Wadau nimefarijika sana na hii thread, kwani imenigusa moja kwa moja kwa kile ambacho nimeanza kukifanyia kazi leo hii tarehe 1.04.2012. Ni study/research itakayonichukua muda wa miaka 3 hivi. Kwa ufupi ni kwamba ninafanya study yangu katika eneo hili. Nina Background ktk construction na Business studies na kwasasa proposal yangu inahusu Entrepreneurship Sustainability and Trade Challenges in Tanzania's Construction Industry; focusing in growth of Local Tanzanians Firms. Bado naweka mambo sawa, halafu nitawasiliana nanyi wadau ili tuweze kuona nini hasa tatizo na nini kifanyike ili kuwasaidia Wazalendo wenzetu kufikia malengo yao na ya jamii ya Watanzania. Pia, matokeo ya study yangu nitayaweka hapa ili kuweza kusomwa na wengine wengi. Hili nitalifanya ikiwa ni pamoja na kuwapa links za International Journals zitakazoweza kuwajenga wale watakaokuwa na hitaji.
NB: Ndudu zangu wakati ukifika nitakapohitaji msaada wenu wa mawazo hasa kwenye dodoso, tafadhali naomba muwe tayari kusaidia.
Natanguliza shukrani.
RDI.