Kwanini Wakristo wanadai Israel ni taifa teule?

Kwanini Wakristo wanadai Israel ni taifa teule?

Si kweli umepotoka na unazidi kupotoka, Biblia ya kiyahudi inamtambulisha Yesu kama "Yahweh " ambako hata Biblia yetu sisi wakristo inamtambua kwa majina mengi likiwemo hilo.

Article mbalimbali za mitandaoni zinajaribu kuwatenganisha na ukristo ni Kweli wanaabudu kitofauti wana mafundisho yao.

Ila wanaabudu kwenye mahekalu, wanamtambua Yesu pamoja na kazi zake alizozifanya Katika Biblia ya kigalatia ambayo ndio ya kiyahudi inampa utukufu sana Yesu.

Wakati nilipohudhuria semina ya wayahudi wao wanasali sana hakuna tofauti na walokole wanatenda miujiza kilokole kupitia jina la yesu japo wana misimamo yao kama hawaweki sanamu lolote la mtu yoyote wala kiumbe chochote kwenye mahekalu yao zaidi ya michoro ya rangi.

Kingine ni marufuku kwa mwanamume au mwanamke kusali wakiwa vichwa wazi hata Biblia yetu sisi wakristo inazungumzia hilo.

Nchini israel watu hawakatwi mikono hawanyongwi wala kupigwa mawe kuna mambo mengi sana nilijifunza
1104710

1104713
1558532404698.png
1558532501633.png

Angalia hizo sehemu nilizo highlight kwenye screenshot. Tena hiyo aish.com ni website ya dhehebu la kiyahudi kote wanaeleza kwanini hawamkubari Yesu kama Masiah sijui wewe umeudhulia kongamano la Wayahudi gani ndugu.
 
Nilitazama mahojiano fulani ya waisraeli wa sasa. Jamaa wanasema wao bado wanamngoja masihi.
Ndiyo, wanamfahamu Yesu (wanamwita Yeshua) kama mwana mmoja aliyeibuka akawa dhidi ya mafundisho ya msingi ya kiyahudi, akawa rabbi anayefundisha imani zake binafsi.

Nionavyo: Wakristo wanaipapatikia Israel sababu ndo mapokeo waliyopewa na viongozi wao wa kiimani.
Yes wewe umeongea ukweli Dripboy anachanganya. Hawa Wayahudi wanamuona Yesu kama alikuwa muongo muongo tu Masiah kwao hajaja bado
 
Hivi ni kwanini tunasema taifa la Israel kuwa ni taifa teule na kukubari hata mabaya inayofanya dhidi ya jamii nyingine kuwa ni sawa.
Mbona hatujafuata dini ya Wayahudi kama kweli ni taifa teule ina maana hata wanachoabudu ndicho sawa maana wao mpaka leo wanafuata torati.
74.2% ya Waisrael ni Wayahudi, 17.4 ni Waislamu na 2.0% ndo wakristo huku 4.4% ni madhehebu mengine.
Kwa mantiki hiyo unaona kwamba zaidi ya asilimia 90 siyo Wakristo na hawaamini kile tunachokiamini.
Sasa iweje tuwaite taifa teule tubishane sana kuwatetea huku hatudfuati wanachokiamini wao?
Hizo data zako ungeweka na link ingependeza
 
Hizo data zako ungeweka na link ingependeza
hizi ni baadhi tu ya sources
 
hizi ni baadhi tu ya sources
Ngoja wataalaamu wa mambo ya Dini za Wakoloni waje
 
Taifa teule wakimaanisha wao wataenda mbinguni wote kwasababu Mungu wao alishawateua.
 
Yes wewe umeongea ukweli Dripboy anachanganya. Hawa Wayahudi wanamuona Yesu kama alikuwa muongo muongo tu Masiah kwao hajaja bado
Nchi zenye wayahudi wengi duniani ni Israel, France na U.S nazungumza kitu nachokifahamu kwa kuzingatia misingi ya imani
 
View attachment 1104710
View attachment 1104713View attachment 1104710View attachment 1104713
Angalia hizo sehemu nilizo highlight kwenye screenshot. Tena hiyo aish.com ni website ya dhehebu la kiyahudi kote wanaeleza kwanini hawamkubari Yesu kama Masiah sijui wewe umeudhulia kongamano la Wayahudi gani ndugu.
Mimi ndiye ninakwambia sasa Yesu kwa lugha ya kiyahudi hutajwa kama "Yahweh" soma Biblia yao achana na source za ajabu kama Wikipedia ambazo hata wewe waweza kuhariri hizo taarifa.

