Kwanini walimu wengi wanaolewa kulinganisha na sekta zingine

Babumawe

JF-Expert Member
Sep 12, 2014
2,556
2,560
Kuna project tulikuwa tunaifanya ambayo tulikuwa tunazunguka sekta karibia zote. Cha ajabu sekta ya ualimu asilimia kubwa wameolewa ukilinganisha na sekta nyingine, kipi kinafanya waalimu wawe na soko sana tofauti na kada zingine?
Mara ya mwisho walimu walikuwa na 90% ya idadi ya walioolewa wakati sekta ya mwisho ilikuwa bank walikuwa na 25%
What is the reasons behind hii kitu wajameni??
 
Walimu wanadanganyika kirahisi mfano mzuri wengi wamedanganywa wakala manyoya qnet.
 
Mwlm anamuda mzur wa kulea familia na kufanya Kaz yake tofaut na wengne.
Mfano uowe nesi anakuacha usik umelala na mtt ye anaenda shift ya night akijipimia ana nafas ya kukudanganya unfkr yuko job kumbe anabandulia.. Yan mazingra yake tu ya kaz yatakua ni mgogoro na hamuwez kudumu kirahis Kama hamna uvumiliv
 
Kwa mujibu wa wizara ya elimu mpaka kufikia mwaka 2016 Tanzania tulikuwa na idadi ya walimu 332,748. Hii ni zaidi ya 70% ya watumishi wote wa umma na zaidi ya asilimia 50% ukijumuisha na sekta binafsi.

Takwimu kama hizi haziwezi kukupa taswira halisi kama utaziangalia haraka haraka. Kwa kifupi ktk kila wanawake 100 nchini Tanzania kuna asilimia kubwa ya kupata walimu zaidi ya 50 hapa ukijumuisha taaluma zingine zote kuanzia udaktari, uchumi, biashara, uhandisi, sanaa, muziki n.k

Kwa maoni yangu unapotaka kugundua jambo kupitia takwimu kama hizi tumia njia ya kuwatenganisha kimakundi yaani walimu waweke peke yao na kada nyingine fanya hivyo hivyo halafu ndio uje na hitimisho.

Utashangaa kuona labda ukiweka walimu pekee yao walio ktk ndoa wanaweza kuwa ni asilimia ndogo sana ukilinganisha na madaktari. Yaani ktk kila madaktari 10 utakuta 8 wana ndoa ila kwa walimu ktk kila walimu 10 ni wanne tu wenye ndoa.
 
Kwamba hili nalo linahitaji utafiti?
 
Siyo wanaolewa tu, na wakiolewa pia wanadum kwenye ndoa kulinganisha na sekta nyingine.

Taaluma ya ualimu inawapa wanawake "PACKAGE " ya tabia nzuri za kuwafanya waonekane wanawake bora kwa wanaume kwa kuolewa lakini zaidi kudumu kwenye ndoa. Kwahiyo kinachopendewa hapo siyo "ualimu" kama taaluma bali tabia za muhusika alizozipata na anazoendelea kuziishi kupitia hiyo taaluma husika.
 
Back
Top Bottom