfano kama hii. Lengo lako nini?
Lengo ni kutaka kujua mantiki ni nini kwamba mbona shule ya msingi ni hivi na secondary ni vile. Alafu kumbuka kuwa mimi nipo humu JF kujifunza kupitia akili za watu wengine na sio kuzodoana...
 
Back
Top Bottom