Kwanini walimu hawazeeki mapema?

Kwanini walimu hawazeeki mapema?

dexterous

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
2,037
Reaction score
3,145
Habari wanajukwaa,
Kuna ka usemi nilikua nakasikia tangu nikiwa shule O-level ila nilikua siamini eti walimu hawazeeki haraka. Kwa kweli nimekuja kushuhudia na kuchunguza juu ya hilo na kuona ni kweli kwa 100% maana juzi kama bahati nimekuta na mwalimu wangu ambaye alinifundisha vidudu(chekechea) sikuweza kuamini kwani haikunipa tabu kumtambua nilivyomuona mara moja niliweza kumfahamu.

Kiukweli yupo vilevile na bado anafundsha na ameweza kufungua center yake mwenyewe sio huyo tu na wengine wengi kuanzia primary mpaka secondary sijajua kiiman kwamba mwenyezi Mungu amewabarki ama vipi au niikwanini inakuwa hivyo.

NAWASILISHA
 
Dah sikutegemeaga kama Kuna mtu atajiuliza swali kama mimi!! Mwalimu alienifundisha primary mpaka leo yuko vizuri, why? Mi nafikiri ni kwa sababu wanaamka kila siku asubuhi, wanapigwa na kale kabaridi.

Pia wanakuwa na maisha ya kati ya kibongo bongo
 
Nikweli kabisa walimu hawazeeki mapema,,nimeanza shule nina mwaka 1994 nikamkuta mwalimu tumbo ni mkuu shule ya msingi nyanza na hadi leo ni mwalimu mkuu pale nyanza na bado anadundika tu.
 
nakumbuka nilimuona mwalimu wangu chekekea a.k.a vidudu kuna ukweli hapo mpaka nilimshangaa
 
Ni Kazi isiyo na stress sana hasa unashinda na watoto na unajua kukaa na watoto its fun lakini pia walimu wengi ni waadilifu wasio na matukio ya kiarifu...nawakilisha pipo
 
Kwa Mtazamo wangu Wanamuziki ndiyo hawazeeki mapema kutokana na kuwa na furaha sana katika kazi yao ya muziki/burudani. Hawana stress

Juzi tu nimemwona mwanamuziki mkongwe mzee Zoro ametupia pensi kama sharo wa umri wa miaka 30 hivi.
 
Habari wanajukwaa,
Kuna ka usemi nilikua nakasikia tangu nikiwa shule O-level ila nilikua siamini eti walimu hawazeeki haraka. Kwa kweli nimekuja kushuhudia na kuchunguza juu ya hilo na kuona ni kweli kwa 100% maana juzi kama bahati nimekuta na mwalimu wangu ambaye alinifundisha vidudu(chekechea) sikuweza kuamini kwani haikunipa tabu kumtambua nilivyomuona mara moja niliweza kumfahamu.

Kiukweli yupo vilevile na bado anafundsha na ameweza kufungua center yake mwenyewe sio huyo tu na wengine wengi kuanzia primary mpaka secondary sijajua kiiman kwamba mwenyezi Mungu amewabarki ama vipi au niikwanini inakuwa hivyo.

NAWASILISHA

nature ya kazi yao inaruhusu kwanza mda mwingi hawana stress wanashinda na wanafunzi tu pia usimama na kufundisha kila cku hivyo kufanya viongo vyao kufanya zoezi..tofauti na wafanyakzi wa ofcn mda mwingi ni makelele full stress tena muda mwingi ni kukaa tu
 
Kwa Mtazamo wangu Wanamuziki ndiyo hawazeeki mapema kutokana na kuwa na furaha sana katika kazi yao ya muziki/burudani. Hawana stress

Juzi tu nimemwona mwanamuziki mkongwe mzee Zoro ametupia pensi kama sharo wa umri wa miaka 30 hivi.
Hahaha mkuu m naona wana mziki wana ma sttess kibao maana kila siku mtu unawza namna gani utawafurahisha mashabiki na usiombe umetoa nyimbo alfu watu wasiipende ndo kabisa stress kibao n unakuta n gharama ulizotumia ni majanga
 
Ikiwa kazi yako ni kucheza na watoto automatically unafanya mazoezi!

Harafu walimu wengi ni watu wa kipato cha chini (kati kwenda chini), hivyo utakuta misosi na starehe zinazozeesha haraka hawakutani nazo sana.
Kumbe starehe zinazeesha mapema kuliko maisha magumu? Mbona kama hii kitu ina-contradict aisee?
 
Mfumo wa maisha pia unachangia hawana hela za anasa na wanatumia muda mwingi kwenye kuandaa madesa na tuitions etc.

Anyway walimu wangu walevi wa gongo nishawazika sana tu pamoja na wale vicheche.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom