Kwanini wakulima watoroshee mazao yao nje?

Kwanini wakulima watoroshee mazao yao nje?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,300
Reaction score
17,577
Hata kama tunasema hali ni safii kwa kutumia njia tofauti lakini hali halisi inapingana na kauli zetu. Kwanini tunatumia nguvu nyingi kulaumu, kuzuia na kuchukulia hatua watu wanaokwenda kuuza mazao yao wenyewe nje ya nchi? Kwanini wanahangaika kiasi hicho kwenda kuuzia mbali mazao yao?

Tumuogopeni Mungu, maana yeye ni mjuaji ya yote hata yale tusiyoyasema.
 
Kama Waganda wanatoa malipo mazuri sisi tunashindwa nini?baadaye tunawaonea wakulima ambao wanatumia jasho lao
 
Ccm n chama cha wakulima na wafanyakazi cjui ni wanchigani?
 
Hizo nguvu zingetumika kuwawezesha wakulima hakika mkulima angekombolewa
 
Sera zeta za agro economy ni mbovu. Hatuhaweza kumuwekea mkuluma mfumo bora wa soko la mazao yake na bado tunamwambia kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa.
 
Hizo nguvu zingetumika kuwawezesha wakulima hakika mkulima angekombolewa
Badala ya kuwapongeza polisi wanaosadia wakulima warudishe jasho lao walilopoteza kwenye kilimo tunawafukuza kazi.

Nadhani mwenye macho haambiwi tazama. Kule Ruvuma, Arusha na Tanga bei ya gunia la mahindi ni sh. 20,000 wakati bei ya cement ni sh. 16,000 kwa mfuko na bei ya sukari ni sh. 3,000 kwa kilo. Hivi kuna dhambi gani kama mkulima akiyapeleka mahindi yake sehemu yoyote duniani akapate zaidi ya sh. 20,000 baada ya kutoa gharama zote za kulifikisha huko? Hivi ni mjinga gani yuko tayari kupoteza muda, nguvu na pesa kusafirisha mazao yake nje ya nchi na kuaacha soko kijijini kwake?

Lazima tuna matazizo makubwa sana, tunataka kulazimisha kushusha mfumuko wa bei kwa kuwakandamiza chini wakulima. Tunasahau kuwa iko siku wakulima wanaweza kususa kulima mazao hayo na kusababisha mfumuko wa bei kupanda mara 1000 kwa kuagiza chakula nje ya nchi. Nimewasikia wakulima wakisema silimi tena mahindi mengi msimu ujao, silimi tena mbaazi, silimi tena ufuta.
 
Kutumbua watendaji sio tija,mazao yataendelea kutoroshwa tu Maana hakuna awezaepambana na nguvu ya pesa, cha msingi waangalie kwa nini wakulima wanapenda kuuza nje kuliko ndani.Wawaboreshee mazingira ya bei nzuri kuliko nje,hakuna mkulima atakaeingia gharama tena ya kuuza nje. Suala la kahawa ya kagera kutoroshea Uganda halikuanza leo, watafute ufumbuzi wa kudumu.
 
kwani mkulima wa kahawa ana tofauti gani na mfanyakazi anayelipwa mshahara? mbona mfanyakazi anaamua wapi akafanyekazi apate ujira mzuri? Kama ndani ajira hakuna kwanini uzuie wasio na ajira wakatafute ajira zinakopatikana? Hata wachezaji wa mpira akina Samatta wametumia mfumo huohuo wa kutafuta maslahi mazuri nje baada ya Simba kushindwa kumpa pesa anayohitaji.
 
Back
Top Bottom