Kwanini wanafalsafa wa kale wa Magharibi walitofautiana juu ya chanzo cha ulimwengu na uhai ?

Kisai

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
27,984
28,102
Historia ya binadamu na ustaarabu wake,inatusimulia na kutilia mkazo juu ya chanzo cha ulimwengu na vilivyomo. Achilia mbali usahihi wa nukuu hizo za kihistoria,hili ni somo kando na hapa halizingatiwi kwa sababu za kielimu na dharura ya muda.

Anasema muandishi wa kitabu "Wanafalsafa wa kale wa Magharibi,uk. 7" alipokuwa anamuarifisha Thales,anasema "Kulingana na Aristoto,Thales alifundisha kwamba viumbe vyote vimekuwepo kutokana na Maji"

Lakini Anaksimanda alipinga vikali wazo hilo la Thales kwamba chanzo cha uhai ni Maji. Anasema tena mwenye kitabu hicho katika ukurasa wa 9, "Sanabu ya upinzani huu ni kwamba maji ni moja ya ukinzani,ambacho msuguano na kumezana kwake lazima ufafanuliwe." Hitimisho lake Anaksimanda kuhusu chanzo cha asili ni kuwa, "....chanzo cha vitu vyote ni kisicho mwisho au hasa kisicho mpaka"(Rejea kitabu Wanafalsafa wa kale wa Magharibi,uk. 9,Stefano Kaombe).

Mkanganyiko huu haukuishia hapo,muandishi anamnukuu Anaksimenesi kwa kusema "Alifundisha kuwa chanzo asili au msingi asili wa vitu vyote ni HEWA",(Rejea kitabu hicho hicho ukurasa wa 10).

Watu wa jumuiya ya Pithagorasi wao wakahitimisha kwa kusema chanzo cha vyote ni namba. (Rejea kitabu hicho hicho uk.12)

Wakafata wanafalsafa kadha wa kadha wapo waliosema ya kuwa "Kuna Mungu mmoja,kati ya miungu na binadamu ,hafanani kabisa na binadamu katika mwili na akili",haya yalisemwa na Khenofanesi.

Kwa kufupisha mada yangu ni kupata majibu ya maswali haya,kwa yeyote mwenye kujua.

1. Kwanini kama wanafalsafa hawa walitofautiana katika kuelezea chanzo cha uhai ? Kama kichwa cha mada kinavyosomeka.

2. Kwanini walifikia mahitimisho haya ? Je waliwakadhibisha mitume ( Waliwapinga kwa kuwasema mitume kuwa ni waongo ?) kwa makusudi au kwa kutokujua ?

3. Au zama zao hapakuwa na mitume na manabii ?
 
Waliwakadhibisha mitume. Falsafa inalazimu kujiuliza uliza na kutumia akili kitu ambacho akili inafeli ni juu ya muumba. Utamjua muumba na ukubwa wake kupitia vitabu vyake na sio akili yako kama watu wa falsafa wanavyotaka.
 
Back
Top Bottom