Sifa za "Yahweh" na namna anavyoabudiwa ukizijua haki ya mungu utaachana na hii mada yako.
 
Kuna kitu kinaitwa Imani, Imani ni mambo yatarajiwayo wakristo tunaamini Biblia huwezi kuwa mkristo kama hujafanya au huamini yafuatayo[emoji116]

(1) haujabatizwa kwa maana wewe sio mkristo aliyezaliwa upya (born again Christian).
(2)Hauamini kama Yesu alikufa na akafufuka siku ya tatu na akapaa mbinguni.
(3) Hauamini utatu wa Mungu baba mwenye enzi yani Baba mwana na roho mtakatifu.
(4) Huamini kama Israel ni nchi iliyobarikiwa Biblia inaitaja sana israel na sifa zake.
N.k

Wayahudi hawafuati Torati za Mussa tafuta Biblia yao inaeleza, kinachowatofautisha wayahudi na wakristo si Mafundisho bali Itikadi wayahudi wana namna yao ya kuabudu n.k ila wanafuata mafundisho ya Yesu.

Nimebahatika kuhudhulia semina zao Dodoma walikuwa wametoka ufaransa wanasali kama walokole na imani zao haziyumbishwi na jambo la kushangaza wanasali kupitia YESU.
We jamaa ni muongo sijapata kuona [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ....hivi hauoni aibu kudanganya uma?
 
Israel iliyokuwa taifa teule sio hii ya sasa. Hawa wa sasa ni wazungu wahuni kutoka Ulaya na America.
 
Yesu ni tapeli na hajawahi kuexist..
Hata hao wayahudi hawamtambui..ni hawa wafia dini wakiafrika wamekazania vitu wasio vijua..
Makaburu kweli wamefanikiwa ku brainwash akili nyeusi
 
Yesu ni tapeli na hajawahi kuexist..
Hata hao wayahudi hawamtambui..ni hawa wafia dini wakiafrika wamekazania vitu wasio vijua..
Makaburu kweli wamefanikiwa ku brainwash akili nyeusi
Sentensi ya Kwanza Nini ?? yaani mtu flani Ni tapeli alafu hajawai kuwepo..?
 
Biblia imetoka Israeli na bila shaka hayo maandiko yote tunayoyasoma yanatoka huko kwenye hiyo hiyo biblia ndio pameandikwa Israeli taifa teule na pendwa..

Miaka 1000 ijayo unafikiri kanisa la Gwajima litakuwa na wafuasi wangapi na hao watakaoamini na kufuata wataambiwa Gwajima alikuwa nani?? Yule mama naye kule Mwanza baada ya miaka 1000 historia ya kanisa lake itamtaja kama nani hakuna uwezekano biblia yake ikasomwa baada ya 1000 na wafuasi wake... Wahindu, Mabudha nk nk...
 
All the content uongo pure!
Hunijui Sikujui, Mimi ni mtu ninayefuatilia sana Dini na pale inapotokea mikutano ya injili katika mji ninaoishi bila kujali ni wa dhehebu gani huwa nahudhuria.

Huwezi kuita maudhuhi ya mwenzako ni ya kiongo pasipo kuwa na ushahidi unanikosea Heshima mimi nina itikadi za kihuni ila muhuni mwenye kujitambua.

Sijabahatika kufika taifa la Israel hata mara moja ila nimebahatika kuhudhuria Semina tano za wayahudi ambao mpaka leo wapo wawili wanaendesha shughuli zao za NGOs hawa ni wafaransa kwa utaifa walipokuja mara ya kwanza wakiwa wote (8) walifundisha Uyahudi ni nini? Kwanini unatofautishwa na ukristo? Uyahudi una misingi gani? Je wayahudi hubatizwa? Je Yesu yumo katika mafundisho yao? Ni baadhi ya mafundisho tuliyoyapata.

Tanzania hasa kanda ya kati kuna wayahudi wakitanzania kabisa na wanafanya maombezi kwa wenye uhitaji huo, Lugha waliyokuwa wakiitumia katika Semina yao ni Kiingereza na kifaransa na kwa bahati nzuri nazijua lugha zote.

Kwa kumalizia ungeuliza na si kuniita mimi ni MUONGO umenifedhehesha sana nilitaka kukujibu kimazingira nayoishi ila nimekustahi TAFADHALI SANA mzee sitarajii unikosoe kwa namna hiyo HUNIJUI SIKUJUI
 
Back
Top Bottom