Kwanini wana CCM wanamuogopa Lowassa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini wana CCM wanamuogopa Lowassa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpanzi, Jan 16, 2012.

 1. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Wakuu baada ya kusoma alichoongea Nyalandu nimeamini kuwa lengo la kutaka Lowasa avuliwe Gamba ni kumuweka nje ya Kinyang'anyiro cha Urais, Sitta, Membe na makundi yao wanamuogopa sana huyu bwana, hata suala la ufisadi wamelitunga ili kumpunguza makali, mi nauliza kama kweli wanakibalika kwa nini wamuogope?
   
 2. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #2
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Simple and clear, kwa sababu hakuna aliyemzidi Lowasa kwa usafi au uchafu - they are all the same, tatizo kubwa, yeye ana njuluku ambazo wengine hawanazo- atawazidi tu, kwa hiyo wanamhofia sana. Wao wangekuwa wasafi, wangeshajiunga na vyama vya upinzani ili wapambane naye vizuri. Kunyukana kwao kikweli ( sio mnyukano wa kusadikika wanaoupeleka kwa nguvu chadema) ni faida kwa Chadema. Full stop.
   
 3. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,897
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  kwa sababu wanatamani wangepata mianya ya kufisidi kama yeye lakini walikosa ndo maana mwakyembe na sitta wanamchukia na kumuogopa lowassa..wote ni mafisadi
   
 4. k

  kuzou JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  jk anaona el si chaguo zuri kwa ushindi wa ccm
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Jan 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hivi ni wana CCM gani wanaomwogopa Lowassa?.. mimi siwajui maana nijuavyo Sitta aliifanya kazi yake vizuri tu ya Uspika, waliobakia ni Secretariat ya chama kina Nnauye na Malima..zaidi ya hawa sioni mtu anayemwogopa Lowassa kama sii wote wanamuunga mkono maana kama kweli walikuwa wanamwogopa asingeweza kubakia mwanachama mkutano mkuu ulopita..
   
 6. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Lowassa anawatisha sana CCM, akitaka uenyekiti anaupata hata kesho, vijana wake wako kila kona hadi vyama vya upinzani, bara na visiwani. Ila wananchi hatumuogopi na sisi ndio wapiga kura wenyewe.
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwa sababu EL ndio potential/tunu pekee iliyobakia ndani ya CCM
   
 8. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hakuna anaemuogopa lowassa zaidi yenu mnaoogopa akivuliwa gamba mtakosa shibe
  OTIS
   
 9. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hawa mwogopi ila wana mheshimu kama PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA 2015
   
 10. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #10
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45

  Kila kikicha wanaimba ufisadi wa Lowasa, Tanzania ni nchi ya tatu kwa kuzalisha dhahabu, Rwanda hawana, Tanzania ni nchi pekee yenye Tanzanite, Rwanda hawana, Tanzania ni nchi pekee yenye Gesi asilia Africa Mashariki, wengine hawana, Tanzania ni nchi pekee yenye ardhi ya kutosha yenye rutuba Afreica Mashariki, wengine hawana, badala ya kufikiria kwa nini tumekuwa maskini pamoja ana rasilimali zetu zote, tunaweka nguvu zetu na muda wetu kupambana na Lowassa, utafikiri yeye ndo chanzo cha umaskini wetu!!
   
 11. Kilahunja

  Kilahunja JF-Expert Member

  #11
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,497
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  umeona eeh
   
 12. m

  mwanamboka New Member

  #12
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wote ni wababaishaji ila Lowassa ni jembe la ukweli!!!!!Membe aende akawe raisi wa MTAMA jimboni kwake lkn Lowassa awe Raisi wa TANZANIA!!!!!!
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Jan 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, unachokiona kama woga, si woga, ni michezo ya kisiasa. wanaweza kuonekana kama wanamwogopa kumbe wanamlia timing na anaweza kujikuta akipigwa dafrao bila kutarajia. lakini kwa upande mwingine, Lowassa naye anajua kuwa wa upande aa pili hawajalala, kwa hiyo na yeye halali, kila mara anazidi kujiimarisha kisiasa na kivingine ili kuhakikisha kuwa utakapotokea mpambano, anaibuka mshindi
   
 14. Ndetirima

  Ndetirima JF-Expert Member

  #14
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 895
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  Wanaogopa wanafikiri akipata urais atawalipizia kisasi kwa mambo yote waliomzushia kwamba yeye ni fisadi na mambo ya kujivua gamba na kumtoa kafara ya Richmond ili kukinusuru chama na mkuu wa kaya. Pia wanaogopa uchapakazi wake na maamuzi yake magumu anayotoaga bila ya kumuogopa mtu yeyote. Nakumbuka enzi zake akitembelea mahali wakuu wa mikoa na viongozi wengine wote walikuwa roho juu wanaogopa kuliko kawaida na waliweka mambo yao na ripoti sawa. Sio sasa hivi viongozi wanajifanyia wanavyotaka, akija Pinda au mkuu wa kaya hakuna anayeshituka wanachezewa ngoma za kwao mambo yanaisha hakuna maswali tena.
   
