Mkuu hoja zako zinaibua maswali makubwa sana. Wewe unasema kwamba Waisraeli (Wayahudi) wanamuamini Yesu na kwamba wao ndio taifa teule. Kwa maana nyingine unatuambia kwamba kama Wayahudi ni taifa teule la Mungu, basi ilibidi sisi wengine wote (Wakristu) tufuate kile wanachofanya wao kwasababu after all wao ndio waanzilishi na wao ndio wanauelewa hasa ukristo kuliko sisi watu baki! Sasa maswali yanakuja:
1. Kwanini Wakristo wengine wanasali tofauti na Wayahudi wakati Ukristo umeanzia kwao?
2. Nani yupo sahihi kati ya Wayahudi na Wakristo wengine?
3. Upi ushahidi (nje ya Biblia) unaoonyesha hawa watu ni taifa teule la Mungu?
4. Je, Waisraeli wa kweli ni wepi? Je watu wanaojiita Waisraeli leo ndio wale kizazi cha Yakobo?
Maswali yako matamu sana kiongozi pili nakupongeza kwa kutokuwa na mihemko👏👏
Swali la kwanza Kwanini wakristo wanasali tofauti na wayahudi wakati ukristo umeanzia kwao?
Ukristo Kiongozi umeanzia Mjini Roma na waanzilishi wake ni kanisa katoliki.
Swali la pili Nani yupo sahihi kati ya Wayahudi na wakristo wengine?
Wayahudi wana namna yao ya kuabudu nasi wakristo tuna namna zetu za kuabudu ila tunaabudu kitu kimoja nacho ni mungu, Katika uyahudi kubatizwa ni lazima, nasi wakristo ni lazima.
Katika uyahudi wana adhana nasi wakristo tuna kengele (si madhehebu yote), Majibu ya hapa kidogo yanaweza kuwa na ukakasi ama magumu kwa kuzingatia Imani huwezi kuwa mkristo kama huamini Yesu alikufa na kufufuka na akapaa mbinguni n.k na huwezi kuwa muyahudi halisi kama unasali kwa kuacha kichwa wazi na humtumikii "Yahweh" ambaye ndio huyo waliemuuwa (YESU).
Swali la tatu upi ushahidi (nje ya Biblia) unaonyesha hawa watu ni taifa teule la Mungu?
Hapa ndipo unapokuja kupata maana ya neno Imani majibu ya hapa yanategemea imani yani mambo yasiyo bayana na yatarajiwayo.
Nakupa mfano Qur'an tunaambiwa ilishuka kutoka mbinguni je tukiomba ushahidi wa nje ya Qur'an tutaupata? Jibu ni HAPANA hivyo ni imani ya maandiko matakatifu ambayo yanatueleza sehemu nyingi sana kuwa israel na wana wake ni taifa teule na wamebarikiwa.
Swali la nne Je waisrael wakweli ni wapi? Je watu wanaojiita waisrael waleo ndio kizazi cha yakobo?
Majibu ni rahisi Waisrael wakweli ni wazawa wa ardhi iliyobarikiwa Mungu aliibariki ardhi ya israel.
Hawa wanaoijiita waisrael waleo ndio ni kizazi cha Yakobo na Hapana sio kizazi cha Yakobo kwanini naandika hivi?
Katika kizazi cha Yakobo hakuna waislamu Israel kuna waislamu hivyo hawa si kizazi chake katika taifa hilohilo kuna wagalatia ambao ndio kizazi cha yakobo (Wayahudi) kwa hiyo kiongozi majibu ya Ndio na Hapana yote ni sawa Waislamu baba yao ni Ishmael