Hivi ni kwanini tunasema taifa la Israel kuwa ni taifa teule na kukubari hata mabaya inayofanya dhidi ya jamii nyingine kuwa ni sawa.
Mbona hatujafuata dini ya Wayahudi kama kweli ni taifa teule ina maana hata wanachoabudu ndicho sawa maana wao mpaka leo wanafuata torati.
74.2% ya Waisrael ni Wayahudi, 17.4 ni Waislamu na 2.0% ndo wakristo huku 4.4% ni madhehebu mengine.
Kwa mantiki hiyo unaona kwamba zaidi ya asilimia 90 siyo Wakristo na hawaamini kile tunachokiamini.
Sasa iweje tuwaite taifa teule tubishane sana kuwatetea huku hatudfuati wanachokiamini wao?
Neno Israel ambalo pia ni jina la Taifa linatokana na jina la baba wa watoto 12 wa kiume aliyeitwa Israel. Hapo awali aliitwa Jacob kabla Mungu hajampa jina hili la Israel.
Sababu zinazolipa Taifa la Israel Utaifa Teule ni moja kuu.
Yesu ambaye wakristo tunaamini ndiye Mkombozi wa Ulimwengu alitokea kwenye ukoo huo.
Yaani Mungu aliamua Yesu azaliwe kwenye ukoo wa Israel.
Hao wengine wachache wanaoishi hapo kwa mujibu wa Bible hawana chao kwenye ardhi hiyo.
Kuhusu kwa nini wakristo wasiwe wayahudi ni kwamba.
Njia kuu ya kwenda mbinguni ni kumkubali na kuamini kwamba Yesu alikufa na kumwaga damu ili awaokoe wanadamu.
Kwa sababu waliotekeleza mauaji ya Yesu ni wayahudi wenyewe ambao pia bado hawajamkubali Yesu wakristo tunawaombea siku moja watamkubali. Hii inafanya tiwapende japokuwa bado hawajaamini.
Bible inatuambia kwamba wayahudi kumkataa Yesu wa kweli wakidhani bado hajafika ni kwa muda tu. Siku za mwisho watamkubali.
Waweza jiuliza tu mwenyewe ikiwa kuuliwa kwa Yesu Kristo ni baraka kwa ulimwengu.
Nani angelitekeleza hilo? Je huoni kwamba huo ni mpango wa Mungu mwenyewe.