Kwanini wakina dada hawawezi kutofautisha kati ya kuchezewa na kuchezeana?

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,612
21,346
Unapopata msichana kwanza huwa anauliza "je utanioa au unanichezea tu?"
Hata kama ana digrii tatu za lugha bado anashindwa kabisa kutofautisha kati ya kuchezewa na kuchezeana.

Inakuaje unasema nakuchezea wakati;
  1. Wote tunapata raha
  2. Simu na vocha nimekununulia
  3. Ukipata jamaa mwenye hela najua kabisa utanikimbia
  4. nk
Swali linatakiwa kuwa "je utanioa au tunachezeana tu?" haya ni maoni tu jamani
 
Kumpotezea muda inakuja pale ambapo una mtu wako wa ndoto zako wa future zako kisha unapata mwengine unakaa nae kwa muda mrefu bila kumtaarifu

huyu anajiaminisha kabisa ndio wewe pekee siku za siku unamwambia nenda nina wangu
hapo hujui kawakataa wangapi waliokua na nia kawakwepa wangapi waliokua wakweli

Hapa ndio kuchezewa inapokuja
vinginevyo ni kuchezeana
 
Kumpotezea muda inakuja pale ambapo una mtu wako wa ndoto zako wa future zako kisha unapata mwengine unakaa nae kwa muda mrefu bila kumtaarifu

huyu anajiaminisha kabisa ndio wewe pekee siku za siku unamwambia nenda nina wangu
hapo hujui kawakataa wangapi waliokua na nia kawakwepa wangapi waliokua wakweli

Hapa ndio kuchezewa inapokuja
vinginevyo ni kuchezeana


Umenena mkuu!
 
Mahusiano yenye ukweli na uwazi tangu day 1 hayanaga mambo ya umenichezea... sijuwi umenipotezea mda wangu.... umenizibia ridhiki... Dawa ni kuwa mkweli kwa mwenzako asijekuwa na matarajio yasiyotekelezeka
 
Nadhani ni msemo wengi wameuzowea,sababu kama unadhani mtu anakuchezea au anakupotezea mda wako kwanini usiseme NO mapema........
 
unapotezewa mda.. muda wa nini wakuolewa au wakupata raha? tengeneza njia upate mlango wakutokea dada usitangulize lawama..shida nyingine mnatanguliza sana maslahi yenu kiasi hata rafiki yako wa kiume anaanza kukuona wewe ni kero, jifunzeni moyo wa uvumilivu sio kile unachotaka unapewa kwa mda huo huo!hapana.
 
nawasuburi waje! mii kuna mmoja alinambia nimempotezea muda wake, nikamwambia "tumepotezeana muda" akawa mbishi, nikamuambia hata huku kubishana, bado tunapotezeana muda!
Ha ha ha mkuu umenichekesha sana.
Hizi kauli zinatokana na udhaifu wa kike tu, kwamba always wao ni victims na hakuna kingine
 
Kama ukimuahidi ndoa halafu umzingue then hapo umempotezea mda!! But kama ni one night stand au mechi za kirafiki aseme wampotezea mda au hamkupeana ahadi zozote basi hapo hakuna cha kupotezeana. Si wajua ahadi ni deni
 
Back
Top Bottom