 15. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #15
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  ccm wanmwogopa kwasababu ana pesa chafu ambazo hazifanyiwi auditing. Pia kwa viongozi wa ccm wanaokaa kwenye vikao vya maamuzi wote wamechafuka kuanzia baba hadi mtoto, hivyo nafsi zao zinawasuta.
   
 16. D

  DOUBLE AGENT Member

  #16
  Jan 16, 2012
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapambe wa Lowassa sasa wahofia afya yake

  Baada ya zoezi la CCM la kujivua gamba kushindwa, Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi ya Richmond, Edward Lowassa, sasa amejitamba kuwa yeye ndiye Rais ajaye wa 2015.
  Watu waliokaribu na Lowassa wameniambia kuwa sasa hivi Lowassa ameshaiweka CCM mfukoni kwake kutokana na utajiri wake mkubwa wa kifisadi ambao umemuwezesha kuwanunua viongozi karibu wote.

  "Sikiliza wewe, wajumbe wengi wa Kamati Kuu wako kwa Lowassa, NEC yote iko kwa Lowassa na zaidi ya asilimia 70 ya wajumbe wa mkutano mkuu wanamtii Lowassa. Hakuna cha kumzuia awe Rais 2015," mmoja wa wajumbe wa timu ya kampeni ya Lowassa alisema.
  "Kikwete alivyoshindwa kutekeleza azma yake ya kujivua gamba imedhihirisha kuwa hana control au authority yoyote CCM. Hiki chama kiko kwenye himaya ya Lowassa."
  Wapambe wa Lowassa wamesema kuwa ameikamata kanda nzima ya Ziwa na Zanzibar ambazo kwa ujumla wake zinawakilishwa na zaidi ya asilimia 50 ya wajumbe wa mikutano ya kitaifa ya CCM.

  "Kitu pekee kitakachoweza kumzuia Lowassa asiwe Rais ni matatizo yake ya afya tu. Huyu mzee yuko very weak, akikushika mkono unatetemeka. Hata akishika kikombe cha chai, nusu ya chai inamwagika kutokana na kutetemeka kwake."
  "Ini lake liko hoi, huyu mzee ni alcoholic sasa ... Anakunywa sana pombe kali, hasa Hennesy."

  Baadhi ya wapambe wa Lowassa wamesema kuwa anaumwa kiharusi (stroke) ndiyo maana alikimbilia kwenda kwa Babu kule Samunge kupata kikombe. Pia Lowassa amekwenda mara mbili kwa mchungaji wa Nijeria, Joshua Emmanuel, katika jitihada zake za kuimarisha afya yake ili atwae uongozi wa nchi na kutimiza lengo lake kuu -- kuwa tajiri mkubwa kuliko wote kwenye bara zima la Afrika.
   
 17. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #17
  Jan 16, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,454
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Hivi bila Lowasa JF Jukwaa la Siasa jua litachomoza kutokea magharibi kuelekea mashariki? Lowasa amejadiriwa kwa mapana hapa JF kuna hoja nyingi zipo humu wala hazijakuwa archives,ni vyema kuzipitia ili kupunguza kujirudia rudia.
   
 18. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #18
  Jan 16, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  The way the cookie crumbles...........:A S embarassed::shock:
   
 19. m

  mimibilly Member

  #19
  Aug 13, 2015
  Joined: Aug 1, 2013
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba kuuliza ccm wanamuogopea nn lowasa??tangua ahamie chadema wamesahau kabisa kama na wao wana makufuli wakumpigia kampeni wao kila siku ni story tu kuhusu lowasa mara hiv mara vile,tuambien nn mchotetemeka kwa yy kuwahama,si ni mgombea tu kama wenu?? Nawashauri fuatilieni mambo yenu the more mnavyowashwa ndo lowasa anavyokuwa strong
   
 20. Cham Bee

  Cham Bee JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2015
  Joined: Feb 10, 2015
  Messages: 3,075
  Likes Received: 1,171
  Trophy Points: 280
  The more the stress of the deffender the more the opportunity of the attacker.Watajikuta wanamuongelea magufuli siku ya kupigwa chini asubuhi 2:30 oct 25...
   
Loading...